Polisi Afukuzwa Kazi kwa Kumbaka Mtuhumiwa wa Kike katika kituo cha polisi

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,090
Points
2,000

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,090 2,000
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitoa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambacho pia kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.
Wakati huohuo, katika kijiji cha Malangali Barabara ya Mbeya-Iringa, Wilaya ya Mbarali gari aina ya Nissan Patrol lilimgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa mwili wa marehemu bado haujafamika na mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Chimala Mission na kwamba juhudi za kuutambua mwili wa marehemu na mahali anapotoka zinaendelea.
 

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
22,194
Points
2,000

Crashwise

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
22,194 2,000
polisi ccm weka mbali na wake zetu..kumbe usiombe mkeo akamatwe wanaenda kumfanya kitoweo kweli serilikali hii haina cha kujivunia cha maana..
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
10,607
Points
2,000

Ukwaju

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
10,607 2,000
ali,baka au walipeana hebu angalieni umri wao kwanza
Huyu Mama mwizi ni hatari naomba Mahakama iangali mwenendo mzima km kuna utata wa Rushwa ya ngono au alimlazimisha
Mimi nina wasiwasi na huyo Mkuu wa Kituo cha Polisi Tunduma, huenda huyo Mdada analipa na alikubali mwenyewe yaishe ahakikishiwe nafuu ya Kesi yake
 

Kiba

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2012
Messages
456
Points
195

Kiba

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2012
456 195
Baba mzazi wa askari ampendi mwanae " anasema kitendo si cha ungwana alichofanya mwanae" je hana uhakika kafanya kweli au huyo mwizi wa kike alikubali then akajeuka ili kujenga umaarufu kuwa yeye ni mkali hadi askari kadata.?
 

Ally Kombo

Verified Member
Joined
Nov 11, 2010
Messages
11,434
Points
1,225

Ally Kombo

Verified Member
Joined Nov 11, 2010
11,434 1,225
ali,baka au walipeana hebu angalieni umri wao kwanza
Huyu Mama mwizi ni hatari naomba Mahakama iangali mwenendo mzima km kuna utata wa Rushwa ya ngono au alimlazimisha
Mimi nina wasiwasi na huyo Mkuu wa Kituo cha Polisi Tunduma, huenda huyo Mdada analipa na alikubali mwenyewe yaishe ahakikishiwe nafuu ya Kesi yake
Unaweza kupeana na mwenzio ndani ya ofisi yako ? Yaaani kula mzigo ndani ya meza yako ya ofisi ?!
 

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
23,042
Points
2,000

idawa

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
23,042 2,000
Huyo askari ameonewa, angeshitakiwa kwa kufanya mapenzi muda wa kazi na kwenye kituo cha kazi.!
 

CRN

Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
60
Points
0

CRN

Member
Joined Oct 24, 2012
60 0
Hapo kuna kitu kilichoandaliwa,mwanamke mwenye umri huo hawezi kubakwa na akakaa kimya bila kupiga kelele bwana,hao watakuwa walikutwa wakifanya mapenzi na kwa kulinda maadili ya kazi wameamua kumfukuza ili kuonyesha uwajibikaji,hata hivyo hawakupaswa kumfukuza kwani hayo ndo mavuno ya walichokipanda,Jeshi la polisi limepoteza sifa kutokana na kuwa na viongozi waliolewa madaraka pamoja na malupulupu ya CCM na kusahau majukumu yao,kwanza huyo dogo ametekeleza vyema dhana ya POLISI JAMII kwa kujamiiana na mwanajamii,big up polisi wetu.
 

kamkoda

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Messages
395
Points
195

kamkoda

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2012
395 195
Siasa mbaya kweli, jambo hili ni la kinidhamu kazini mpaka magazetini? Leo hii kunawatu wanavunja amri hii ya sita kwenye maofisi mchana kweupeeeeeeee!!!! tena na watendaji wakuu wa sehemu husika iwe ofisini ama nje wakati wa saa za kazi, ziandikwe na hizo, askari wa miaka 22 damu yake inachemka mbaya!!!...Samahani lakini ni maoni!
 

Forum statistics

Threads 1,390,122
Members 528,091
Posts 34,043,135
Top