Polisi acheni kutumika kuminya haki ya kikatiba ya vyama vya upinzani

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Kauli yenyewe ni hii hapa nainukuu kama ilivyo " kama Wapinzani wanakusanyika na wanafanya mambo yao ya Kisiasa bila kufanya fujo yoyote na hayo wanayoyafanya yana tija fulani ya Kisiasa na Kidemokrasia kwa nchi yetu hakuna haja ya kuwafukuza au kuwazuia kwani kuwafanyia hivyo itakuwa ni sawa na kuwanyanyasa wakati na wao wana haki kama wengine " mwisho wa kuinukuu.

TANGAZO LA SERIKALI NA. 215 la tarehe 12/10/2007


SHERIA YA VYAMA VYA SIASA
(SURA YA 258)

-------------
KANUNI
(Zimetungwa chini ya fungu la 22(b))

KANUNI ZA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA ZA
MWAKA 2007

SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI

1. Kanuni hizi zinaitwa kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa Mwaka 2007 na zitaanza kutumika mara tu baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali.

2. Kanuni hizi, zitatumika Tanzania bara na vilevile Tanzania Zanzibar

3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale muktadha utaelekeza vinginevyo- “chama cha siasa” maana yake ni chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kwa mujibu wa Sheria.
“Msajili” maana yake ni Msajili wa Vyama vya Siasa aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria pia itajumuisha Naibu Msajili na Msajili Msaidizi;
“Sheria” maana yake ni Sheria ya Vyama vya Siasa.

SEHEMU YA PILI
HAKI YA CHAMA

4.–(1) Kila chama cha siasa kitakuwa na haki zifuatazo-

(a) Kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kwa wananchi kwa kufuata sheria na kanuni za nchi;
(b) Kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar;
(c) Kujadili na kushindanisha sera zake na zile za chama cha siasa kingine kwa lengo la kutaka kukubalika na wananchi;
(d) Kuwa na uhuru wa kutafuta kuungwa mkono na wapiga kura; na
(e) Kila Chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa;
(2) Wakati wa uchaguzi wowote utakaoendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, kila chama cha siasa kitakuwa na haki na uhuru wa kushiriki na kushirikishwa na Tume ya Uchaguzi na au chombo chochote chenye mamlaka katika kufanya uchunguzi na kupata matokeo katika jambo au suala lolote linalohusu uchaguzi.

SEHEMU YA TATU
WAJIBU WA CHAMA

5.-(1) Kila Chama cha Siasa kitakuwa na wajibu wa kutunza maadili chini ya kanuni hizi kwa: -
(a) kukieleza kwa wanachama wake ili kuongeza uadilifu wa kisiasa ndani na nje ya chama cha siasa;
(b) kulaani, kuepukana kuchukua hatua zitakazofaa ili kuzuia au kuepusha vitendo vya vurugu, uvunjaji wa Amani au ukandamizaji wa aina yeyote ile;
(c) kutotumia vyombo vya dola kukandamiza na kutoa vitisho kwa chama cha siasa kingine kwa manufaa yake;
(d) kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni ya uongo na kuhusu mtu yeyote au chama cha siasa chochote;
(e) kufanya mkutano wa kisiasa na maandamano bila kufanya vurugu kwa mujibu wa sheria za nchi;
(f) kulaani na kupinga-
(i) vitendo vyenye kuashiria ukandamizaji;
(ii) matumizi ya lugha ya matusi
(iii) vitendo vya kibabe na vurugu
(iv) matumizi ya nguvu ili kujipatia umaarufu wa chama au sababu yeyote ile;
(f) Kuepuka kuteremsha bendera iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria, kuharibu kwa namna yeyote ile kitu chochote ambacho ni ishara au nembo inayotumiwa na chama kingine kama sehemu ya utambulisho wa chama hicho;
(g) Kuepuka kushawishi kwa kutoa rushwa kama kichocheo ili kupata upendeleo au heshima kwa nia ya kufanikisha malengo;
(h) Kuepuka kutumia mamlaka. Rsilimali za serikali, vyombo vya dola, au wadhifa wa kiserikali, kisiasa au ufadhili wa nje ama wa ndani kwa namna yeyote ile ili kukandamiza chama kingine.
(i) Kuepuka vitendo vya ubaguzi wa rika, kabila, jinsia, dini na mahali alipozaliwa mtu yeyote ikiwa ni jamii au asili Fulani kwa kufanikisha malengo ya siasa; na
(j) Kuheshimu maamuzi halali yaliyofanywa kwa pamoja na vyama vyote.
(2) Kwa kuzingatia Sheria, kila chama cha siasa kitakuwa na uhuru wa kushirikiana na chama cha siasa kingine kwa nia njema kwa ajili ya kupanga vikao, mikutano ya hadhara kwa pamoja au maandamano kwa wakati mmoja kama kwamba mambo hayo yamefanywa na chama cha siasa kimoja au bila kuvunja sheria za nchi.

NB: Hii ni sehemu tu ya Sheria ya Vyama vya siasa NCHINI TANZANIA

MANI lusungo Tetty Maserati MENGELENI KWETU tindo Salary Slip Elli Erythrocyte Quinine Isanga family Nyemanze Root Retired Ciril NIYOMBARE BONGOLALA Mag3 Nzi othiambo
 
Tumeandika katiba wenyewe

Tumeipitisha wenyewe

Cha ajabu serikali hiyo hiyo inageuza utekelezaji juu chini

This must be shithole.......hatuiheshimu, hatujiheshimu na hatujuwi tunafanya nini kwanini
 
Huu ni ushahidi tosha kati ya vyama vya upinzani na chama cha wahuni ni chama kipi kinataka kuvuruga nchi na kuiingiza kwenye machafuko makubwa yanayowza kabisa kusababisha umwagaji wa damu mkubwa.

Tumeandika katiba wenyewe

Tumeipitisha wenyewe

Cha ajabu serikali hiyo hiyo inageuza utekelezaji juu chini

This must be shithole.......hatuiheshimu, hatujiheshimu na hatujuwi tunafanya nini kwanini
Bandiko zuri sana Mkuu..
Mtu akikwambia "akili zako kama Polisi wa Tanzania.. " usikubali, jitetee maana hilo ni TUSI kubwa sana kufananishwa na hayo majamaa.
Hii nchi si ya kikatiba tena..ya ki dikteta tu
 
kinya26022018.jpg
 
Back
Top Bottom