Polisi acheni kusambaza mbinu za uhalifu

Malilambwiga

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
485
296
Jana kupitia taarifa za habari kwa njia ya televisheni na radio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro alionyesha kukamatwa kwa majambazi wanane waliokutwa na silaha za moto mbili aina ya shortgun pump action.

Aidha mbali na silaha hizo pia mkuu huyo wa polisi alionyesha watuhumiwa hao kukutwa na madawa ya kulevya ambayo kwa maelezo yake yalikuwa yamefungwa (kusokotwa) kwa kutumia karatasi/kurasa zilizochanwa kutoka ktk biblia takatifu.

Kwa mtazamo wangu haikuwa sahihi kwa kamanda kutaja kurasa za biblia kudaiwa kutumika kufungia madawa ya kulevya.

Kitendo hicho ni sawa na kusambaza mbinu mpya kwa wahalifu ambao bado hawajaigundua na hivyo kupelekea uhalifu wa aina hiyo kutumia kurasa za biblia kufungia madawa ya kulevya kuenea nchi nzima.

Pamoja na polisi kutoa taarifa za uhalifu kwa umma lakini pia polisi inatakiwa kuchuja ni kipi kiwasilishwe kwa umma kwa kuzingatia IMPACT kwa jamii.

Kuonyeshwa hadharani kwa kurasa za kitabu kitakatifu kudaiwa kutumika kufungia madawa ya kulevya kunaweza kupelekea vitabu hivyo kununuliwa kwa wingi na wahalifu na hivyo likawa ni tatizo jingine ktk jamii.

Silaha zile mbili zilizoonyeshwa zingetosha kama lengo la polisi lilikuwa ni kufikisha habari kwa jamii.
 
Ccp huwa inachukua wengi waliofeli form 4 na darasa la saba sasa ulitegemea nini hapo wakikamata madawa au pembe za ndovu wanataja thamani yake hapo si kuhasisha vijana wawe punda na wengine kuingia msituni
 
Jana nilishangaa sana hawa polisi wetu mambo wanayofanya ni aibu tupu .hayo madawa ya kulevya wanayokamata kila siku wanayapelekaga wapi?hao wahusika huwa wanachukuliwa hatua gani?mtu anakamatwa na madawa ya kulevya utasikia uchunguzi unaendelea duh mambo mengine kujadili ni kuumiza kichwa bure
 
Polisi inafichua maovu siyo kuficha ! Kila mbinu inayotumiwa na waarifu ni lazima ifichuliwe! Mode of operandi
 
Naomba ufafanuzi kidogo mtoa mada, tatizo liko wapi kwa kamanda wa polisi mkoa wa morogoro kutoa taarifa jinsi wauza madawa ya kulevya wanavyotumia kitabu kitakatifu cha mungu kufungia hayo madawa, hapa cha msingi ni jamii kuisaidia polisi kuwabaini hao wauzaji ili waweze kukamatwa, maana tukisema tuwaachie hao polisi wenyewe itakuwa tunawapa lawama bure, kwani jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mtanzania
 
Back
Top Bottom