Polisi acheni kuingilia kazi za wanasiasa

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,744
5,446
Jeshi letu la polisi limejikuta likitumika kisiasa ili kuwapendeza watawala. Gazeti la Mtanzania ambapo Rain Magufuli amenukuliwa akisema waliohamia Chadema ni majizi! Sijashangazwa na kauli ya rais maana ni mwanasiasa na kauli zake zinafanana na wanasiasa wengine was Tanzania.

Najiuliza, iwapo Zitto, Lissu, Mbowe au mpinzani yeyote angetumia kauli kama hiyo dhidi ya mwanasiasa mwenzake ambaye ni rais, polisi wangemwacha salama?

Natoa wito kwa polisi wawaache wanasiasa wafanye kazi zao badala ya kuwaingilia wanaporushiana mipasho yao ya kisiasa vinginevyo wataabika na kudharauliwa na umma.

[A
20171101_123108.jpg
TTACH=full]621978[/ATTACH]
 
Hii kauli ya Rais Magufuri ni kauli uliyojaa hasira, ghadhabu, uchungu , chuki ,fitina na inaoneka wazi ndani ya hii kauli ni kutaka mtu ashikishwe hata kesi isiyo yake akae hata jela, Magufuri komaa kisiasa uache siasa za chuki.
 
Kwahyo unataka rais akamatwe! embu nenda kasome sheria inasemaje kuhusu viongozi ambao hawatakiwi kushitakiwa.
 
Jeshi letu la polisi limejikuta likitumika kisiasa ili kuwapendeza watawala. Gazeti la Mtanzania ambapo Rain Magufuli amenukuliwa akisema waliohamia Chadema ni majizi! Sijashangazwa na kauli ya rais maana ni mwanasiasa na kauli zake zinafanana na wanasiasa wengine was Tanzania.

Najiuliza, iwapo Zitto, Lissu, Mbowe au mpinzani yeyote angetumia kauli kama hiyo dhidi ya mwanasiasa mwenzake ambaye ni rais, polisi wangemwacha salama?

Natoa wito kwa polisi wawaache wanasiasa wafanye kazi zao badala ya kuwaingilia wanaporushiana mipasho yao ya kisiasa vinginevyo wataabika na kudharauliwa na umma.

[AView attachment 621978TTACH=full]621978[/ATTACH]
Huu uhai kidogo ilionao hii ccm ni msaada kutoka polisi tu , bila polisi ccm haimalizi wiki !
 
Kwahyo unataka rais akamatwe! embu nenda kasome sheria inasemaje kuhusu viongozi ambao hawatakiwi kushitakiwa.
Hujanielewa. Nawataka polisi waache wanasiasa wacheze ngoma yao wenyewe, hao majizi wakirudisha majibu polisi watulie waendelee kulumbana na kupashana.

Vv
 
msameheni ana hasira....
amegundua nguvu kubwa anayotumia kuwaaminisha Wananchi kuwa anakubalika , imekuwa bure.....
kaanzisha mahakama ya mafisadi...kajikuta anaotakiwa kuwapeleka huko ni maswahiba zake.
ile mahakama kama mahame
 
Huyu mzee ni wa hovyo sana aisee. Sijui kichwa chake kina nini. Yaani anaropoka hadi unajiuliza huyu mtu yuko sawa kweli kichwani. Anashindwa hata kujua yeye ni nani, hatambui nafasi yake kabisa. Inabidi wasaidizi wake wamsaidie ajitofautishe na Lusinde kibajaj.
 
Back
Top Bottom