Polisi 4 wafukuzwa kwa rushwa ya kumbambikiza ugoni mchina

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
Polisi 4 wafukuzwa kazi kwa rushwa
POLISI mkoani Kigoma imewafukuza kazi askari wake wanne kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na kujipatia fedha isivyo halali kutoka kwa raia wa China. Kamanda wa Polisi wa Mkoa Kigoma, Fraiser Kashai, ametaja askari waliofukuzwa kuwa ni makonstebo Admirabis, Waziri, Makasi na Elias.

Akieleza jana sababu za kufukuza kazi askari hao, Kamanda Kashai alisema mwanzoni mwa wiki hii katika kijiji cha Uvinza, walimvamia raia huyo wa China, Mafutao War, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni inayojenga barabara ya Kidahwe-Uvinza na kuchukua fedha.

Alisema awali askari hao walivamia nyumba ya kulala wageni ya Manchester ambako War alikuwa amepanga akiwa na mwanamke aitwaye Mary Kapele na kumkamata Mchina huyo na kumpeleka Polisi Uvinza kwa madai kuwa wamemshika ugoni.

Alibainisha kuwa baada ya kumfikisha Polisi askari hao walimtaka awape fedha na akawapa dola 300 za Marekani na Sh 10,000 ili kumaliza kesi hiyo. Hata hivyo, wakati sakata hilo likiendelea, raia wema walitoa taarifa Polisi mkoani ndipo uchunguzi ulipofanyika na askari hao wakabainika kutenda kosa hilo.

Kwa uchunguzi huo, Polisi iliwashitaki katika Mahakama ya kijeshi na kufikia uamuzi wa kuwafukuza baada ya kuthibitika kutenda kosa na kulifedhehesha Jeshi hilo kwa vitendo.
 
Ndiyo wakome wamezdi kubambikiana kesi.

Hivi ww kidume unasurport nn hapo mungekuwa mmewafukuza Ma waziri wenu hapo sawa dollar 300 na elfkumi ni pesa ya kuanza mfukuza mtu? Ukome mwenyewe na deni la serikari unalo daiwa.
 
Yaani kwa sababu ni mchina wananchi mara ngapi wamelalamikia jeshi la polisi na hawa chukui hatua jeshi gani linalo acha mapapa wakitanua na kuangamiza nchi
 
wangewafunga kimya kimya tuu bila kutangaza hi sio issue wananchi tunayotaka kusikia,kuna migube gube huku street ndio tunataka ikapumzike ndani.
 
Yaani kwa sababu ni mchina wananchi mara ngapi wamelalamikia jeshi la polisi na hawa chukui hatua jeshi gani linalo acha mapapa wakitanua na kuangamiza nchi

Mwanamke aliyekutwa naye kwenye guest house hakumtetea mchina kwa hao polisi hadi wamchukue kituoni na kumdai rushwa? Kibaya zaidi siku hizi rushwa iko wazi hadi kituo cha polisi maana tumezoea rushwa kabla ya kufika kituoni.
 
Fikiri kidogo great thinker,Hapo mwanamke alishapata chake toka kwa mchina polisi aende akafanye nini? Eti amtetee mmh maelezo hayaelezi uhusiano wao zaidi kukutwa gesti, sasa kashamaliza kazi kasepa!
 
Au huyo mwanamke alitumwa vinginevyo yasingefika huyo mchina.
 
Sheria ya nchi hii inatamka wazi kwamba " mtoa na mpokea rushwa wote wametenda kosa. Mbona habari hii haelezei lolote juu ya mtoa rushwa?au na makandarasi wa kichina nao wanakinga kama Rais?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom