Polisi 10 nusura wapigwe bomu.*Jambazi lilitaka kuwarushia likajilipua lenyewe

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,738
155,421
*Jambazi lilitaka kuwarushia likajilipua lenyewe


MAJAMBAZI watatu wameuawa kwa kupigwa risasi katika wilaya ya Ngara na Muleba baada
ya kupambana na polisi kwa dakika kadhaa huku mmoja akijilipuliwa na bomu mwenyewe
na kumfumua kichwa alililotaka kuwarushia polisi.
Kamanda wa polisi Mkoani Kagera, Henry Salewi alisem katika tukio la kwanza
ililitokea Januari 6, mwaka huu saa 3.30 usiku katika kijiji cha Kasande kata ya
Umuruvyangira mpakani mwa Tanzania na Burundi Wilayani Ngara.

Majambazi waliokuwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono, walikuwa kwaipamban ana polisi
hao huku wao wakirusha mabomu na polisi waliwamiminia risasi.

Alisema majambazi hayo yalitaka kumvamia mfanyabiashara mmoja wa kijijini hapo
ambaye hakuwa tayari kumtaja jina lake.

Kamanda Salewio alisema raia wema wa kijijini hapo walifanikiwa kutoa taarifa kwa
polisi wilayani humo siku hiyo saa 11 jioni ambapo jeshi hilo nalo liliweka mtego
wake.

Kutokana na hali hiyo, baada ya polisi kupata taarifa hizo askari wapatao 10
wakiongozwa na Mkuu wao wa upelelezi wa makosa ya jinai waliondoka kuelekea kijijini
hapo ambapo ilipofika saa 3.30 usiku walijitokea watu watatu katika eneo hilo
ambapo polisi waliwataka wajisalimishe lakini walionekana kukaidi na hivyo mmoja wa
watu hao akarusha bomu la kutupwa kwa mkono.

Hata hivyo polisi hao walijibu bomu hilo kwa kumimina risasi mfululizo ambapo
ilimweza kumpata mmoja wa majambazi hao na kumuua papo hapo.

Kutokana na mwenzao kuuawa jambazai mwingine alitaka kurusha bomu jingine kabla ya
kutenda ghafla lilimlipukia yeye na kumpasua kichwa na kufa papo huku mwingine
aliyebaki akifanikiwa kutoroka akiwa amepigwa risasi sehemu mbali mbali za mwili
wake na haijulikani alikimbilia sehemu gani.

Katika tukio la pili lilitokea katika kata ya Kamachumu Wilayani Muleba Januari 6
mwaka huu saa 4 usiku jambazi mmoja aliuawa katika majibizano makali ya risasi kati
ya polisi na majambazi hayo.

Kamanda Salewi alisema majambazi hayo walitaka kumvamia mfanyabiashara mmoja wa
nyama choma ambapo hata hivyo taarifa za uvamizi huo uliweza kupatikana na polisi
kupata habari hizo na hivyo kuweka mtego wao.

Alisema majambazi wapatao wanne walijitokeza katika eneo hilo, ambapo polisi
walipowamuru
kuweka silaha chini walikataa kutekeleza na matokeo yake kuanza kurusha risasi mbili
hewani kutishia polisi hao.

Kutokana na hali hiyo iliamusha hari za polisi hao na kuanza kujibizana nao kwa
risasi kwa dakika kadhaa na walifanikiwa kumuua jambazi moja na majamabzi wengine
walikimbia kusiko julikana na huyo aliyeuawa alipopekuliwa alikutwa na risasi tatu
za short gun na bunduki aina ya gobole.

SORCE: MAJIRA
 
Back
Top Bottom