Police Na NEC wanaweza chemsha usalama ktk hizi kampeni na baadaye wakakuta watu walichagua shari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Police Na NEC wanaweza chemsha usalama ktk hizi kampeni na baadaye wakakuta watu walichagua shari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Mar 12, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Leo CDM wakiwa Tengeru ktk Viwanja kando ya barabara, CCM walikuwa Usa River na bahati mbaya nao walikuwa na watu wengi toka nje ya Arumeru.Baada ya mkutano ilibidi magari mengi yaanze rudisha watu makwao nje ya mji na hawana njia mbala ya haraka zaidi ya kupita tengeru kuelekea mjini kabla ya kuchukua route zao. Muda huo wafuasi na wengine waliohudhuria mkutano wa CDM ndio walikuwa wakiruka barabara kwa wingi, CCM walikuwa wakipita na magari ,wabunge na matajiri walipita na magari mapya na mazuri ila hawa waliotoka njia za Vumbi wapo ktk magari chakavu na wanaonekana kuchoka huku wakishangaa mazingira. Kulikuwepo na akina mama mashaningi na wengine wa design hiyo walianza wanyooshea chadema vidole kwa style ya kuwaambia mnatobolewa...chadema nao wakaanza piga mayowe kuwazomea kwa style ya mayowe ya kifo/msiba kwa watu wa kaskazini wanayajua""Uwii uwii xn"". Nyumba ya gari alilokuwa maepnda Juma nkamia kuna land cruiser likuwa inakuja kasi na alikuwa apiga S barabarani kwa nia ya kugonga wana chadema.Nilikuwa nasubiri basi nami nilikoswakoswa na hilo gari nilipata hasira kwani sikuwa na camera yangu niwarushie hewani . Kuongea na watu wa karibu wa CCM hawakauwa waelewa , nilipowaambia kuwa kwa nini Polisi hawakuwepo kusaidia logistic nzima, hata km wana CCM wa nje ya mji walikuwa wanawahi ndoa zao mwisho wa lami+barabara za Vumbi.CDM wameonyesha ukomavu kwani uendeshaji huo ulionekana mbove tangu mbali na wangeweza anzisha mawe na kila kitu.Next time nadhani usalama uwe imara.Mbaya zaidi hata mjini walikuwa CCM wanazomewa kila wakipita.Nilipokuwa narusi mjini ktk mabaa na vituo vy mabasi kulikuwa na mayowe ya wezi, mafisadi, vibaraka, wafu, mashoga(NIkambiwa kijana katoga sikio na amekaa kwa cameron), n.k. Polisi wakiwa hawaonekani wala kuwasiliana ili kuepusha route za viongozi wa vyma na wafuasi wasikutane,basi mwisho wa kampeni watakuta watu walishajifunza shari za kujilinda na kuongeza ushawishi.
   
Loading...