Police Himo mkoani Kilimanjaro waitenga Rombo kuwa ni sehemu ya Kenya

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,481
1,364
Mu khali gani wana jamvi?

Huku kwetu rombo hali si shwari kwani sukari imezidi kupaa bei toka 2400 hadi 3000, hali hii inatokana na police wa himo kuzuia magari yote yanayotoka moshi yaliyobeba sukari na mahindi na kudai kuwa yanapeleka kenya na pindi gari likikutwa na hata mfuko mmoja wa sukari wanalipeleka kituoni na kudai ilikutwa mpakani.

Kwa sisi huku Rombo sukari tunaitegemea toka Moshi, kinachonishangaza tangia lini mpaka wa TZ na Kenya kuhamia himo? Au sisi sio sehem ya TZ? Mbunge wetu bwana SELASINI uko wapi? Wananchi wako tunateseka.

Source madereva wa malori wanaotoka Moshi

Nawasilisha
 
Polisi "nji" hii wa ajabu sana, wanafanya kazi kwa kukurupuka normally, haiyumkini baada ya kuumbuliwa deal lao la magendo lililomwondoa hata mkuu wa upelelezi mkoa ndo imepelekea hali hiyo sasa! ni kama wanataka kuwakomoa wananchi waliotoa taarifa ngazi za juu based on dhana ya polisi jamii
 
poleni sana mbe. ni ujinga wa polisi wetu wengi ni wale wa darasa la 7
sidhani kama kuna sheria inayosema anaepeleka sukari rombo anapeleka kenya
kwani huko hakuna wafanyabiashara wanaochukua TPC kwa vibali?
yawezekana wachaga hapo rombo mashati useri na tarakea wanachukua advantage hiyo kuwakamua.
 
Inawezekana polisi wametumwa kuwaadhibu wananchi wa Rombo (kwa kuchagua CDM). Na kama mpaka wa sukari kati ya Kenya na Tanzania sasa upo Himo, basi mpaka wa mali nyingine kama mafuta uhamie Himo vile vile.

Mpaka ukiwa Himo halafu polisi wa Bongo akaonekana Rombo hatakuwa na kosa la kuvamia nchi ya jirani?

Madereva wa malori yenye sukari wakubali kukamatwa ila wadai kufikishwa mahakamani mara moja. Polisi watathibitishaje sukari ilikuwa inapelekwa Kenya?
 
Back
Top Bottom