Police Central Dar ukwepaji kodi huu mnaujua?

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
WANA JF, kuna kampuni moja inaitwa Whymbi Freight Ltd, inashughulika na Clearing and Fowarding bandarini. Desemba 24, mwaka 2018, walitoa bus dogo aina ya Toyota Coaster (Chassis NO. BB40-0004233) la mteja aitwaye Sleiyum Hemed Ally, ambaye taarifa za awali zilisema ni raia wa Zambia mji wa Ndola.
Document zote zilikuwa safi kuhusu kodi za Mamlaka ya Mapato (TRA). Bus hilo lilitakiwa kusafirishwa na Kampuni ya Whymbi yenyewe kwenda Ndola Zambia kwa Sleiyum ambaye ni mmiliki na dereva wao alikuwa tayari kwa safari. Lakini wakapokea taarifa kutoka kwa Sleiyum kwamba, anamtuma dereva wake aitwaye Seleman ambaye atalipeleka bus hilo Ndola.
Desemba 26, siku mbili mbele, Seleman alifika eneo husika na kukabidhiwa Coaster hilo sanjari na document zote za gari zinazoonesha kuwa, limeingia nchini kihalali na limepitishwa na TRA.
Lakini baada ya siku kadhaa, system ya kampuni likaliona gari hilo bado lipo Dar, yaani halijeanda Ndola. Maana lingeondoka, lilitakiwa kupita Check Point Misugusugu, Kibaha-Pwani, Check Point Makambako- Njombe na Exit Point Tunduma-Songwe kisha kuingia Zambia.
Kwa vile wana namba ya simu ya dereva Seleman aliyeagizwa kulichukua, wakampigia simu kumuuliza, akasema kuna mtu anamsubiri ana pesa yake, kama shilingi laki mbili, akimlipa atazitumia kuweka mafuta ya kumfikisha Ndola, Zambia.
Kwa sababu kampuni ilikuwa inategemea gari lifike ili ilipwe pesa zake, uongozi ulijitolea kumpa Seleman kiasi hicho cha pesa ili asipoteze muda Dar, apeleke gari kwa mteja wao, Zambia.
Baada ya hapo, kampuni ikawa inalitazama gari hilo kwenye system kama litavuka mpaka kuingia Zambia, lakini halikuonekana. Ndipo uongozi ukaingiwa na wasiwasi na kuanza kufuatilia kwa undani ambapo iligundulika kuwa:
1. Mmiliki wa Coaster hilo siyo Sleiyum Hemed Ally, bali ni Mtanzania aitwaye Omari, mkazi wa jijini Dar, ‘alicheza’ na makaratasi.
2. Sleiyum Hemed Ally ni mtu hewa, hayupo Ndola Zambia.
3. Omari ndiye aliyejifanya Sleiyum Hemed wa Ndola, Zambia na kuagizia gari hilo kupitia kampuni hiyo.
4. Coaster hilo lilipelekwa sehemu (pengine gereji) maeneo ya Tabata, Dar na kubadilishwa mfumo wa viti ndani, lengo lifanye kazi ya kubeba abiria (labda daladala).
5. Pia, kuna Mkongo mmoja, aliuziwa Coaster hilohilo kwa dola za Kiamerika 10,000 (kiasi cha milioni 25 za Kibongo), akatoa lakini hakupewa gari na akaripoti Police Central.

Kampuni iliamua kumtafuta dereva huyo ambaye alikuwa hana majibu yaliyonyooka, ikabidi kampuni ikimbilie Kituo cha Police Central na kutoa maelezo ambapo lilifunguliwa jalada NO: DSM/ILALA/CID/PE/15/2019.
Seleman alikamatwa na mke wa Omari, wakakaa Central kwa siku kadhaa. Baadaye akakamatwa na Omari ‘Sleiyum’ naye akakaa kituoni hapo kwa siku kadhaa, wakaachiwa kwa dhamana (pengine kwa mujibu wa makosa yao).
Habari za uhakika ni kwamba, Omari ambaye kampuni inamwona ni mtuhumiwa namba moja, baada ya kuachiwa alikwenda nchini Afrika Kusini kwani alipokamatwa ‘aligundulika’ na makosa mengine, ikiwemo kukutwa nyumbani kwake magari kadhaa yakiwa na namba zinazofanana.
Baada ya kuona hakuna kinachoendelea, uongozi wa kampuni hiyo uliamua kuandika barua kwa MKURUGENZI WA UPELELEZI MAKAO MAKUU YA POLISI, DAR ES SALAAM ikisomeka hivi;
Sisi Kampuni ya Whymbi Freight Ltd, tunaomba msaada wa kiofisi na kisheria juu ya mwenendo mzima wa kesi NO. DSM/ILALA/CID/PE/15/2019 iliyofunguliwa Central Police Station inayohusu wizi wa gari tajwa hapo juu uliofanywa na ndugu Seleman na ndugu Omari ambao namba zao za simu ni… (zimeandikwa).
Barua ikaendelea: Gari hiyo ilitolewa bandarini tarehe 24/12/2018 na tulimkabidhi ndugu Seleman mnamo tarehe 26/12/2018 kwa ajili ya kuipeleka Ndola Zambia kwa mmiliki wa gari hilo ajulikanaye kwa jina la bwana Seleiyum Hemedi Ally kitu ambacho hakikufanyika.
Barua ikasema: Madhara ya gari hilo kutokufika sehemu husika litapelekea kampuni kupewa adhabu ya kulipa faini ya BOND SECURITY, pili kufungiwa kampuni lakini pia hata serikali kupoteza mapato yake. Hivyo basi tunaomba msaada wa dhati kwa sababu kampuni hairidhishwi na mwenendo mzima wa tatizo linavyoshughulikiwa.
Barua hii iliandikwa Machi 18, mwaka jana ambapo uongozi uliambiwa urudi Central kushughulikiwa, mtuhumiwa mmoja akiwa Sauzi mwingine akiendelea na maisha yake jijini Dar mpaka mwezi huu, Oktoba, 2019.
Lakini pia, Machi 29, mwaka jana, kampuni hiyo iliandika barua kwa MKURUGENZI WA INTELEJENSIA YA JINAI, MAKAO MAKUU YA POLISI, DAR kwa malalamiko hayohayo na kutakiwa kurudi Central.
Pamoja na hali kuwa hivyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitengo cha magari (TMU), iliendelea kudai mapato kutokana na zoezi la kulitunza na kulitoa gari hilo bandarini ambapo kampuni, awali ilitakiwa kulipa shilingi 21,405,520 lakini kwa kupitisha muda (wakati kampuni inadili na kesi na Omari na Selemani), Oktoba 2, mwaka jana wamepigwa penati na sasa wanatakiwa kulipa shilingi 33,238,889 kwa bill No. TZDL19P01988320.
Kampuni pia iliandika barua kwa IGP, Simon Sirro kwa vile inamjua hataki kusikia mwananchi akilalamikia kunyimwa haki na kwamba, Sirro ni kamanda mchapa kazi asiyetaka kunusa harufu ya rushwa popote pale, lakini haijajulikana kama barua hiyo ilimfikia mezani kwake au la!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaonekana polisi wamewekwa mfukoni hapo. Kwa hatua mlizochukuwa sijui ni kwa nini hao wakubwa hawajachukuwa hatua. Bila shaka hii thread itasomwa hata na rais mwenyewe na hatua zitachukuliwa. Msichoke kusambaza haya malalamiko kila sehemu.
 
Nadhani kiutaratibu, mlipaswa kumsindikiza huyo Selemani hadi afike mpakani na kuhakikisha gari limemfikia muagizaji wa Ndola, vinginevyo kila mtu atafanya kama mlivyofanya nyinyi halafu muombe msilipe kodi? Ni wajibu wenu kuhakikisha gari linatoka nje ya mipaka ya Tz, vinginevyo mlilipie kodi hilo gari.
 
Inaonekana hii kampuni yao wanamhudumia huyu mzambia mubongo kwa muda mrefu mpaka sasa na waliufahamu huu ukwepaji tangia muda sana kwa nini hawakuriibua hili mapemaa!! rejea andiko la mleta maada akisema “ huyo sleyhiman ana magari mengi ambayo kayamiliki kwa njia hiyo hiyo kama hili ambalo kaja kuwa badilikia na kutowalipa wakaamua kumlipua” nahisi hii kampuni ya clearing and forwarding itambue lasimi kuwa nayo kuna mahari ilijikwaa hasa kwa kufumbia macho hilo swala bila kulilipoti kwa mamlaka husika, hii maana ake tunaweza kusema nayo hii kampuni ilishiriki kubariki ukwepeshaji kodi kwa hayo magari ya awali yanayosemwa na mleta maada.
 
Acha kuhisi kwenye vitu nyeti kama hivi.
Inaonekana hii kampuni yao wanamhudumia huyu mzambia mubongo kwa muda mrefu mpaka sasa na waliufahamu huu ukwepaji tangia muda sana kwa nini hawakuriibua hili mapemaa!! rejea andiko la mleta maada akisema “ huyo sleyhiman ana magari mengi ambayo kayamiliki kwa njia hiyo hiyo kama hili ambalo kaja kuwa badilikia na kutowalipa wakaamua kumlipua” nahisi hii kampuni ya clearing and forwarding itambue lasimi kuwa nayo kuna mahari ilijikwaa hasa kwa kufumbia macho hilo swala bila kulilipoti kwa mamlaka husika, hii maana ake tunaweza kusema nayo hii kampuni ilishiriki kubariki ukwepeshaji kodi kwa hayo magari ya awali yanayosemwa na mleta maada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WANA JF, kuna kampuni moja inaitwa Whymbi Freight Ltd, inashughulika na Clearing and Fowarding bandarini. Desemba 24, mwaka 2018, walitoa bus dogo aina ya Toyota Coaster (Chassis NO. BB40-0004233) la mteja aitwaye Sleiyum Hemed Ally, ambaye taarifa za awali zilisema ni raia wa Zambia mji wa Ndola.
Document zote zilikuwa safi kuhusu kodi za Mamlaka ya Mapato (TRA). Bus hilo lilitakiwa kusafirishwa na Kampuni ya Whymbi yenyewe kwenda Ndola Zambia kwa Sleiyum ambaye ni mmiliki na dereva wao alikuwa tayari kwa safari. Lakini wakapokea taarifa kutoka kwa Sleiyum kwamba, anamtuma dereva wake aitwaye Seleman ambaye atalipeleka bus hilo Ndola.
Desemba 26, siku mbili mbele, Seleman alifika eneo husika na kukabidhiwa Coaster hilo sanjari na document zote za gari zinazoonesha kuwa, limeingia nchini kihalali na limepitishwa na TRA.
Lakini baada ya siku kadhaa, system ya kampuni likaliona gari hilo bado lipo Dar, yaani halijeanda Ndola. Maana lingeondoka, lilitakiwa kupita Check Point Misugusugu, Kibaha-Pwani, Check Point Makambako- Njombe na Exit Point Tunduma-Songwe kisha kuingia Zambia.
Kwa vile wana namba ya simu ya dereva Seleman aliyeagizwa kulichukua, wakampigia simu kumuuliza, akasema kuna mtu anamsubiri ana pesa yake, kama shilingi laki mbili, akimlipa atazitumia kuweka mafuta ya kumfikisha Ndola, Zambia.
Kwa sababu kampuni ilikuwa inategemea gari lifike ili ilipwe pesa zake, uongozi ulijitolea kumpa Seleman kiasi hicho cha pesa ili asipoteze muda Dar, apeleke gari kwa mteja wao, Zambia.
Baada ya hapo, kampuni ikawa inalitazama gari hilo kwenye system kama litavuka mpaka kuingia Zambia, lakini halikuonekana. Ndipo uongozi ukaingiwa na wasiwasi na kuanza kufuatilia kwa undani ambapo iligundulika kuwa:
1. Mmiliki wa Coaster hilo siyo Sleiyum Hemed Ally, bali ni Mtanzania aitwaye Omari, mkazi wa jijini Dar, ‘alicheza’ na makaratasi.
2. Sleiyum Hemed Ally ni mtu hewa, hayupo Ndola Zambia.
3. Omari ndiye aliyejifanya Sleiyum Hemed wa Ndola, Zambia na kuagizia gari hilo kupitia kampuni hiyo.
4. Coaster hilo lilipelekwa sehemu (pengine gereji) maeneo ya Tabata, Dar na kubadilishwa mfumo wa viti ndani, lengo lifanye kazi ya kubeba abiria (labda daladala).
5. Pia, kuna Mkongo mmoja, aliuziwa Coaster hilohilo kwa dola za Kiamerika 10,000 (kiasi cha milioni 25 za Kibongo), akatoa lakini hakupewa gari na akaripoti Police Central.

Kampuni iliamua kumtafuta dereva huyo ambaye alikuwa hana majibu yaliyonyooka, ikabidi kampuni ikimbilie Kituo cha Police Central na kutoa maelezo ambapo lilifunguliwa jalada NO: DSM/ILALA/CID/PE/15/2019.
Seleman alikamatwa na mke wa Omari, wakakaa Central kwa siku kadhaa. Baadaye akakamatwa na Omari ‘Sleiyum’ naye akakaa kituoni hapo kwa siku kadhaa, wakaachiwa kwa dhamana (pengine kwa mujibu wa makosa yao).
Habari za uhakika ni kwamba, Omari ambaye kampuni inamwona ni mtuhumiwa namba moja, baada ya kuachiwa alikwenda nchini Afrika Kusini kwani alipokamatwa ‘aligundulika’ na makosa mengine, ikiwemo kukutwa nyumbani kwake magari kadhaa yakiwa na namba zinazofanana.
Baada ya kuona hakuna kinachoendelea, uongozi wa kampuni hiyo uliamua kuandika barua kwa MKURUGENZI WA UPELELEZI MAKAO MAKUU YA POLISI, DAR ES SALAAM ikisomeka hivi;
Sisi Kampuni ya Whymbi Freight Ltd, tunaomba msaada wa kiofisi na kisheria juu ya mwenendo mzima wa kesi NO. DSM/ILALA/CID/PE/15/2019 iliyofunguliwa Central Police Station inayohusu wizi wa gari tajwa hapo juu uliofanywa na ndugu Seleman na ndugu Omari ambao namba zao za simu ni… (zimeandikwa).
Barua ikaendelea: Gari hiyo ilitolewa bandarini tarehe 24/12/2018 na tulimkabidhi ndugu Seleman mnamo tarehe 26/12/2018 kwa ajili ya kuipeleka Ndola Zambia kwa mmiliki wa gari hilo ajulikanaye kwa jina la bwana Seleiyum Hemedi Ally kitu ambacho hakikufanyika.
Barua ikasema: Madhara ya gari hilo kutokufika sehemu husika litapelekea kampuni kupewa adhabu ya kulipa faini ya BOND SECURITY, pili kufungiwa kampuni lakini pia hata serikali kupoteza mapato yake. Hivyo basi tunaomba msaada wa dhati kwa sababu kampuni hairidhishwi na mwenendo mzima wa tatizo linavyoshughulikiwa.
Barua hii iliandikwa Machi 18, mwaka jana ambapo uongozi uliambiwa urudi Central kushughulikiwa, mtuhumiwa mmoja akiwa Sauzi mwingine akiendelea na maisha yake jijini Dar mpaka mwezi huu, Oktoba, 2019.
Lakini pia, Machi 29, mwaka jana, kampuni hiyo iliandika barua kwa MKURUGENZI WA INTELEJENSIA YA JINAI, MAKAO MAKUU YA POLISI, DAR kwa malalamiko hayohayo na kutakiwa kurudi Central.
Pamoja na hali kuwa hivyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitengo cha magari (TMU), iliendelea kudai mapato kutokana na zoezi la kulitunza na kulitoa gari hilo bandarini ambapo kampuni, awali ilitakiwa kulipa shilingi 21,405,520 lakini kwa kupitisha muda (wakati kampuni inadili na kesi na Omari na Selemani), Oktoba 2, mwaka jana wamepigwa penati na sasa wanatakiwa kulipa shilingi 33,238,889 kwa bill No. TZDL19P01988320.
Kampuni pia iliandika barua kwa IGP, Simon Sirro kwa vile inamjua hataki kusikia mwananchi akilalamikia kunyimwa haki na kwamba, Sirro ni kamanda mchapa kazi asiyetaka kunusa harufu ya rushwa popote pale, lakini haijajulikana kama barua hiyo ilimfikia mezani kwake au la!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mji una mambo mengi
 
Mkuu soma uzi sawasawa. Polisi walikuja kugundua jamaa ana magari mengi yanayofanana namba. Siyo kampuni inajua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona picha limeishia kati???Hii inabidi mumsubiri namba moja akifanya ziara mlie na mic

Back
Top Bottom