Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Kuna udhaifu wa kimsingi katika haki na mahakama Tanzania. Sioni polisi wakishitakiwa kwa makosa ya (1)Assault na (2)wrongful arrest ambayo wanayatenda mara kwa mara.

Huyo binti kwenye picha amekuwa assaulted na polisi. A crime has been committed. Kinaisha hivi hivi?

Watetezi wa Watanzania wakati huu, has CDM, waweke kumbukumbu ya picha kama hizi. Siku tukitokana na huu utawala wa kinyanyasaji basi tutazitumia hizi picha kuwashtaki wahusika.

Hii picha iwekwe vile vile kwenye website nyingine za Watanzania na hata za majirani zetu. MABALOZI Dar wanaona picha kama hizi?

Kuna uwezekano wa kupata nakala ya picha hii ambayo inaonyesha wazi wazi sura za mapolisi husika? Ni vema wajulikane vizuri na wajionee kazi waliyofanya.
 
Image15.jpg

[SIZE=+0]Above. Members of the Field Force Unit beating up Muslims at Manzese area on 13 February, 1998.[/SIZE]
[SIZE=+0]Below. Police officers opening fire on unarmed Muslims at Mwembechai on 13 February, 1998.[/SIZE]
 
Mzee Mwanakijiji said:
Labda tatizo niliwaambia wanaweza kuhojiwa na CNN kwa ajili ya habari n.k wakaamua kusepa!
Hapo...!

Watakuwa walihofia usalama wa maisha yao, ndo bongo hiyo.
 
Sasa CNN ndiyo watatusaidia? Mbona watu wa Occupy Wall Street wametoswa? Mnataka Dunia ijue? kwani unafikiri hawajui? Wake up TZ.

Kama wangekuwa wanajua hawangeendelea kusifia AMANI Tanzania. Hawajui. Wangejuaje? Nani kawaambia?

Ingetoka video kwenye youtube, ya huyo binti kwenye picha hapo juu, akiparamiwa kinyama na mapolisi ingeonyeshwa BBC, CNN na hata FOX NEWS. Hapo ndio "wangejua", na wangemnyoshea JK kidole.

Tupaze sauti bila kuchoka labda mmoja wa wafalme atasikia sauti za nyikani.

Ninachojiuliza mbona hili linalohusu kabinti ka kati ya 22-23 kanakonusuru maisha yake hatujasikia likikemewa kama lile la Mama aliyevuliwa hijabu kule Igunga.
 
Mwezi wa October mwaka 1966, wanafunzi wa elimu ya juu wakiongozwa na wale wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walifanya maandamano ya kugomea sheria mpya ya JKT iliyopitishwa na Bunge. Pamoja na mabango waliyokuwa wameyatayarisha yaliyosema “afadhali wakati wa mkoloni” pia walikuwa na ujumbe maalum waliotaka kumfikishia Raisi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliouita “ultimatum”.

Mwalimu Nyerere kwa busara kubwa alihakikisha wanafunzi wote walioandamana hawabughudhiwi bali wanapewa "escort" hadi Ikulu ambako angewapokea. Na kweli walipofika Ikulu walikaribishwa na msemaji wao akaombwa asome ujumbe waliokuwa nao na Mwalimu alimsikiliza kwa makini hadi alipomaliza. Mwalimu hakukubaliana nao na hivyo aliamuru chuo kifungwe na warudi makwao wakakomae kwanza.

Huo ndio ulikuwa utawala na hakuna mwanafunzi hata moja aliyedhurika kwa kupigwa virungu au kurushiwa mabomu ya machozi. Siku hizi tunao viongozi ambao wako tayari kuwapiga mabomu hata watoto wa chekechea kama watathubutu kulalamikia magari yanayopita barabarani kwa kasi na hivyo kuhatarisha maisha yao. Ni kama vile kazi ya jeshi la polisi si tena kutulinda sisi na mali zetu bali kutupiga mabomu na kupora mali zetu.

Kusema kweli hakuna picha iliyonihuzunisha kama ya huyo binti hapo juu na nimebaki nikijiuliza hivi huyo Mkandala si mzazi ? hana familia ? hana watoto ? Je alijisikiaje alipoitazama hiyo picha ? Alikunywa hiyo glasi yake ya whisky na kujipongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya huyo binti kudhalilishwa na hao wahuni ? Mkandala, Mkandala, Mkandala najua ulienda shule lakini mbona hata hujaelimika ? Shame on you !

kuna 'documentary' ya mwaka 1966 niliangalia kuhusu huo mgomo wa kugomea JKT wanafunzi hao walipewa adhabu ya kuchapwa viboko kama wanavyochapwa wa shule ya msingi,, ila now we don't have legitimate police force to protect civilians and their properties instead we've soul taking police force
 
kuna 'documentary' ya mwaka 1966 niliangalia kuhusu huo mgomo wa kugomea jkt wanafunzi hao walipewa adhabu ya kuchapwa viboko kama wanavyochapwa wa shule ya msingi,, ila now we don't have legitimate police force to protect civilians and their properties instead we've soul taking police force

sure, that all we have.
 
111511reutersowsraw_512x288.jpg

Ubabe upo hata ktk Dunia ya Kwanza.
Hapo huwezi kulinganisha na huku kwetu... Kwanza siuoni moshi wa mabomu ya machozi hapo. Polisi wetu wamechanganyikiwa kiasi kwamba hata watoto wa chekechea wakiandamana watapigwa mabomu ya machozi. Mbeya walipiga hadi dispensary. Haina maana kutumia nguvu ya ziada wakati unayepambana naye hana nguvu kama yako. Polisi wetu hawana sera ya kuzuia maandamano, sera yao ni kutawanya maandamano, tena kwa mabomu. Polisi wetu inaonekana hawana mafunzo ya kutosha ya kupambana na waandamanaji. Kikubwa zaidi polisi wetu ni wezi, wanatumia mwanya wa kukamata watu wengi ili ukifika polisi wanasema kuingia bure na kutoka ni hela, kila anayekamatwa kupatia dhamana ukiwa polisi ni hadi utoe hela. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu, Said Mwema anaigaragaza reputation yake. Ameshindwa kuzuia uhalifu, kutenda haki na muhimu zaidi kuzuia rushwa. Wakati mwingine naamini kuwa polisi wanaisaidia sana CCM kwa vile imeoza na iko blind kiasi kwamba haioni uozo wa hali ya juu ndani ya jeshi, kikija chama makini na mfumo makini utawaharibia ulaji.
 
Image15.jpg

[SIZE=+0]Above. Members of the Field Force Unit beating up Muslims at Manzese area on 13 February, 1998.[/SIZE]
[SIZE=+0]Below. Police officers opening fire on unarmed Muslims at Mwembechai on 13 February, 1998.[/SIZE]
Haki, umenikumbusha mbali, siku hiyo nilikuwepo eneo la tukio, na niliripotia chombo fulani cha habari, by then, young and brave, sikuogopa kusema nilichokiona na kilichofanyika. Now old with family atachments, sasa nikiona kitu, najikuta nafikiri kwanza kabla ya kusema, sometimes unajukuta unaishia kujinyamazia tuu. Where are the young and brave of this time, mbona wakati wetu tulikuwepo?.
 
One day it will be pay day!!!!

Ni wahuni tu wanaficha sura zao !

943234.jpg

9013142-essay.jpg

tz_pix.jpg

normal_moro9.jpg

Things cannot continue this way - these are not police but trained thugs ! Polisi wetu hawatulizi ghasia, kazi yao ni kuchochea ghasia waweze kuwapiga na kuwaumiza wananchi. Maandamano ya Watanzania siku zote yanakuwa ya amani hadi wanapofika hawa wavuta bangi, vijana wa Afande Mwema.
 
The world needs to see what is taking place in peaceful warless Tanzania. Police are there to serve and protect the public. If anyone has a phonecam, use it. Record what is taking place in front of your eyes. Get a twitter account & upload images and tag them.
I think JF is a limited medium. A website dedicated to Tanzania police brutality and other violations of human rights in this country would be a better tool for reaching a wide audience. Even organisations like the UN, AU, etc. could easily be directed to the site. Any tech savvy kids to volunteer for the job? We can contribute towards some of the costs. We would also need someone to coordinate the job.
 
Tunaangamia kwa kukosa maarifa
Siyo kukosa maarifa. Ni kukosa ujasiri. Ni wepesi wa kulalamika, kulaumu na kubwabwaja. Unapofika wakati wa kutenda kila mtu anataka mwenzie ndiye aanze halafu yeye atoke nyuma tena kwa kujifichaficha.
 
Kama wangekuwa wanajua hawangeendelea kusifia AMANI Tanzania. Hawajui. Wangejuaje? Nani kawaambia?

Ingetoka video kwenye youtube, ya huyo binti kwenye picha hapo juu, akiparamiwa kinyama na mapolisi ingeonyeshwa BBC, CNN na hata FOX NEWS. Hapo ndio "wangejua", na wangemnyoshea JK kidole.

Kama unaongelea nchi za magharibi na vyombo vyao vya habari umekosea. Huwa hawagusi vikaragosi vyao au watawala wanaolinda maslahi yao. Ni pale wanapoenda kinyume na matakwa yao au wanapompata kibaraka mwingine mzuri zaidi ndipo ubaya unapoonekana kwao. Nchi zote za Arabuni ambazo zimefanya 'mapinduzi ya umma' zilikuwa zinasifiwa kwa kuwa marafiki wa magharibi. Mapinduzi hayakuanzishwa na nchi za magharibi bali walijiingiza baada ya watu wenyewe kuchoka na kuchukua hatua. Nal engo lao si kutetea wanyonge bali kulinda maslahi au kuanzisha maslahi mapya kama vile nchini Libya. Na JK na serikali yake ni vibaraka wakubwa.
 
Mwezi wa October mwaka 1966, wanafunzi wa elimu ya juu wakiongozwa na wale wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walifanya maandamano ya kugomea sheria mpya ya JKT iliyopitishwa na Bunge. Pamoja na mabango waliyokuwa wameyatayarisha yaliyosema “afadhali wakati wa mkoloni” pia walikuwa na ujumbe maalum waliotaka kumfikishia Raisi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliouita “ultimatum”.

Mwalimu Nyerere kwa busara kubwa alihakikisha wanafunzi wote walioandamana hawabughudhiwi bali wanapewa "escort" hadi Ikulu ambako angewapokea. Na kweli walipofika Ikulu walikaribishwa na msemaji wao akaombwa asome ujumbe waliokuwa nao na Mwalimu alimsikiliza kwa makini hadi alipomaliza. Mwalimu hakukubaliana nao na hivyo aliamuru chuo kifungwe na warudi makwao wakakomae kwanza.

Huo ndio ulikuwa utawala na hakuna mwanafunzi hata moja aliyedhurika kwa kupigwa virungu au kurushiwa mabomu ya machozi. Siku hizi tunao viongozi ambao wako tayari kuwapiga mabomu hata watoto wa chekechea kama watathubutu kulalamikia magari yanayopita barabarani kwa kasi na hivyo kuhatarisha maisha yao. Ni kama vile kazi ya jeshi la polisi si tena kutulinda sisi na mali zetu bali kutupiga mabomu na kupora mali zetu.

Kusema kweli hakuna picha iliyonihuzunisha kama ya huyo binti hapo juu na nimebaki nikijiuliza hivi huyo Mkandala si mzazi ? hana familia ? hana watoto ? Je alijisikiaje alipoitazama hiyo picha ? Alikunywa hiyo glasi yake ya whisky na kujipongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya huyo binti kudhalilishwa na hao wahuni ? Mkandala, Mkandala, Mkandala najua ulienda shule lakini mbona hata hujaelimika ? Shame on you !

It is true hawakupigwa virungu na polisi lkn walichapwa viboko na Nyerere mwenyewe, mmoja wao akiwa Samuel Sitta
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom