Kinachoendelea sasa kwa jeshi letu la polisi ni muendelezo tuu wa haya!.Wanabodi
Nimeangalia ITV news hiyo kamata kamata ya jana ya waunini wa kanisa la Ephata, vijana wako wameonyesha udhaifu mkubwa!.
Baada ya kuwalipua wale waumini kwa mabomu ya machozi na kuwa contain, walitumia risasi za moto za nini kukabiliana na watu wasio na silaha yoyote?.
Kitu cha kusikitisha zaidi ni watuhumiwa hao kuendelea kushushiwa kipigo hata baada ya kuwa mikononi mwa palisi!.
Baada ya vijana wako kuwakamata watuhumiwa kuna sababu gani ya kuendelea kuwashushia kipigo mpaka wakiwa ndani ya defender ya polisi?.
Naomba niwakumbushe tuu baadhi ya visa vya police brutality and no one amechukuliwa hatua zozote!.
Kuna kisa cha watuhumiwa fulani 4 kilichotokea Arusha ambapo watuhuniwa hao walikamatwa toka nyumbani mwao mmoja baada ya mwingine wakiwa wazima huku wakitembea wenyewe siku ya Ijumaa.
Jumamosi ndugu zao wakafika kituo cha polisi kuwaletea ndugu zao chakula, walielezwa watuhumiwa hao wamepelekwa mahali kwa mahojiano.
Kesho yake Jumapili waliporudi polisi walielezwa ndugu zao wamepelekwa hospitali ya Mt. Meru.
Walipofika hospitali waliinyeshwa miili ya watu wanne waliouwawa kinyama na majeraha ya vipigo!. Polisi walipoifikisha miili hiyo hospitalini hapo, waliandikisha kuwa wameiokota eneo la Unga Limited baada ya kupigwa na watu wenye hasira!.
The story ended up there and then!. Hakuna chochote kilicho fuatia hata tuu japo kuulizwa kama ile kesi ya Zombe!.
Kwa nini mtuhumiwa aliyekuwa mzima afie mikononi mwa polisi bila uwajibikaji wowote wa jeshi la polisi?!.
Kamanda Mwema, haya yanatokea kwa sababu mnajua Watanzania hawajui haki zao, polisi wako hawajui haki za binaadamu na kama arrest kama za jana zenye police brutality zimefanywa mbele ya camera, and no body cares, huko behind bars ni nini haswa kinafanyika?. Si ndio itakuwa worse?!.
Yote haya yanawezekana kwa sababu Watanzania hatujui haki zetu, chochote kinachofanywa na polisi wanajua ndio haki yao tena watu hawajui kabisa kuwa raia wa kawaida anaweza kulishitaki jeshi la polisi!.
No one is above the law, please stop this police brutality inayofanywa wazi wazi and behind clossed doors!.
Thanks.
Pasco.
HIYO NDIO DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI NCHINI
Action & Reaction unadhani mwisho wake ni nini?.Hakuna brutality yoyote....ni lazima tujifunze kutii mammlaka....force/nguvu iliyotumika ni reasonable....compared to resistance kutoka kwa raia....usiseme brutality ni kubwa ....sema pia kiwango cha wananchi kukaidi na kutokutii mammlaka kimeongezeka.....action and reaction
Hhaahhah Chuki .... Say That when your Mother get shotWakuu ni ombi tu hizi picha zinazidisha hasira kwa wale walio namna moja au nyengine athirika na fujo au matukio hayo. Sidhani kama ni busara kuziweka kwani unachochea chuki katika jamii!! Ni mtazamo tu.