Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Odinyo, sitetei walichofanya hao wavamizi, au sitetei uhalifu wa aina yoyote, ninachotetea, ni kuwa
1. Hao wahalifu hawakuwa na silaha yoyote ya moto, sasa polisi wanapiga risasi za moto za nini?.
Sipo sheria, taratibu na kanuni zinazotawala uvamizi wa polisi kwenye nyumba za ibada pale wahalifu
wanapokimbilioa kwenye nyumba hizo kujisalimisha!, zilifuatwa?. Sikuona gari la matangazo, sikuona polisi
wakilizunguka jengo kuwataka wajisalimishe, baada ya kutumia mabomu ya machozi kwa wahalifu wasio na silaha
za moto, kinachofuatia ni ruber bullets na sio fire bullets!. Nilichoona ni fire bullets as if jamaa wako vitani, na hao
askari wenyewe nimeona wanavyo advance, wako nyoro nyoro tuu, wakikutana na watu wa ukweli wa shughuli hizo
wangeweza wiped out!.

2. Wahalifu umeshawashika, wako chini ya ulinzi wa polisi, kwa nini ni polisi hao hao waliendelea kuwashushia vipigo?.
Nilidhana mikononi mwa polisi ndizo safe hands za wahalifu kujisalimisha!, kichapo cha nini?. I wish kama hilo kanisa ni kweli linamwabudui Mungu aliyejuu, hao askari wote waliofanya waliyoyafanya, yatawakuta ya kuwakuta!.

kipigo lazima wajifunze..'ndo maana kunanguvu ya kawaida..'na nguvu ya ziada,,?hii hapo ya ziada ndo pale palikuwa mahala pake
 
Tena kama mm ndo ningekuwa igp ningeruhusu nakoz za kutosha..'m raia ina mambo ya kibish ndo maana inasomeka TANZANIA POLICE FORCE ni sahihi kabisa kupewa nakozi m naona hata hicho kipondo hakikuwatosha

Ujinga kama huu unatokaga mdomoni kwa mtu ambaye hajawahi kuwa victim wa polisi. Ndugu yangu, niliwahi kupigwa makofi na polisi pale Kilwa Road bila kujua sababu, wakaniweka chini ya ulinzi na baadaye jioni nikaachiwa kwa kuombwa radhi ya mdomo kuwa walinifananisha. Hakuna statement, hakuna jalada wala kitu gani. NIlipotoka nje, nilikuta gari langu halina mafuta. Ninachokwambia ni kwamba, sikuchukua hatua yeyote kwa kuwa najua ni kutwanga maji kwenye kinu, lkn umewahi kujiuliza moyoni mwangu nawachukuliaje polisi?

Usipende kushabikia uovu, one day itakuwa zamu yako. Na kama ni mdogo kiumri basi weka kipimo cha mambo unayoshabikia.
 
Wanabodi

Nimeangalia ITV news hiyo kamata kamata ya jana ya waunini wa kanisa la Ephata, vijana wako wameonyesha udhaifu mkubwa!.

Baada ya kuwalipua wale waumini kwa mabomu ya machozi na kuwa contain, walitumia risasi za moto za nini kukabiliana na watu wasio na silaha yoyote?.

Kitu cha kusikitisha zaidi ni watuhumiwa hao kuendelea kushushiwa kipigo hata baada ya kuwa mikononi mwa palisi!.

Baada ya vijana wako kuwakamata watuhumiwa kuna sababu gani ya kuendelea kuwashushia kipigo mpaka wakiwa ndani ya defender ya polisi?.

Naomba niwakumbushe tuu baadhi ya visa vya police brutality and no one amechukuliwa hatua zozote!.

Kuna kisa cha watuhumiwa fulani 4 kilichotokea Arusha ambapo watuhuniwa hao walikamatwa toka nyumbani mwao mmoja baada ya mwingine wakiwa wazima huku wakitembea wenyewe siku ya Ijumaa.

Jumamosi ndugu zao wakafika kituo cha polisi kuwaletea ndugu zao chakula, walielezwa watuhumiwa hao wamepelekwa mahali kwa mahojiano.

Kesho yake Jumapili waliporudi polisi walielezwa ndugu zao wamepelekwa hospitali ya Mt. Meru.

Walipofika hospitali waliinyeshwa miili ya watu wanne waliouwawa kinyama na majeraha ya vipigo!. Polisi walipoifikisha miili hiyo hospitalini hapo, waliandikisha kuwa wameiokota eneo la Unga Limited baada ya kupigwa na watu wenye hasira!.
The story ended up there and then!. Hakuna chochote kilicho fuatia hata tuu japo kuulizwa kama ile kesi ya Zombe!.

Kwa nini mtuhumiwa aliyekuwa mzima afie mikononi mwa polisi bila uwajibikaji wowote wa jeshi la polisi?!.

Kamanda Mwema, haya yanatokea kwa sababu mnajua Watanzania hawajui haki zao, polisi wako hawajui haki za binaadamu na kama arrest kama za jana zenye police brutality zimefanywa mbele ya camera, and no body cares, huko behind bars ni nini haswa kinafanyika?. Si ndio itakuwa worse?!.

Yote haya yanawezekana kwa sababu Watanzania hatujui haki zetu, chochote kinachofanywa na polisi wanajua ndio haki yao tena watu hawajui kabisa kuwa raia wa kawaida anaweza kulishitaki jeshi la polisi!.

No one is above the law, please stop this police brutality inayofanywa wazi wazi and behind clossed doors!.

Thanks.

Pasco.

njia rahisi ya kuzui POLICE BRUTALITY ni kuzitumia sheria zilizopo kudai haki itendeke. usitegee polisi apige halafu ajipinge.

maoni yangu.

ukamataji upo wa aina mbili. wa kutumia hati na bila hati. hati hizo zipo za aina mbili, za POLICE ambayo ni namba ya kesi husika, wengi tunaita RB, na mahakamani.

ukamataji wa aina zote huwa unakumbwa na pingamizi, kwa anayekamatwa kujaribu kugoma kukamatwa, hata kama kafanya uhalifu na wote wameona uhalifu wake. katika mazingira ya namna hiyo, police kama ana weza, anaruhusiwa kutumia nguvu inayoendana sambamba na nguvu anayotumia mtuhumiwa uhalifu kupinga kukamatwa.

na kama hana uwezo wa kutumia nguvu hizo, police siku zote anashauriwa asilazimishe mambo, kwani anaweza kuumia na pengine kupoteza maisha. anaruhusiwa kwenda kutoa taarifa kwa kiongozi wake, na hivyo kiongozi atateua kundi mojawapo kwenda kufanya ukamataji. kundi hilo likija, halina dialogy, ni nguvu kwenda mbele kwani tayari umesha onesha wewe nawe ni bingwa. na kama hutaki yote hayo, huwa ni kuitikia wito, na kuangali namna ya kusolve kwani hakuna kilicho na mwazno kikakosa mwisho, lakini tii kwanza halafu hayo mengine yatafuata baadae.

niliwahi kupata kipeperushi cha polisi kinasema "utii wa sheria bila shurti" epuka fedheha, tii bila shurti, ukisubili kulazzimishwa kutii madhara yake ni makubwa mno

sasa, umekubali kukamatwa, hujaleta upinzani lakini unapigwa, nini kifanyike?

kama utaona kwenda POLICE hawatatenda haki, nenda moja kwa moja mahakani. mahakani dai kuwa umeumizwa ili wakupe fomu maalum ambayo kimsingi inatolewa na police PF3 ili uende kwa dr. dr akisha thibitisha kuwa umeumizwa vya kutosha, ni ushahidi wa kwanza.

pili, kama tukio la kwa mwingira, kuna video zinaonesha matukio yalivyokuwa. pata cd yake iwe ushahidi mwingine, kesha nenda mahakani kufungua kesi ambapo utafungua kesi dhidi ya kiongozi wa askari hao au askari wenyewe kama utawakumbuka. ukifanya hivyo, na kama sheria ikimtia hatiani, nadhani wataanza kuheshimu watu wengine, lakini usitegemee IJP kukusaidia.

 
Ujinga kama huu unatokaga mdomoni kwa mtu ambaye hajawahi kuwa victim wa polisi. Ndugu yangu, niliwahi kupigwa makofi na polisi pale Kilwa Road bila kujua sababu, wakaniweka chini ya ulinzi na baadaye jioni nikaachiwa kwa kuombwa radhi ya mdomo kuwa walinifananisha. Hakuna statement, hakuna jalada wala kitu gani. NIlipotoka nje, nilikuta gari langu halina mafuta. Ninachokwambia ni kwamba, sikuchukua hatua yeyote kwa kuwa najua ni kutwanga maji kwenye kinu, lkn umewahi kujiuliza moyoni mwangu nawachukuliaje polisi?

Usipende kushabikia uovu, one day itakuwa zamu yako. Na kama ni mdogo kiumri basi weka kipimo cha mambo unayoshabikia.

ulistahili kuchukua hatua, najua wangekutisha lakini mwisho wa siku ungepata haki yako, japokuwa wengi tunaogopa kujenga bifu na hawa polisi wetu kwamba watakufanyia zengwe uumbuke
 
Odinyo, sitetei walichofanya hao wavamizi, au sitetei uhalifu wa aina yoyote, ninachotetea, ni kuwa
1. Hao wahalifu hawakuwa na silaha yoyote ya moto, sasa polisi wanapiga risasi za moto za nini?.
Sipo sheria, taratibu na kanuni zinazotawala uvamizi wa polisi kwenye nyumba za ibada pale wahalifu
wanapokimbilioa kwenye nyumba hizo kujisalimisha!, zilifuatwa?
. Sikuona gari la matangazo, sikuona polisi
wakilizunguka jengo kuwataka wajisalimishe, baada ya kutumia mabomu ya machozi kwa wahalifu wasio na silaha
za moto, kinachofuatia ni ruber bullets na sio fire bullets!. Nilichoona ni fire bullets as if jamaa wako vitani, na hao
askari wenyewe nimeona wanavyo advance, wako nyoro nyoro tuu, wakikutana na watu wa ukweli wa shughuli hizo
wangeweza wiped out!.

2. Wahalifu umeshawashika, wako chini ya ulinzi wa polisi, kwa nini ni polisi hao hao waliendelea kuwashushia vipigo?.
Nilidhana mikononi mwa polisi ndizo safe hands za wahalifu kujisalimisha!, kichapo cha nini?. I wish kama hilo kanisa ni kweli linamwabudui Mungu aliyejuu, hao askari wote waliofanya waliyoyafanya, yatawakuta ya kuwakuta!.

pasco bwana? kwani jamaa walienda kuomba hifadhi au kuharibu? hujaangalia vizuri au hukuwepo kwenye tukio, lazima tahadhari kwanza, wakisha onesha ukaidi ndipo hatua zile zilifuatwa. labda kama unazungumza kama shahidi uliyeshudia sakata lilivyo kuwa. lakini kupitia picha zile niliona kama walitahadharishwa lakini wao ndo kwanzo wakazidisha moto
 
Someday the sirens of oppression will still, someday we will be free/ Dennis Brutus South African poet
 
Mwema naye ni askari polisi na alipita huko huko kwenye kuwapiga raia, kwahiyo hakuna jipya kwake hapo.

Ni muhimu tuzingatie kwamba mwema ameshakunywa mvinyo wa ulevi wa madaraka, hawezi kuwa msaada kwa wananchi dhidi ya uonevu wa vijana wake.

Mwisho na la kipekee kwa jeshi la polisi, mafunzo wanayopatiwa katika vyuo vyao vya polisi ni dhahiri kwamba ndio chanzo cha hivi vipigo. Kama tunataka kukomesha unyanyasaji wa polisi dhidi ya raia ni lazima kwamba kuipitia na kuirekebisha mitaala ya mafunzo ya polisi. Ni dhahiri kwamba hiki tunachokiona ndicho wanachofundishwa kwa sasa huko kwenye vyuo vyao.
 
Wana JF,

Kulingana na matukio ya kikatili (mauaji) yafanywayo na mapolisi nchini sababu kuu ni kuzuia maandamano ya wananchi kwenye mikutano ya CHADEMA, moja ya kazi zao polisi ni kulinda raia na mali zao lkn wamegeuka wao ndo wezi na wauaji wa raia wasio na hatia(rejea mauaji ya Arusha, Songea, Morogoro na sehemu nyingine).

Hivyo hadi hapo hakuna umuhim kua na jeshi la polisi kwani raia wanaweza kulinda haki zao na mali,hiki ni kipindi cha mabadiliko nchini suala lisiloepukika polisi wanapaswa kuzingatia hilo, nashangaa hata wakuu wa polisi (IGP)Wanakaa kimya ni kama wanaridhia yanayotokea.

Niwaase polisi kwani nao ni binadam kwa hiyo kifo kipo kwa wote wanapaswa kuacha kutumia madaraka vibaya nyakati hizi watz hawakandamizwi pia, risasi haziwezi kumaliza uma wote naamini risasi zitaua lkn wapo watakaobaki tena wengi, kibao kitageuka kwao polisi.

Je wewe mtanzania mtazamo wako ni upi kuhusu jeshi la polisi?
 
Kuna taarifa kuwa IJP ni shemeji wa mwenyekiti wa magamba....tutaponea wapi zaidi ya kumlilia Mungu wetu wa wanyonge?
 
Ni jambo la kusikitisha sana kuona kua katika kipindi cha miaka miwili tu 2011 na 2012 jeshi la polisi chini ya uongozi wa Said Mwema,limeamua kwa makusudi kuua raia wasiokua na hatia bila kuulizwa na wizara husika au serikali iliyopo madarakani.

Mbaya zaidi hata jeshi la polisi lenyewe limeshindwa tu hata kuwahoji hao polisi walioamua kuondoa uhai wa raia wasio na hatia na ambao hawakua hata na fimbo ya kumrushia polisi.

Ni wazi kua uongozi wa jeshi la polisi,wizara ya mambo ya ndani na serikali kwa ujumla imebariki hatua hizi za polisi kujichukulia hatua za kuua raia wasio na hatia kwa jinsi watakavyo.

Kinachosikitisha zaidi hata hao wanaojiita wanaharakati na Watanzania kwa ujumla tumekaa kimya kama vile tumehalalisha polisi kutuua kwa jinsi watakavyo bila kuhojiwa na chombo chochote.

Mauji ya Mbeya,Songea,Makumbusho, Dar es salaam,Arusha na jana Morogoro sasa imetosha,naomba hao wanaharakati mbalimbali na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha tunamfikisha panapostahili huyu askari aliyehusika jana kumuua kijana Ally Zona mchuuzi wa pale Msamvu Morogoro,tusikae kimya na kuhalalisha unyama na upuuzi huu,askari aliyeua jana anajulikana na kisheria kumpiga mtu risasi ya kichwa ni kuua kwa kudhamiria,japo kuna tetesi askari huyo jeshi la polisi Morogoro wameamua kumkingia kifua na kumficha ili jambo ili lipoe.

Kwa nguvu moja wanaharakati na Watanzania wote kwa ujumla tuungane kuhakikisha askari huyu anafikishwa kwenye mkono wa sheria,kwa kua mkono wa sheria hauna mipaka,na hakuna mtu yoyote ndani ya nchi aliye na haki kuliko Mtanzania mwenzake!shime wanaharakati,wanasheria na wananchi kwa ujumla tuunganishe nguvu ili kwa huyu askari aliyehusika jana mfano uanzie kwake.
 
Kuna taarifa kuwa IJP ni shemeji wa mwenyekiti wa magamba....tutaponea wapi zaidi ya kumlilia Mungu wetu wa wanyonge?
kupona kwetu ni kujilinda sisi wenyewe kwani tumetambua nia yao ni kuua na si kulinda tuache woga kwenye kutetea maslahi yetu na uhai,haipingiki kwamba kwa sasa adui wa mtanzania ni polisi,kwa sababu tumemjua adui yatupasa kujiandaa kumkabili,kama hawarejei misingi ya kazi yao wajihadhari kwani watz as soon tutachoka kupoteza wenzetu.
 
Tuandamane na na kuwatanguliza ndugu zao na wake zao au maandamano yafanyike karibu na makazi yao ili tuone kama ni jasiri kuua au wana uwezo wa kulinda mali zao.
 
Wao watakufa vifo vibaya sana, wakazane tu na hiyo tabia lakini mwisho wa ccm na polisi wao ni mbaya sana.
 
mi nadhani viongozi wa chadema nao wa kulaumiwa kwa hili, kwani toka watu waanze kupigwa risasi kwa kusapoti maandamo yao hakuna hatua yoyote ya msingi ambayowaeichukua zaidi ya kelele kwenye vyombo vya habari. hizi kelele hazisaidii kitu, watu watazidi kupigwa risasi na kuuwawa, kama chadema wameshindwa kutatua hili tatizo ni bora wakaacha kuitisha hii mikutano ambayo sasa naiona haina tija zaidi ya kusababisha vifo vya ndugu zetu tu.
 
Haiwezekani hata siku moja ukategemea polisi ajitambue kuwa na yeye ni mwanadamu akiwa ametumwa na kiongozi mwenye lengo la kukuua eti atakuacha.

Ni lazima polisi awaogope raia wakiwa na maamuzi yao kama jamii moja au taifa na hili halitawezekana kama raia watabaki kuangalia na kuvumilia vifo na kupoteza maisha eti kwasababu ya viongozi wa serikali walioshindwa kulinda ustawi wa maisha ya raia waliowatuma kuwaongoza.

Hivyo Raia anayetaka mabadiliko lazima atambue kwamba mabadiliko hugharimu hata maisha yake au ya yule asiyeyataka kama polisi,hivyo wananchi wahakikishe wanawakabili polisi kwa njia yeyote ile na matokeo yoyote yale ikiwamo kifo hapo ndipo polisi wa nchi hii watakapo heshimu umma wa watanzania na sio kutumiwa na CCM.

Mbona hatujawahi kusikia polisi wamezuia mkutano wa Nape au CCM kwa sababu zozote zile?Wakati umefika wananchi kumwaga damu kwa manufaa ya kizazi kijacho na sio kuogopa kifo hata kwa haki yako mwenyewe.
 
mi nadhani viongozi wa chadema nao wa kulaumiwa kwa hili, kwani toka watu waanze kupigwa risasi kwa kusapoti maandamo yao hakuna hatua yoyote ya msingi ambayowaeichukua zaidi ya kelele kwenye vyombo vya habari. hizi kelele hazisaidii kitu, watu watazidi kupigwa risasi na kuuwawa, kama chadema wameshindwa kutatua hili tatizo ni bora wakaacha kuitisha hii mikutano ambayo sasa naiona haina tija zaidi ya kusababisha vifo vya ndugu zetu tu.

suala la cdm kuitisha mikutano ni SAHIHI katika nchi yoyote inayofuata mfumo wa vyama vingi. Labda hilo la uongoz wa cdm kuchukua au kutochukua hatua ndo tujadili.
 
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikisema sana juu ya U-CCM na U-Chadema ambao umekuwa ukikomaa nchini siku hadi siku. Sijasita kusema wazi kwamba mara nyingi sana matendo na maneno ya viongozi wa CCM na serikali yake yamechangia sana kukuza ufa kati ya wafuasi wa CCM na Chadema nchini.

Nimeweka wazi kwamba U-CCM na U-Chadema nchini ni mbaya sawa tu u-dini. Hatuwezi kuupigia kelele u-dini na kudhani U-CCM na U-Chadema unaokua siku hadi siku ni hali ya kawaida ya siasa za vyama vingi. Lakini je, inawezekana pia kwamba mgongano kati ya polisi na Chadema ni nje na ushindani kati ya CCM na Chadema? Inaweza ikawa kweli kwamba wengi wa makamanda wa Polisi wanaelewa kwamba Chadema wakichukua serikali wengi wao wataondolewa madarakani na hivyo polisi hao wameanzisha kampeni yao binafsi dhidi ya Chadema?

Kwa namna yeyote ile, yaliyotokea Misri yanafanana sana na kule tunakoelekea. CCM ina daraka la kuzuia huu mgongano wa polisi na Chadema, bila kujidanganya kwamba mgongano huo ni kwa manufaa ya CCM. Yanayotokea sasa Tanzania ndivyo yalivyoanza kule Syria, Libya, Tunisia, Algeria na hata Afrika Kusini; kwamba inafikia mahali watu hawajali kifo katika kupigania kile wanachoona ni haki yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom