Polepole: Wapinzani wamekuwa na juhudi kubwa ya kuchonganisha na kuifitinisha serikali na wananchi

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603
Katibu wa Halmashauri kuu, itikadi na uenezi Ndg Humphrey Polepole anakutana na kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

NB;
Waandishi wameshaingia ukumbini na Mkutano unategemea kuanza muda si mrefu, nitaripoti kwenu moja kwa moja kila litakalokuwa linaendelea kutoka ukumbu huu wa mikutano wa CCM Lumumba.

----------------------







Updates kutoka kwa Troll JF

Hatutashiriki malumbano ya kisiasa/wanasiasa yasiyo na tija na yanayolenga kuzorotesha jitihada za kuleta maendeleo kwa watu.

Wanasiasa wa vyama ambavyo si CCM wamekuwa na juhudi kubwa kufanya uchonganishi na kuifitinisha Serikali na Wananchi. Tunatoa wito kwa wananchi kuwapuuza wanasiasa wanaotumia matatizo na majanga kuwa mtaji wao kisiasa, Serikali ipo ili kuwahudumia.

Siasa yetu ni ya Ujamaa na Kujitegemea, tutaendelea kuhimiza Watanzania kujitegemea na kuongeza juhudi katika kazi.

Siasa safi zitatupatia uongozi bora, siasa za kufitinisha watu zina gharama kubwa na hatari kwa Taifa.

Inapotokea baa la njaa ama janga lingine, Mkuu wa Nchi anayo dhamana ya kulitangazia Taifa na kuweka utaratibu wa kulikabili. Kutoa taarifa za uongo kwa lengo la kuleta taharuki kwa watu ni kosa la jinai, ni vyema wanasiasa kujifunza kusema UKWELI.

Tunazo zaidi ya tani milioni 1.5 za chakula ambazo zinaweza kusambazwa maeneo yatakayothibitika kuwa na upungufu wa Chakula.

Tunahimizana kujitegemea na kukataa kuwa ombaomba. Anapotokea Kiongozi akasema ataenda kuomba nje ya nchi tunamshangaa.

Imani ya CCM inasema "binadamu wote ni sawa". Serikali yetu itaendelea kutoa huduma iliyo sawa kwa watu wote.

Mageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya CCM yanalenga kukiimairisha Chama kuisimamia Serikali na kushughulikia matatizo ya watu.

"Tutasema kweli daima, fitina kwetu mwiko" tutaendelea kusimamia imani hii ya Chama chetu na kuhimiza watanzania kuifuata.
 
Katibu wa Halmashauri kuu, itikadi na uenezi Ndg Humphrey Polepole anakutana na kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

NB;
Waandishi wameshaingia ukumbini na Mkutano unategemea kuanza muda si mrefu, nitaripoti kwenu moja kwa moja kila litakalokuwa linaendelea kutoka ukumbu huu wa mikutano wa CCM Lumumba.
Pamoja Mkuu
 
Njaa ni nini?


Njaa ni kukosa chochote cha kula, vyakula hakuna masokoni, mazao yamekauka nchi nzima, watu wanachinja kwa lazima ng'ombe na mifugo yao mingine kama chakula, mifugo kufa kwa ukame na rasmi inatangazwa na serikali KUWA BAA LA NJAA LIMETUFIKA.. sio mtu yeyote yule kutangaza, na hapo serikali inachukua jukumu la kusambaza chakula bure na ikibidi hadi wanajeshi wanapewa jukumu la kusambaza vyakula bure nchi nzima kwa haraka na vyakula vinatoka nje ya nchi, sio hapa nchini, sbb hakuna vyakula masokoni, na naposema hakuna vyakula SIMAANISHI MAHINDI TU, naamanisha vyakula vyote, Mchele, Maharagwe, Mahindi, Viazi, Uwele, mbaazi, Unga wa ngano, Ndizi, Mihogo, matunda, mboga mboga, maboga, choroko, mtama, ulezi, etc etc..

Sasa mm napita masokoni vyakula vimejaa, narudia vyakula vimejaa masokoni..!! Njaa haswa bado, labda ije baadae mwezi wa 3 huko kama inavyotabiriwa mvua zikikosekana hadi March
 
Back
Top Bottom