Brother Mshana usiashangae sana hawa hawajui walitendalo. Unamuhongaje amiri jeshi mkuu halafu ukaendelea kula ugali? Au kahongwa na Trump nini? maana ndo mtu pekee ambae hatuwezi mkamata... wengine niliona wakipewa persona non granta wakafukuzwa sasa huyo ana immunity gani ya kuzuia his/her prosecution?Basi yasitangazwe...kutaka kumhonga rais ni tusi kashfa na dharau kubwa
Hapa ndio pa kuonyesha meno na makucha yake makali
Kuishia kusema ALITAKA lakini AKAKATAAA ni kuongeza ukakasi kwenye sakata zima
Kama kuna mambo ya kuweka wazi bila kificho na kwa haraka hili ni mojawapo
Huyo polepole alikuwepo au alisimuliwa na nani? Atoe taarifa kamili jibu la Magufuli lilikuwa nini?Humphrey Polepole kasema kuwa Magufuli alitaka kuhongwa Billioni 300 ili asifanyie kazi taarifa ya mchanga wa madini .
Polepole ambaye ni Katibu wa Uenezi wa CCM,amesema hayo kwa uchungu akitoa msimamo wa chama juu ya uchunguzi uliofanyika
Hoja: Kina nani walitaka kumhonga rais?Wamechukuliwa hatua gani?
Vitu vingine vinatia aibu. Hivi mtu unaweza kujitokeza hadharani ukatamka nilitaka kuhongwa wakati vyombo vyoote vya usalama unavimiliki! Wasitake kutufanya sisi hamnazo kwa kuamini hadithi za alfu lela ulela.Si akamatwe huyo mtoa rushwa au kakukuru hawapo
hivi ni nani aliyewaloga? Mmekuwa watetezi wa mabeberu dhidi ya taifa lenu, yaani damu yenu? Aibu hiiIngekuwa ni ukweli mbona dunia nzima ingejua?
Kumbe mnajua kuna utaratibu wa kufanyia kazi mambo haya.sasa mnatangaza kuwa amekataa rushwa ya b.300 ili iweje? Mlidhani ni sifa. ?Wakati mwingine watu mnajipambanua mlivyo wajinga na msiojielewa. Hivi mnajua Taasisi kama Urais, Takukuru, Polisi n.k? Vinafanyaje kazi? Mbadhani kila tukio ni Takukuru au Polisi na kukamata na kuhoji? Uelewa mdogo ni Dhambi.
SalutePolepole kijana wangu,usilibebe hili jambo "kisiasa" zaidi.Hili jambo tuende nalo "kiuweledi" zaidi,ili huko mbele ya safari tusije tukapoteza na kumpotezea Rais wetu heshima kimataifa.Kila mtu anamuunga mkono Mh.Rais,wengi wanachotofautina naye labda ni "Approach" ya suala hili.
Ndio maana Tundu Lisu kasema tujitoe kwanza huko kwenye "MIGA" ndio tuanze "harakati" za kudai "mapanki" yetu ya dhahabu.Kama hatutakuwa tumejitoa,basi hao "mababeru" lazima watuadabishe,sbb tutakuwa tumevunja mikataba ambayo sisi wenyewe,kwa utashi na akili zetu timamu,tuliikubali na kuanguka saini.
Tukishamaliza huko,tuje tujitoe kwenye hizi "Bilateral Treaties" ambazo tuliingia kwa "mbwembwe" na USA,Canada na UK.Tukimaliza hapo,tuje kwenye bunge letu na tupeleke mswaada kwa hati ya dharura ili kufanya marekesbisho ya sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997 na sheria ya Misamaha ya Kodi za madini ya 1998 na ile Sheria ya Madini ya 2010 iliyoletwa Bungeni sbb ya "Buzwagi Saga-2007"
Vinginevyo,tutabaki kupiga kelele na kujazana upepo tu.
Wewe askari muoga: haya huwa yanatokea sana katika nchi zetu masikini zenye utajiri mkubwa wa asilimali. Nchi hizi hadi huwa zinanunuliwa na wakubwa. Rasilimali zetu ndizo zilisababisha tufanywe makoloni ya wakubwa hawa. Tulipewa uhuru wa bendera lakini wakubwa hao wanahakikisha rasilimali zetu wanaendelea kuzichota kama awali kwa mbinu zingine kama hizi (neocolonialism).kwanza ni aibu Rais kutangaza kuwa aliongwa ni kushusha thamani ya Urais kma watu wana uwezo wa ku attempt kumuonga Rais basi cheo cha Urais hakiheshimiki
B.300 kwa CCM hiyo ni hela ya mboga.kwani tangu 1998 mpaka juzi mliposimamisha uchimbaji wa dhahabu mmekula sh.ngapi?Wewe askari muoga haya huwa yanatokea sana katika nchi zetu masikini zenye utajiri mkubwa wa asilimali. Nchi hizi hadi huwa zinanunuliwa na wakubwa. Polepole anaweza akawa amevujisha ukweli. Na kama ni kweli tukio hilo lazima litakuwa limenaswa na kamera za ikulu. Muda mwafaka zinaweza kuwa presented kwenye hiyo International arbitration court ambayo wakina Tundu Lissu wanatuaminisha itatunyoa bila maji.
Ila I'm just imagining kama angekuwa Mr Grey H. angekuwa na gut kweli hizo USD 150 million sawa na hizo tsh 300 billions angezikataa kweli? Ingewezekana kweli akazikataa?