Polepole: Walitaka kumhonga Rais Magufuli Sh. Bilioni 300 ili asifanyie kazi taarifa ya mchanga

Hivi katibu mwenezi ina maana ya kusema chochote kile!

Porojo at its best. He should also given their identities and should have said that they have been arrested and are behind bars. To bribe a sitting president should have been BREAKING NEWS.! Labda kama wewe Okwan Sunzu umetunga hii habari!
 
This Ugly kid is full of BS, Walitaka Kumhonga Rais akawafanyaje? Akawaacha wakaenda! Mtu kumfuata Rais na Kumtaka amhonge ni Sawa na Mtu amfuate Askofu atake amfanyie yasiyofaa kinyume na maumbile! Inapaswa Rais antwange makofi na aamuru akamatwe kama huyu ati aliachiwa aende zake hii ni ngonjera na uharo mtupu sio kweli!
 
Huyu dogo unafiki wake umepitiliza na kujipendekeza kumepitiliza analeta upotoshaji na hajui anachafua Ikulu siyo anapendezesha.
Kutaka ukuonwa kwa Rais/Ikulu na nani hao???????
Hii tswira na tafsiri mbaya sana kwa ndani ya nchi na hata nje ya nchi.
Kufungunga bakuli muda mwingine haina maana hujui kitu,ninamuambia Polepole funga bakuli lako utakuja kuchafua khali ya hewa kwa unafiki na uzambiki wako.
 
Ikiwa zimepita siku mbili tangu Rais John Magufuli kueleza kuwa kwa sasa nchi iko katika vita ya uchumi na kwamba ana majina ya watu waliotaka kuingilia na kuharibu uchunguzi wa Kamati Maalumu aliyoiunda ili kuchunguza thamani na viwango vya madini vilivyomo kwenye mchanga wenye madini (Makinikia) katika makontena 277 yaliyozuiliwa kusafirishwa nje ya nchi, ili kupoteza ushahidi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole Mei 25, 2017 aliibuka na kudai kuwa kuna wahujumu uchumi walitaka kumhonga kiasi cha Bilioni 300 Rais Magufuli, ili kusitisha zoezi la uchunguzi huo, huku akihoji masilahi wanayopata watu wanaofanya biashara ya kusafirisha makinikia hayo nje ya nchi.

“Vita ziko za aina nyingi, ziko zile tunazopigana kwa silaha mtu na mtu, na nchi na nchi, lakini sasa ziko vita za kiuchumi, ni mbaya zaidi zinalenga kuturudisha nyuma.Wahujumu uchumi hawapigani na rais, bali wanapigana na maisha ya wananchi wa Tanzania, tukiwa wamoja tutashinda vita hii, wako watu wanaipinga vita hii yenye dhamira njema, huu si wakati wa kutofautiana ni wakati wa kusimama kumshinda adui,” alisema.

Polepole aliyasema hayo, wakati akitoa wito kwa wananchi, kumuunga mkono Rais Magufuli katika kipindi hiki kigumu kwani nchi iko katika vita mbaya ya uchumi ambayo wahujumu uchumi wamelenga kupigana na maisha ya watanzania na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

“Kuna watu walitaka kumhonga rais bilioni 300 ili kusitisha uchunguzi. Walitaka kuhonga bilioni 300 kwa ajili ya kusitisha uchunguzi huo, hivi wao wanapata fedha kiasi gani? Lakini rais akawatolea nje, akasema subirini uchunguzi ukamilike. Tusiamame naye na hakika tutashinda na historia itaandikwa kwamba tulisimama katika kulinda urithi wetu,” amesema.

Katika hatua nyingine, Polepole aliwajibu baadhi ya wanansiasa wanaoikosoa CCM kutokana na viongozi wake waliopita kutunga na kupitisha sheria za madini ambazo zinatetea masilahi ya wawekezaji kuliko nchi, kwa kusema kuwa viongozi walioko sasa ni tofauti na waliopita, na kwamba serikali iliyoko madaraka itarekebisha sheria hizo.

“Tumehujumiwa sana, tumedhurumiwa sana mali za watanzania ambazo tumezirithi kutoka kwa mababu zetu na tuna dhamana ya kuhakikisha zinawafikia watoto wa watoto wetu,” alisema

Hoja:
Kina nani walitaka kumhonga rais?Wamechukuliwa hatua gani?
Mbona hizi rushwa zinaishia walitaka? Mitego si iko?
 
Tusikurupukie hili suala la rushwa japo laweza kuwa na siasa mingi lakini kuwa watu wanaitwa lobbyists ni watu wa hatari sana. Mfano mdogo tu ni Zitto Kabwe (anayeweza kukusanya kura za kumng'oa waziri mkuu) japo yeye bado sio expert kama watu ambao wameSpecialize kwenye hiyo field. Kwa wenzetu maSenator huwa wanahongwa na ukielezewa wanavyohongwa bila kuvunja sheria unachoka kabisa. Mfano ili raisi wa marekani aweze kuendesha nchi vizuri lazima awe na watu kama hao wamsaidie kulainisha uungwaji mkono bungeni.
 
Wametaka kumuonga Rais bilioni 300.
Rais yuko kimya.
TISS wako kimya.
TAKUKURU wako kimya.
POLISI wako kimya.
Bunge liko kimya.
AG yuko kimya.

Anaibuka Polepole na kuanza kuimba taarab badala ya watu kuchukuliwa hatua.

Logical...!!
 
Muongo mkubwa huyo kama hayo yasemwayo ni ya kwel huyo mtoa rushwa kwanini wasimtaje na akamatwe?? Aende kudanganya watoto wake na cyo cc
 
Yaani sjawah kuona mtu wa ajabu kama polepole ni ndumila kuwili huyu ni nyoka makengeza huyu ,hana aibu ni mchumia tumbo.
 
polepole peleka ujinga kule unaropoka tuu kumwabisha rais wetu. nnavomjua magu angeikubali hio hela na kuwasweka ndani waliotaka kumhonga. na hio ndo ingekuwa sbu ya kuonyesha ulimwengu hawa c wema na tungevunja mikataba yote na kuwashtaki. siamini kama hio ni kwel na kama imetoka kwa pole pole. ila kama imetoka kwa polepole bas kijana amefikia mwisho wake wa kuwaza.
 
Hao watakuwa ni makachero wa Mkapa na Kikwete tu kwani hao marais ndio waliozorotesha hii nchi kwa kujiingiza kwenye mikataba kwa ajili ya familia zao tu na si nchi yetu.
 
Ikiwa zimepita siku mbili tangu Rais John Magufuli kueleza kuwa kwa sasa nchi iko katika vita ya uchumi na kwamba ana majina ya watu waliotaka kuingilia na kuharibu uchunguzi wa Kamati Maalumu aliyoiunda ili kuchunguza thamani na viwango vya madini vilivyomo kwenye mchanga wenye madini (Makinikia) katika makontena 277 yaliyozuiliwa kusafirishwa nje ya nchi, ili kupoteza ushahidi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole Mei 25, 2017 aliibuka na kudai kuwa kuna wahujumu uchumi walitaka kumhonga kiasi cha Bilioni 300 Rais Magufuli, ili kusitisha zoezi la uchunguzi huo, huku akihoji masilahi wanayopata watu wanaofanya biashara ya kusafirisha makinikia hayo nje ya nchi.

“Vita ziko za aina nyingi, ziko zile tunazopigana kwa silaha mtu na mtu, na nchi na nchi, lakini sasa ziko vita za kiuchumi, ni mbaya zaidi zinalenga kuturudisha nyuma.Wahujumu uchumi hawapigani na rais, bali wanapigana na maisha ya wananchi wa Tanzania, tukiwa wamoja tutashinda vita hii, wako watu wanaipinga vita hii yenye dhamira njema, huu si wakati wa kutofautiana ni wakati wa kusimama kumshinda adui,” alisema.

Polepole aliyasema hayo, wakati akitoa wito kwa wananchi, kumuunga mkono Rais Magufuli katika kipindi hiki kigumu kwani nchi iko katika vita mbaya ya uchumi ambayo wahujumu uchumi wamelenga kupigana na maisha ya watanzania na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.

“Kuna watu walitaka kumhonga rais bilioni 300 ili kusitisha uchunguzi. Walitaka kuhonga bilioni 300 kwa ajili ya kusitisha uchunguzi huo, hivi wao wanapata fedha kiasi gani? Lakini rais akawatolea nje, akasema subirini uchunguzi ukamilike. Tusiamame naye na hakika tutashinda na historia itaandikwa kwamba tulisimama katika kulinda urithi wetu,” amesema.

Katika hatua nyingine, Polepole aliwajibu baadhi ya wanansiasa wanaoikosoa CCM kutokana na viongozi wake waliopita kutunga na kupitisha sheria za madini ambazo zinatetea masilahi ya wawekezaji kuliko nchi, kwa kusema kuwa viongozi walioko sasa ni tofauti na waliopita, na kwamba serikali iliyoko madaraka itarekebisha sheria hizo.

“Tumehujumiwa sana, tumedhurumiwa sana mali za watanzania ambazo tumezirithi kutoka kwa mababu zetu na tuna dhamana ya kuhakikisha zinawafikia watoto wa watoto wetu,” alisema

Hoja:
Kina nani walitaka kumhonga rais?Wamechukuliwa hatua gani?

kama kweli hili limesemwa na pole pole basi atakuwa ametumwa msishangae na hizo figures za mchanga kamati pia imezitengeneza kwa maslahi ya kisiasa!
 
Back
Top Bottom