Polepole vs Nape Nnauye: Nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
Baada ya kusoma nyuzi kadhaa ambazo zinahoji utendaji wa Polepole katika nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, naomba tujadili hawa watu wawili, Polepole (Katibu wa sasa -Itikadi na Uenezi CCM) na Nape (aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kipindi kilichopita).

Tujadili kwa kina juu ya ambaye aliitendea/anaitendea haki vizuri nafasi hiyo na nani alipwaya/anapwaya kwenye nafasi hiyo

Karibuni.
 
Mimi ninachojua wote walipata uongozi sababu ya kumsema vibaya ENL
Sifa nyingine ni wanasiasa walio kwenye kundi la wasaka tonge
 
Naona unatoa nafasi kwa majungu. Kwa nini tusingoje walau Polepole amalize mwaka kazini ndo tufanye upembuzi linganishi?
 
nape ni mtu wa kawaida sana sema kafika alipofika kwa unafki, always haonekani kuwa mtu serious......angefaa kuendelea kufanya kazi ndani ya chama kuliko serikalini.
 
Nafikiri Polepole alipata nafasi sio kwa kuangalia uwezo wake kwny uenezi walilewa zaidi na image yake kwny society wanajua ana wafuasi wengi na kajitahidi ku maintain nadhan mpk uchaguz ulipoisha kapoteza almost 3% of waliokuwa wanampenda.

Nape alikwiza kweli kweli katika Uenezi alijitahidi kutokua msemaji wa serikali lakini Polepole anatembelea mwavuli wa serikali na they push him chama kimebaki jina tu sababu hata propaganda and political games kwa kiwango kikubwa zinaendeshwa na serikali which means Polepole hawez kuongeza uwezo kiubunifu zaidi utakuwa huyuhuyu tu
 
Mimi kwa Mtazamo wangu naona NAPE was the best. But ngoja tusubiri Mheshimiwa Pole pole naye amalize japo mwaka mmoja. Ndipo tuje ukumbini hapa.
 
Polepole anatumia akili sana kuliko Nape.

Pia kumbukeni wakati wa Nape siasa za majukwaa ziliruhusiwa, tofauti na sasa ambapo polepole anashindwa kufanya siasa. JPM kazuia siasa matokeo yake hata chama chake kinashindwa kuueleza umma kuhusu hali ilivyo kwa kupitia majukwaa ya siasa.

Mfano sasa hivi hali ya pesa ni mbaya mtaani, polepole alitakiwa aelezee kinachoendelea, lakini hawezi kwa kuwa Rais kazuia mikutano ya siasa
 
Back
Top Bottom