Polepole usimlazimishe Rais kuleta Katiba mpya

KUPOTELEWA NA CARD YA CHAMA:

Ndugu zangu wapendwa naomba kuleta taarifa hii kwenu
Mnamo tarehe 16/04/2017 nikitoka Fery kwenye shughuli zangu za hapa Kazi tu nilipoteza porch yangu kwenye daladala za Gongo la mboto fery
Ndani ya ile porch hapakuwa na chochote zaid ya kitambaa changu cha jasho na kadi yangu ya chama cha Mapinduzi nilioipata mkoani Tabora wilaya ya Uyui katika ofisi za chama nimekuwa nayo Leo mwaka wa saba kwa yeyote alieikota naomba tuwasliane kabla ya 2020
Nitashukuru Mimi mpendwa wenu
Mwana Maheraa-
Mhhh!!!!@lizaboni mpe kadi mpya huyu
 
Wengi wetu humu tumezaliwa kuanzia miaka ya 80_2000 katiba ya 77 tumeikuta rasimu ya kwanza ya katiba mpya tumepoteza zaid ya billion 27 badala ya kuiendeleza tunataka fedha zile zipptre bure.ccm acheni kuogopa nchi ni ya watanzania wote na wote tunataka katiba mpya kama nchi haina fedha watanzania tuchangishwe tutazitoa
 
Nimemsikia Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akisema kuwa mchakato wa Katiba utakuja baada ya Rais Magufuli kuinyoosha nchi. Hata muda huu anaongea kwenye kipindi cha Sema kweli (Chanel 10). Hivi lini Rais Magufuli aliahidi kuleta Katiba mpya?

Mwenyewe alishasema suala hilo halikuwepo kwenye ahadi zake za uchaguzi. Sasa wewe Polepole umeteuliwa juzijuzi unawaahidi Watanzania kuwa wakishanyooshwa ndiyo katiba italetwa, je Rais akikataa?

Wakati Polepole akiwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alikuwa akisisitiza madai ya Katiba mpya, hakujua kama kuna kunyooshwa? Mabilioni ya fedha yametumika ya nini kama mlikuwa mnajua nchi inatakiwa kunyooshwa kwanza? Huu ni unafiki tu.

Eti warejeshe kwanza nidhamu, aliyeiharibu ni nani? Amechukuliwa hatua gani?
Polepole aache kuwa kigeugeu.

Polepole halazimishi chochote. Sidhani kama ushiriki wa Mzee Warioba kwenye kampeni za uchaguzi wa 2015 baada ya kutukanwa sana na kudhalilishwa na makada wa ccm ulikuja hivi hivi tu. Bila shaka kulikuwa na ahadi nzito. Kitendo cha kuwavuta karibu baadhi ya wajumbe wa Tume ya Katiba mpya nacho siyo cha hivi hivi tu. Jambo moja lipo wazi pia kuwa Rais wetu hana lugha ya kidiplomasia. Hata hii ya kunyoosha nchi siyo lugha nzuri. Ndiyo maana mara kwa mara wasaidizi wake hujitokeza kufafanua matamshi yake muhimu ili watu wapate ujumbe ambao wanaamini ndio uliokusudiwa.
 
Wewe ndo hujaelewa.
Atawaachia mchakato huo kipindi Chake cha mwisho cha utawala wake 2025
 
Inaonyesha muda si punde Tanzania itakuwa imenyoka toka dar mpaka hororo dar mpaka tunduma ni rula kwa kwenda mbele kama sivyo basi tujue anayosha wapi na kivipi?

Kama anaubavu ajinyooshe Mwenyewe. Mwizi ni mwizi tu,haoni yale madeal yake ya Kivuko kibovu duh!Kweli uke usemi toa kwanza boriti ndipo uone Kibanzi kinafanya kazi Kweli Kweli.
 
Sione kosa la Polepole anapoongelea mambo yanayo husu Nchi na Chama chetu sivema kubeza kila maoni na kiongozi yeyote hasa wa Kitaifa hata kama umeona hujaguswa na alichoongea tusipende kujenga majibizano yasio weza kujenga wala kusaidia chochote kwa Taifa letu !Katiba ya Nchi haipaswi kuwa na utikadi fulani yeye ndie anajua kwanini aseme hili la Katiba naje Rais akikubali kuna wakukataa?Tutoe Nafasi kwa wahusika watajadriana wao
 
Back
Top Bottom