Richard Robert
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 632
- 340
Unasema CCM haijawahi kuchukua mali za umma na kujimilikisha.. Kauli hii inatia aibu na hata kujenga mashaka kuwa tunaweza kuwa na Bashite mwingine ambaye hajui nchi yetu inatoka wapi na inakwenda wapi.
Naomba nitoe mifano michache tu.
1. Shule za sekondari zinazomilikiwa na chama cha mapinduzi nyingi ni mali ya umma. Kwa mfano META HIGH SCHOOL ya Mbeya ilikuwa inaitwa Mbalizi Road Primary School. Mwaka 1984 wanafunzi wa shule ya msingi (ya serikali na mali ya watanzania wote ikageuzwa kuwa shule ya sekondari chini ya jumuia ya wazazi ya CCM.
SANGU SEKONDARI ilikuwa chini ya kanisa lakini sasa ni mali ya jumuiya ya wazazi wa CCM.
Kaole sekondari ya Bagamoyo, Pwani.. ilikuwa ni kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji sawa na chuo cha ualimu Mtwara... lakini sekondari hii ni mali ya CCM.
2. Viwanja vya mpira nchi nzima - Umoja, CCM Kirumba, Sheikh Abeid Karume, n.k. ni Mali ya Umma.
Uwanja wa Sokoine umejengwa kwa nguvu za umma kwa kushirikiana na serikali. Na wanafunzi wa shule za msingi zilizopo manispaa ya Mbeya (leo jiji) walishiriki kujenga huku wakikatisha masomo. Ni uwanja wa Umma.
3. Vilabu vya pombe (wao wanaviita vilabu vya maendeleo ya wananchi) viko Mbeya, Rukwa, Iringa, Lindi, Mtwara, Pwani n.k. vilijengwa kwa nguvu za wananchi na vingine leo vinatumika kama ofisi za kata za CCM, Mfano ofisi ya CCM - Nianjema, Kerege kwa kiwete na Kerege chama ni mali ya umma.
Mf. Kilabu cha Mlongawima - Nzovwe Mbeya, na Kilabu cha Maendeleo Kalobe vilijengwa na wananchi lakini vikataifishwa na CCM, 1990.
Kwa ufupi zaidi ya asilimia 90 ya mali za CCM ni mali za umma.. Ushahidi upo!