Polepole toa somo kwa wamachinga

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Wamachinga ni watanzania wenzetu wenye haki na wajibu kamili kwa taifa lao. Machinga ni watoto, kaka, dada, wapwa, shangazi, wajomba, wajukuu, bibi, babu, ndugu na rafiki zetu. Ni kundi la wanajamii ambao wamejiamulia wenyewe mahala pa kufanyia biashara sawa na makundi mengine ya watanzania ambao wamejiamulia wenyewe mahala pa kujenga nyumba, kulima, kuchimba visima, kuchimba madini, kuchungia mifugo, kuvulia samaki, kuwinda, kumiliki silaha, kujichukulia sheria mikononi, kujisaidia haja ndogo na kubwa, kujiendeshea magari bila leseni na mambo yote ya kujiamulia bila kufuata taratibu zilizopo kuhusu jambo hilo.

Hivi makundi yote haya yaliyojiamulia wenyewe cha kufanya ni makosa kama siku serikali itawaambia acheni kufanya hicho mlichojiamulia kufanya wenyewe bila kufuata taratibu za jambo hilo? tukumbuke kuwa kuna wananchi pia wanaokamatwa na bunduki za magobore ambazo zilikuwa zinawasaidia kwenye kulindia mali zao kama mifungo dhidi ya wezi na wanyama wakali, mashamba yao dhidi ya wanyama waharibifu, mizinga yao zidi ya wezi wa asali, wagoni wa wake zao, nk. Je, ni makosa serikali kuwanyang'anya wananchi hawa magobore yao hivihivi bila kuwapitia kwanza silaha nyingine mpya na nzuri za kisasa kuendelea kulinda mali zao kabla ya kuwanyang'anya silaha zao duni walizozimiliki bila kufuata utaratibu? Mbona kundi hili la watanzania Mh. Polepole hasemi kuwa linaonewa na serikali?

Polepole hawatetei pia watanzania wenzetu wanaokamatwa kwa makosa ya kutafuta riziki kwa kuendesha magari bila leseni kabla ya serikali kuwapa leseni kwanza, wanaobomolewa nyumba zao mabondeni na kwenye vyanzo vya mito kabla ya kupatiwa nyumba sehemu nyingine, wanaokatazwa kujisaidia porini na kuchimba dawa kabla ya serikali kuwachimbia kwanza vyoo, kunyang'anywa nyavu zao za kuvulia zenye matundu madogo kabla kwanza ya serikali kuwapa nyavu safi zinazoruhusiwa, kuwapa wafugaji maeneo ya kuchungia kwanza kabla ya kuwapiga marufuku kuchungia kwenye mashamba ya wakulima ili waendelee kupata kipato chao na familia zao?

Ni Kwanini Humphrey Polepole na wenzake wanawatetea wamachinga tu na sio makundi mengine yote yanayopitia kadhia kama ya wamachinga kwenye kutafuta riziki zao, Kwanini hatetei makundi mangine "yanayonyanyaswa" na serikali kwa kunyang'anywa nyavu zao, wanaokamatwa na traffic wakitafuta riziki zao kwa kuendesha magari bila kuwa na leseni, wanaopigwa marufuku kuchungia mashamba ya watu, nk.kama wale waliochomewa nyavu zao ambazo pia zilikuwa zinawapatia riziki zao sawa na wamachinga wanavyotafuta riziki zao? Bw. Polepole ana agenda gani na wamachinga?

Wamachinga ni wahalifu sawa na wahalifu wengine wanaojimilikisha bunduki bila utaratibu, wanaowinda bila utaratibu, wanaovua samaki kwa nyavu zenye matundu madogo, wanaoendesha magari bila kuwa mafunzo, wanaochungia mashamba ya wenzao, na wote wanaojichukulia sheria mikononi. Serikali inaposema sasa basi kuvua samaki kwa nyavu hizo au inapozuia kuvua samaki kwenye bwawa kwa kipindi fulani ili samaki wakue na kuongezeka hailazimiki eti kuwapa kwanza nyavu nyingine au kuwahamishia kwanza kwenye bwawa lingine wakaendelee kuvua kama vile Polepole na wenzake wanavyotaka serikali iwape machinga sehemu nyingine kufanyia biashara kabla ya kuwaondoa kule walikofanya uhalifu wa kuvamia maeneo yasioruhusiwa.

Kama Polepole na waenzake wakitaka waeleweke kuhusu wamachinga wangepaswa wayasemee makundi mengine pia ambayo yanaadhibiwa kwa kutafuta riziki bila kufuata taratibu, vinginevyo Polepole anafanya vurugu kwa chama na serikali yake kwa kupitia hoja ya wamachinga kama kichaka tu.

Serikali pia inafanya makosa kwa kuwatafutia kwanza "wahalifu" machinga pekee sehemu ya kuendelea kupata kipato chao na kuyaacha makundi mengine ya wavuvi, wafugaji, wenye magobore, wanaoendesha magari bila leseni, wanaobomolewa nyumba zao mabondeni nk.

Polepole anapaswa kutoa elimu ya ujasiliamali kwa machinga na makundi yote yanayotafuta riziki bila kufuata taratibu ili yahamu faida na hazara zake. Polepole lazima atoe definition kamili ya nani ni machinga na nani sio machinga. atoe elimu kwa machinga wayajue makosa yao, haki zao na wajibu wao kwa makundi ya watu wengine ili wajue faida na kero wanazosababisha kwa makundi ya watanzania wengine kwenye mitaa.
 
Umendika upuuzi but I admire your passion to write!
 
sema tu mnaemtumikia, baasi!!!!. watu walikuwa wanchomewa nyavu zao zinazowaingizia kipato cha kila siku, mbona hukunyanyua mdomo wapewe nyavu nyingine na serikali. Waliochomewa nyavu zao waliishi vipi na familia zao? kwanini unadhani machinga watakufa wote kama wakiondolewa kwenye maeneo waliovamia. cheap politics hata mtoto mdogo anagundua.
 
Kwa sheria ya Tanzania hao Ni wahalifu, sasa Nani anyanyue mdomo kutetea wahalifu!
 
kwahiyo wamachinga sio wahalifu? kukwepa kodi, kufanyabiashara bila kibali, kuziba njia za kupita maji taka na mvua na kujenga kwenye njia za waenda kwa miguu na road reserves sio uhalifu!!! Semeni mnamtumikia nani, baaasi!!
 
Mimi Na wewe tunaishi Dunia tofauti, tusibishan
 
hauko tz? uhuru wa kutoa maoni lazima uzingatie kanuni, taratibu, kumbukumbu na consistency. Mtu makini anafanya kilekile na vilevile jana, leo na kesho.
 
Mimi Na wewe tunaishi Dunia tofauti, tusibishan
Cha msingi hapo piga kelele waliopokonywa na kuchomewa nyavu zao warejeshewe au wapewe nyingine au wapewe fedha za kujikimu na serikali, na wale waliofungiwa mialo yao wapewe naeneo mengine ya kuvua, wafugaji wapewe maeneo ya kuchungia, wenye magobore wapewe bunduki nyingine za kulindia mali zao kama unavyofanya kwa wamachinga. Maana wote ni wakosaji kwa mujibu wa kanuni na taratibu na wote hawa walikuwa wanatafuta riziki kutokana na hali zao mbaya.
 
Cha msingi hapo piga kelele waliopokonywa na kuchomewa nyavu zao warejeshewe au wapewe nyingine au wapewe fedha za kujikimu na serikali, na wale waliofungiwa mialo yao wapewe naeneo mengine ya kuvua, wafugaji wapewe maeneo ya kuchungia, wenye magobore wapewe bunduki nyingine za kulindia mali zao kama unavyofanya kwa wamachinga. Maana wote ni wakosaji kwa mujibu wa kanuni na taratibu.
Umachinga siyo uhalifu bana...hao wengine uliowataja ni wahalifu kwa mujibu wa sheria hiki kitu mbona kiko wazi Sana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kuuza mboga chini kwenye mavumbi, matope na sehemu isiyokuwa na vyoo sio uhalifu kwa binadamu? Kuwasha moto barabarani kunakopita watu na msongamano wa watu na magari kukaanga chips na mihogo sio uhalifu kwa binadamu wengine, kufanyabiashara bila kulipa kodi wala kusajiliwa sio uhalifu?
 
Cha msingi hapo piga kelele waliopokonywa na kuchomewa nyavu zao warejeshewe au wapewe nyingine au wapewe fedha za kujikimu na serikali, na wale waliofungiwa mialo yao wapewe naeneo mengine ya kuvua, wafugaji wapewe maeneo ya kuchungia, wenye magobore wapewe bunduki nyingine za kulindia mali zao kama unavyofanya kwa wamachinga. Maana wote ni wakosaji kwa mujibu wa kanuni na taratibu na wote hawa walikuwa wanatafuta riziki kutokana na hali zao mbaya.

Walikuwa wahalifu, napiga kelele za kubadili Katiba au?
 
Back
Top Bottom