Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Salaam wakuu,
Siku mbili baada ya Rais John Magufuli kupokea ripoti ya Kamati ya Prof.Abdulkarim Mruma, iliyochunguza mchanga wa dhahabu unaosafirishwa nje ya nchi, Katibu wa NEC Humphrey Polepole alitoa kauli ya kustaajabisha.
Alisema, nanukuu, "kuna watu walitaka kumhonga rais(John Magufuli), kiasi cha Sh. 300 bilioni, ili kusitisha uchunguzi. Lakini rais akawatolea nje. Akasema, 'subirini uchunguzi ukamilike'".
Maneno yake yanawasha masikio ikiwa utayatafakari kwa kina.
Ikiwa rais alitaka kuhongwa na wafanyabiashara wa madini, ni vema na haki tuelezwe ni kina nani walitaka kumhonga, je TAKUKURU wana taarifa? Hii ni kwa sababu tuhuma hizi ni nzito na zinahusisha Mkuu wa Nchi. Zikiachwa hivi hivi reputation ya Rais wa Tanzania itashuka sana.Mtu au watu wenye kuthubutu kumhonga rais ni watu wa hatari, wana uwezo wa kumhonga yeyote seuze rais.
Kwa nafasi yake, huwezi kumwona rais bila appointment. Nani walifanikisha mpango huo wa kihuni? Lazima wasaidizi wa Ikulu wanalijua hili. Wamehojiwa? Wamesimamishwa kazi kwa kumkutanisha rais na genge la wahuni? Kama rais anaweza kukutana na yeyote basi maisha yake yapo hatarini. TISS wana jukumu la kufuatilia jambo hili kwa mapana.
Jambo jingine la msingi ni kuhoji kuhusu majukumu ya Polepole. Je, miongoni mwa majukumu yake ni uofisa mawasiliano wa Ikulu? Nani alimkasimisha madaraka na lini?
Sasa uchunguzi umekamilika,je wahongaji wana ruhusa ya kuhonga.?Kumbuka kwa mujibu wa Polepole,rais aliwaambia wasubiri uchunguzi ukamilike.
Ieleweke kuwa hakuna mtu anayepinga rais kufuatilia uvunaji wa rasilimali zetu.Tunamuunga mkono rais kwa kuwa ndilo tulilolisubiri kwa muda mrefu.Maneno mengine ya Polepole yanaashiria kuwa kuna watu wanapinga juhudi za rais anaposema..."Huu si wakati wa kutofautiana,ni wakati wa kusimama kumshinda adui."
Sote tunajua adui namba moja wa mikataba ya madini iliyotufikisha hapa ni watendaji tuliowaamini na kuwapa dhamana,wakaandika mikataba kwa siri.Hii inajumuisha wabunge wetu wa CCM wanaounga mkono mikataba tata na kushabikia wenzao wanaopinga kufukuzwa Bungeni(Zito Kabwe na Buzwagi mwaka 2007)
Tujadili.