VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Nakuandikia Katibu wangu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Ndugu Humphrey Polepole. Kwanza nakupongeza kwa wazo lako ambalo limeitetea hata Jamiiforums. Utakumbuka tulijadiliana vya kutosha namna ya kujiimarisha kwenye mitandao kama JF, Facebook, Twitter, WatsApp na hata Instagram.
Tulijadiliana, kama kikosi kazi cha kichama, kujiimarisha kwenye mitandao katika kuanzisha au kujibu hoja za kisiasa zinazohusu chama chetu cha Mapinduzi. Tulikubaliana kuwa tuunde IDs za kutosha na kutisha mitandaoni na wenye ID hizo wawe wanawezeshwa ili kukitetea chama na kuwasambaratisha wapinzani wetu.
Tulijadiliana na kukubaliana kuwa IDs hizo zitumike kubeba na kutetea Itikadi ya CCM na utekelezaji wa Ilani yetu. Ikawa vizuri ukakubali mapendekezo na kuyafanyia kazi. Vijana wanawezeshwa kwa vocha na hata 'vipesa vya mboga'. Kwa hilo nakupongeza kwakuwa IDs zipo za kutosha na zinajituma. Chama kinatetewa na JF ikabaki badala ya kufungiwa.
Lakini, nakulaumu kwa jambo moja. Vijana 'waliotumwa' kichama mitandaoni hawakupewa Orientation ya kutosha katika kutenda kazi zao. Hawakuambiwa matumizi sahihi ya lugha na namna ya kujenga hoja za haja katika kutetea CCM yetu. Wao wanaandika chochote hata bila ya kutafakari kwa makini. Usimamizi wao unahitajika. Wawekwe sawa.
IDs zote za chama, popote zilipo, ziwe regulated vya kutosha. Lilikuwa ni wazo zuri kuzianzisha na zinasaidia kujibu mashambulizi na kuwasambaratisha watani zetu. IDs zisiachwe zifanye zitakavyo kwakuwa zitaishia kuaibisha CCM yetu na malengo kupata mapengo.
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam