Polepole na Jerry Muro wamkimbia Mgombea wa CCM jimbo la Siha kisa hali mbaya ya kisiasa waliokutana nayo

Yote yanaweza yakawa na ukweli ila hilo la kukopa chipsi mayai umetia chumvi
 
DR MOLELI ATAMANI KUJITOA UBUNGE JIMBO LA SIHA

Mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Dr Godwin Molel amesema anatamani kujitoa katika kinyang'anyiro cha ubunge katika jimbo la Siha kutokana na ushirikiano mdogo anaoupata ndani ya Ccm katika kutafuta kura na mara kadhaa amekuwa akizomewa kwenye majukwaa wakati wa kujinadi na kuomba kura.

Akizungumza katika vikao vya ndani vya mikakati ya ushindi Dr Molel amesema amekuwa akipata wakati mgumu pale anapojaribu kujenga hoja lakini wananchi wanamzomea na kumuita Kahaba wa siasa kutokana na yeye kujiuzulu ubunge alafu anarudi tena kupitia chama kingine kutaka tena ubunge katika Jimbo la Siha (CCM).

Mjumbe mmoja wa timu ya kampeni aliejulikana kwa jina moja la (Jerry) amesema mgombea huyo anatamani kujitoa na kunawakati anaongea mwenyewe kama chizi kutokana na msongo wa mawazo alionao hasa linapokuja swala la uchaguzi.

Mara kadhaa mwenyekiti wa chama hicho Mh Magufuli Pombe ambae amesema chama kimetumia gharama kubwa sana kuwafanyia uhamisho hivyo ahakikishe pesa hizo alizopewa ndio zinatumika kufanya Kampeni, mtoa taarifa wetu anasema jambo hili limezidi kumkatisha tamaa Dr Moleli na kupoteza kabisa matumaini ya kuendelea kufanya kampeni kutokana na ukweli kwamba hakupewa pesa zote kama walivyokubaliana.

"Huwezi amini sasaivi mgombea wetu hana pesa kabisa,jana amekopa chipsi na mayai hana pesa kabisa,hivi Mkuu wa wilaya ameomba wafanya biashara wamchangie hata pesa ya kutengeneza mabango huoni Jimbo zima hakuna bango hata moja la mgombea wetu?? Yani ni shida tupu ndugu yangu, Amesema mtoa taarifa".

Kiongozi mmoja wa Ccm amesema kwakweli mgombea wa CHADEMA ELVIS MOSI anakubalika sana mtulivu na anaonekana anayajua matatizo ya wananchi wa Siha hili limekuwa kikwazo kikubwa sana kwa chama chetu kwasababu hatukutarajia kama CHADEMA wangesimamisha mgombea katika jimbo hili,na kama tungelijua hili naamini mwenyekiti angeruhusu chama kifanye kura za maoni ili kuona ni nani anakubalika katika jimbo hili kuliko matatizo haya tunayokutana nayo huko kwa wanachi Dr Moleli hauziki na amekuwa mzigo kwetu hapa tupo tu kwaajili ya chama tusijekuonekana wasaliti.

Naye kiongozi Mkuu wa kabila la wamasai katika eneo la mitimirefu,jina tunalihifadhi amesema kitendo alichofinya Dr Moleli ni aibu kubwa kwa kabila la wamasai na inawezekana kabisa kwakuwa alisaliti makubaliano ya mila zao maziwa aliyomwagiwa na wazee wa mila yakampalia na anaweza kuugua ukichaa kabisa akileta utani na mila, na asitegemee kabisa kupata kura za wamasai sisi hatuko tayari na kuwa sehemu ya laana yake.

Kwakweli Dr anajutia sana,alishazoea maisha ya ubunge sasa zimebaki siku chache sana anarudi kuwa mwananchi wa kawaida kama sisi, na kilichomshtua zaidi ni Mh Pole pole na Jerry Muro kukimbia kimyakimya bila kumuaga baada ya kupata taarifa mbaya sana kutoka kwa wananchi wa Siha,( alieleza mtoa taarifa).

Nikiripoti kutoka Jimbo la Siha.

Mwakilishi

Mwanahabari Huru

Siha Kilimanjaro
Hata kama wananchi wa Siha ni mbumbumbu lakini sio kwa kiasi hiki, yaani mgombea yule yule waliyemchagua 2015 kupitia ukawa wamchague tena huyohuyo kupitia CCM. Yaani awatie tena hasara ya pesa ya kurudia uchaguzi na muda wa kumpigia kampeni na kupiga kura!!! labda angewekwa mwingine agombee
 
tukiwa pacha chakubanga atakuwa nani?
Achana naye huyo amekalia ufahamu wake.

Endelea kutupa habari huku Kinondoni tunajaandaa kumuapisha Salim Mwalimu..,hatuwezi kumpa kura mtu ambaye ameachia Ubunge kwa ridhaa yake.

Yani uache Ubunge mwenyewe alafu urudi tena uombe huohuo Ubunge sio Watz wa Leo...!!!

Mtulia na Molleli waanze kuandaa mashamba msimu kilimo unakaribia kuanza.
 
Ndio propaganda za chadema zilipofikia, lowest.
Eti anakopa chips mayai.
Bure kabisa
 
.......Mara kadhaa mwenyekiti wa chama hicho Mh Magufuli Pombe ambae amesema chama kimetumia gharama kubwa sana kuwafanyia uhamisho hivyo ahakikishe pesa hizo alizopewa ndio zinatumika kufanya Kampeni, mtoa taarifa wetu anasema jambo hili limezidi kumkatisha tamaa Dr Moleli na kupoteza kabisa matumaini ya kuendelea kufanya kampeni kutokana na ukweli kwamba hakupewa pesa zote kama walivyokubaliana........

Jamani hili ni la kweli? kama ni la kweli , basi tusubiri!
 
Back
Top Bottom