Polepole: Maoni ya Katiba Mpya yafanyiwa majaribio

Jina lenyewe Polepole na mtu pia ni Polepole hata Katiba itakuja Polepole kwa kupitia maoni Polepole
 
idaw post: 19159165 said:
Naona hiyo nafasi ili ikufiti lazima ujitoe ufahamu kidogo, alieondoka na aliyeingia hakuna tofauti.!
Pingeni hoja yake kwa hoja msipinge hoja yake kwa viroja!!
 
Watanzania piganieni tume huru ya uchaguzi..hizi zingne sarakasi tu. Nchi hii mambo yanavyoenda ni mungu ndo anajua tu. Ccm na Magufuli hawaeleweki wanataka nini, nchi priorities km mia Mara kuhamia Dodoma, Mara majipu. Wananchi tunataka maisha mazuri..mnaharibu uchumi mnaleta swaga tunajenga Nchi..unajenga kwa kuharibu uchumi.
Bad enough hata wapinzani hawajui wanapinga nn na wanakosoa nn. Nyie wapinzani mngekaa Uganda sidhani km kuna MTU angekuwa hata mmoja bungeni. Naona baada ya bosi wenu mbowe kutekenywa kwenye biashara amekuwa kimya.
 
Wednesday, January 4, 2017
Polepole : Maoni ya Katiba Mpya yafanyiwa majaribio



polepole.jpg


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole

Kwa ufupi
Akizungumza katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na televisheni ya Channel Ten, Polepole amesema mchakato wa kupata Katiba Mpya ni mgumu kuuendeleza kwa sasa hadi hapo Rais John Magufuli atakapoinyoosha nchi.

By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema Serikali ya chama hicho inayatekeleza maoni yaliyotolewa na wananchi wakati wa mchakato wa Katiba Mpya kwa kuyafanyia majaribio.

Akizungumza katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na televisheni ya Channel Ten, Polepole amesema mchakato wa kupata Katiba Mpya ni mgumu kuuendeleza kwa sasa hadi hapo Rais John Magufuli atakapoinyoosha nchi.

Mchakato wa Katiba Mpya ulizinduliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka 2011 alipounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba na Polepole akiwa mmoja wa wajumbe.

Hata hivyo, mchakato huo uliishia kwenye Bunge Maalumu la Katiba ambalo licha ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa ambayo haijapigiwa kura ya maoni hadi leo, baadhi ya vyama vya upinzani vilijitoa na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).


Chanzo: Mwananchi
Shenzi kabisa huyu, unaweza kutwambia hii nchi imepinda upande gani? Na je atainyoosha kwa kutumia nyundo au mikono?
 
Kwa hakika siamini kama kweli maneno hayo kaongea kaka yangu Polepole. Yaani siamini kabisa.
Ndio yeye Polepole. Aliyekuwa anahanikiza kwa nguvu zooote Katiba ya Warioba. Sasa anaonyesha rangi nyingine iliyokuwa huifahamu.
 
Katiba mpya si ni ili itusaidie kunyoosha nchi... Sasa huyu mtu amekuwa wakushangaza?!? Khaa! Ivi huyu ndiye yule alokuwa tumeni? Mungu amsaidie...doooh! Hekima ni kitu aghalabu kukikuta kwa mwanasiasa!! Leo katiba hainahaja Tena?? Nchi itanyooka lini? Na kigezo kuwa imekwisha nyooka ni kipi?? Tunaendesha nchi kwa fikra za mtu? Jamani nsaidieni ninchi gani rahisi kupata uraia nikamalizie hii miaka Minne? Tiresome
Hahah kajamaa kanaongea kama kamekatika kichwa, hahaha, njaa jamani mmhh
 
Back
Top Bottom