Polepole: Magufuli na Raisi Samia walikuwa na jambo lao

Shhh
Humphrey Polepole wacha kupiga domo
Tundu Lissu, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
 
Licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa msimamo wake kuhusu usimamizi wa rasilimali za Taifa, lakini hilo litatokana na nidhamu na uadilifu wa viongozi wote.

Hayo yameelezwa bungeni leo Ijumaa ya Aprili 9, 2021 na Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Humphrey Polepole, akisisitiza kuwa utawala bora na uwajibikaji kwa kupiga vita rushwa na ufisadi unatakiwa kutekelezwa na viongozi wote ili kumsaidia Rais Samia.

Polepole, ambaye pia ni Katibu wa NEC ya CC, Itikadi na Uenezi, alikuwa akichangia

mjadala wa kupitisha mpango wa tatu wa maendeleo wa kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 - 2025/26.

“Katika utawala bora na uwajibikaji ningeweza kusema wakati wa msiba wa Hayati Magufuli (Dk John) wale watu walikuwa wanalia sio kwamba Rais Magufuli ametangulia mbele ya haki, mimi nasema hapana wale watu walikuwa wanalia kwa sababu Rais Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan walikuwa na jambo lao na wananchi wale na kulia kwao walikuwa wanaonyesha yale waliyo wahaahidi yataendelea hata kama Magufuli hayupo,” amesema Polepole.

Amesema rai yake kwa Serikali, Rais Samia ameonyesha msimamo kwamba, kazi lazima iendelea na usimamizi mzuri wa raslimali za Taifa unatokana na nidhamu ya viongozi wote hivyo wanapaswa kumsaidia.


“Vita dhidi ya rushwa, ufisadi, matumizi mabaya rasilimali za umma, mambo hayo hatutakiwi kurudi nyuma asilani… kinyume na hapo Watanzania wale waliokuwa wanalia watakuwa wanalia kwa baadhi ya viongozi wetu humu muda sio mrefu kwa sababu watasema tumewageuka. “Rai yangu tumsaidie Rais Samia ili ile ndoto waliyotuletea yeye na Mzee Magufuli na tukawaamini, tukawapenda ikatimie chini ya uongozi wake,” amesema Polepole

Pia, amewataka viongozi wasisahau kuzingatia haki za watu hasa wanyonge kwani, hilo ni muhimu kuzingatiwa muda wote.
Pimbi kweli huyo
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom