James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana kampeni za uchaguzi huu na mmoja wa watu wanaoshiriki sana kwenye kampeni ni Humphrey Polepole.
Mimi si mwanachama wa CCM lakini nadiriki kusema Polepole ni mkomavu kwenye mambo ya siasa na ni hazina kwa chama chake cha CCM.
Ila kuna kitu kimoja kinanichefua kwenye kampeni zake: kuwatukana na kuwakejeli viongozi wenzake wa vyama vya upinzani. Huko nyuma aliwahi kumtukana Godbless Lema kwa kusema eti kuna mambo mengine yaliyomtokea jela hakuyahadithia. Polepole una bahati sana, yaani uniambie mimi maneno hayo wakati ule nipo kijana lazima zipigwe tu!
Sasa kama hiyo haitoshi, jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari alimwita mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe kuwa ni mlevi.
Kwenye upande mwingine, Tundu Lissu hajawahi kumtukana mtu kwenye kampeni zake zaidi ya kukosoa sera za CCM na mapungufu ya Magufuli kwenye utendaji wake serikalini.