Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Hii picha inasambazwa na katibu wa NEC itikadi na Uenezi ndugu Humphrey polepole akidai Katibu Mkuu wa CCM akiongoza kikao cha Makatibu wakuu wa vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika huko Angola, sina tatizo na post yake ila kuna maswali kadhaa hapa:
(1.) Kama ni vyama vya ukombozi hao Wachina ni chama gani kutoka eneo hili Kusini mwa Afrika
(2.) Vyama vya ukombozi vilivyopo madarakani mpaka sasa ni ANC-Afrika kusini, SWAPO-Namibia, MPLA-Angola, FRELIMO-Msumbiji, CCM-Tanzania, hao Makatibu wakuu wa hivi vyama wako wapi.
(3.) Katibu Mkuu wa ANC Comrade Gwede Mantashe hayuko Angola yeye wala mwakilishi wake.
Kama kweli Kinana ameenda huko Angola km Katibu Mkuu wa chama tawala mbona hakuna press release kuhusu ziara hiyo kubwa, Wakati “alipotumwa India kutibiwa”(Propaganda) taarifa ilitoka.
Nadhani Ndugu Polepole inafaa awe makini anapofanya upotoshaji, huyu Kinana kama amejiuzulu tangazeni kuliko kumsingizia mara yuko India, mara yuko Angola huku mnajua yuko “under house arrest” Kinana hastahili hayo kwa kazi aliyoifanyia CCM tangu akiwa Kampeni meneja wa wagombea Urais mwaka 1995-2010 na baadaye Katibu mkuu makini sanjali na kijana wake makini Nape Moses Nnauye walioitoa “CCM shimoni”-In Nape’s Voice
By the way hakuna anayepuuza hili, Abdulrahman Kinana ni mmoja wa wataalam wachache wa mikakati ya kisiasa(Political strategist) binafsi namkubali kwa weledi wake katika mkakati, Ndugu Polepole jipange.