Polepole jikite katika kuimarisha rasilimali watu ndani ya CCM. Hao wahamiaji watatuletea anguko huko mbele

CCM ni kubwa sana kuweza kuangushwa na binadamu xyz anayehama chama chake ni kujiunga, waache waje, hawawezi kuiangusha CCM, CCM is too big!
 
Huu mkakati wa kununua wapinzani umeitambulisha CCM hasisi. CCM iliyo tayari hata kutoa rushwa kwa ajili ya kuwadanganya wananchi kuwa inakubalika. CCM inayoweza kuvunja katiba ya chama chao wenyewe ili kuwasukumiza wahamiaji haramu kwenye uongozi bila ridhaa ya wanachama. CCM inayobebwa na polisi na tume ya uchaguzi. CCM iliyochoka na kukataliwa na wapigakura (kwa kunukuu kauli ya katibu mkuu wa CCM). CCM inayotawaliwa na kikundi kidogo kisichokuwa na mbinu za kufanya siasa, kinachoamini kuwa siasa za kuua upinzani ndio zitaifufua CCM (CCM haitafufuka kwa kuua Chadema).

CCM ilitakiwa ijionyeshe kama chama kinachoweza kusimama upande wa wananchi kwa kuwaletea 1. Demokrasia ya kweli, 2. Maendeleo shirikiri (inclusive), 3. Mifumo iliyo imara ya kujipatia haki, fursa na uhuru kamili, 4. Uwezo wa kuwawajibisha wale wanaohatarisha hiyo misingi ya taifa.

Wasichokijua CCM ni kuwa hata wakiamua kuvifuta kabisa kisheria vyama vya upinzani, bado hawatakubalika. Kutokukubalika kwa CCM ni kutokana na MATENDO yao. Wanasema maneno matamu yasiyokuwa na uhalisia, ila fikra zao zimejaa rushwa, upendeleo, ukandamizaji, ujinga, ushamba, ufisadi, nk. MATENDO ya CCM ndio kikwazo.
 
Mtu aliyekula nyama ya mtu hawezi kuacha ataendelea tu by mwalimu Nyerere ( Mwenyeheri).

Mfano mdogo ni yule Waitara alihama CCM kwa kisingizio cha kumkimbia Nchimbi na sasa kahama CCM kwa kisingizio cha kumkimbia Mbowe.

What next!! Niishie hapo.
Roho zimeanza kuwauma baada ya kuambulia fulana tu huku wenzenu wakilamba vyeo , na bado kudadeki !
 
Mtu aliyekula nyama ya mtu hawezi kuacha ataendelea tu by mwalimu Nyerere ( Mwenyeheri).

Mfano mdogo ni yule Waitara alihama CCM kwa kisingizio cha kumkimbia Nchimbi na sasa kahama CCM kwa kisingizio cha kumkimbia Mbowe.

What next!! Niishie hapo.
Kupiga kura panapokua na mabishano ni agizo la Kimungu kwenye vitabu vya dini.

Ni sawa na agizo la Kimungu kuzitii mamlaka zilizopo .

Watawala wanapodharau agizo la Mungu la kupiga kura kwa haki kwenye mabishano ya watu zaidi ya mmoja ili apatikane anayefaa ujue dharau hiyo haitaishia nje ya Chama bali ikishazoeleka nje itarudi ndani kwa hiyo patakua hakuna nguvu ya kura bali kura ya nguvu. Wenye mamlaka watamuweka wanayemtaka bila kujali katokea wapi na kaja lini!!

Swali la kujiuliza ni je, ni kwa nini watawala hawataki kuona kuwa kuvunja moja ya maagizo hayo ya Kimaandiko ya utii kwa mamlaka na kupiga kura ili kuondoa ubishani ni jambo la kumuasi Mungu na litaleta adhabu na mahangaiko kwa taifa zima kuanzia kwenye vyama vya siasa??
 
Tatizo lenu kubwa ni unafiki.. Kama hampendezwi na jambo mnalisema kwa kutumia katiba ya chama chenu.. Sio peke yako, karibia asilimia 80 ya wanasisiemu hawapendezwi manunuzi haya yanayoendelea.. Wengi wangependa kuona jitihada katika uboreshaji wa maisha ya Watanzania.. Mmempa Mwenyekiti madaraka makubwa mpaka amekihodhi chama.. Anachotaka yeye ndicho kifanyikacho, hutaki unatimuliwa..
 
Mtu aliyekula nyama ya mtu hawezi kuacha ataendelea tu by mwalimu Nyerere ( Mwenyeheri).

Mfano mdogo ni yule Waitara alihama CCM kwa kisingizio cha kumkimbia Nchimbi na sasa kahama CCM kwa kisingizio cha kumkimbia Mbowe.

What next!! Niishie hapo.
Hilo taifa limejaa ngombe na nguruwe ninyi ni wajinga
 
Back
Top Bottom