Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

Kuwa Amiri Jeshi Mkuu si kuogopwa. Bali ni heshima tu. Mie nadhani hii ya makamu kuwa Rais ili kuondoa sintofahamu. Makamu wa Rais ashike madaraka ya urais kwa kipindi cha miezi kadhaa kuelekea uchaguzi wa Rais. Iwapo Rais atakuwa amefariki...
Afadhali ungesema mambo ya uchaguzi periodic wa Rais yafutwe kabisa tuwe kama China--president for life. Wabunge wapungue hadi 150 tu. Mawaziri wawe 20. Wakuu wa mikoa na wilaya waondoke zao. Makatibu wakuu wateuliwe kwa sifa za uzoefu wa kazi na taaluma.
 
Mama SSH ni Rais wa awamu ya sita.
Awamu inaanza pale kiongozi anapokula kiapo cha kuwa Rais wa nchi.
Hata Katibu Mwenezi mstaafu anajua hivyo,lakini anajitoa ufahamu au ndiyo zile kampeni zao za kutaka Mama SSH asigombee urais 2025 kwa kigezo kuwa yeye alikuwa anaongoza awamu ya tano.
Mama SSH ni Rais wa awamu sita kipindi Cha kwanza.
Mfano ni Zanzibar,Dr Hussein Hassan Mwinyi ni Rais wa awamu ya nane
akitanguliwa na
1).Mzee Abeid Amani Karume,
2).Aboud Jumbe,
3).Ali Hassan Mwinyi,
4) Abdul Wakil,
5) Dr Salmin Amour
6).,Aman Abeid Karume
7) Dr Ali Mohamed Shein na
8) Dr Hussein Ali Hassan Mwinyi
Polepole aache kupotosha wananchi, wakati wa awamu ya kwanza Tanzania tumefanya chaguzi chini ya chama kimoja Cha siasa mwaka 1965,1970,1975,1980,1985, 1990
-TANU/CCM walikuwa wanaandaa election manifest (Ilani ya Uchaguzi) ambayo chama na wabunge walikuwa wanainadi,
mgombea Urais alikuwa mmoja na wananchi walikuwa wanapiga kukubali au kukataa (Ndiyo/Hapana).
Ukichagua Ndiyo maana yake ndiyo yeye,ukichagua Hapana maana Hapana mwingine.
-Hoja ya kusema awamu ni kutawala miaka kumi haina mashiko.
Ushauri;
-Ni vema na busara Mama SSH aachwe apange Safu au timu yake ya kufanya nayo kazi ya kuwatumikia wananchi.
wale ambao wako bench au jukwaani/ kando kubali matokeo na subiri mpaka 2030 au wakati wa kipindi cha pili unaweza kuingia mchezoni
 
Chikuvi2021.

Awamu ya sita imechaguliwa na nani, sera zake ni zipi, ilani yake ni ipi, maono yake ni yapi, kazi iendelea inamaanisha nini, kazi gani iendelee?

Strategy ni hii, tunatukana kila alichofanya JPM, ingawa tulikuwa wasaidizi wake wakuu. Kila kizuri tulishiriki, vibaya hatuwepo.

Elimu watoto milioni kumi kwenda shule serikali ya sasa inakwambia sio kitu, Maji, Umeme wa uhakika wanatafuta sababu za kijinga.

Afya, barabara, sheria za madini rasilimiali, kuliokoa taifa kwenye janga la Covid -19, Corona kwa kuhimiza kuchukua tahadhari, barakoa, kunawa mikono, lakini hakutakuwa na Lockdown wanakwambia wote ujinga.

Nidhamu serikalini imeshuka,Ufisadi, rushwa, madawa ya kulevya, ukiritimba umerudi kwa nguvu, familia chache kuitawala Tanzania labda ndio tunamaanisha awamu ya sita.

Janga la Corona bila serikali makini Wananchi wangeuliwa na polisi (mfano ni Kenya) wakionekana mtaani, wengi wangekufa na njaa, familia nyingi zingevunjika. Watoto kukosa elimu (Uganda).

Polepole anajaribu kuwakumbusha mlikuwa pamoja, mkachaguliwa kwa mgongo wa JPM 2015. Mmemzima labda mipango yenu baadaye ni kumuua. Visasi. Gwajima kumfunga mdomo kisa msimamo wake.

Ushauri Fanya kazi zaidi ya Magufuli utapendwa, Fanya Umeme, maji, huduma serikalini zipatikane kwa Watanzania.

Bei za pembejeo, mbolea, mafuta, petrol, diesel, vifaa vya ujenzi viwe rafiki. Punguza mfumuko wa bei.

Tengezeza ajira, sio kwa washikaji wachache kama wewe Chikuvi2021, wahuni ndugu zako. Futa kesi ya Mbowe.

Utapendwa zaidi.
 
Huyu ni kiongozi aliyepikwa na kupikika chini ya uongozi imara na madhubuti wa JPM. Haihitaji akili nyingi kugundua kuwa serikali iliyopo ni dhaifu na imepoteza mwelekeo. ukiwa kama kiongozi uliyepikwa na kupikika chini ya JPM hauwezi kukaa kimya
 
Kuwa Amiri Jeshi Mkuu si kuogopwa. Bali ni heshima tu. Mie nadhani hii ya makamu kuwa Rais ili kuondoa sintofahamu. Makamu wa Rais ashike madaraka ya urais kwa kipindi cha miezi kadhaa kuelekea uchaguzi wa Rais. Iwapo Rais atakuwa amefariki...
Umeenda deep sana.

Nimewaza ingetokea awamu ya Nne kipindi cha 2 kama ilivyotokea march 2021 Yule makamu angeshika kijiti? Hatakuongea tu ilikuwa shida.

Angeshinda Lisu 2020 then ingetokea kama march Salum Mwalimu angekamata madaraka.

NB!
Nafasi ya Makamu was Rais,

Spika,

Jaji mkuu inapaswa itafutwe njia sahihi yakuwapata.Siyo kwa kupendekezwa na mtu mmoja kwa mahaba yake tu.
 
Umeenda deep sana.
Nimewaza ingetokea awamu ya Nne kipindi cha 2 kama ilivyotokea march 2021 Yule makamu angeshika kijiti? Hatakuongea tu ilikuwa shida...

Katiba mpya ndio jibu, ikishindikana hata kuboresha katiba hii tuliyonayo.

Makamu wa Rais anaogopa kukaimu nchi hata, hata kwa wiki moja tu.

Rais badala ya kutatua kero, matatizo ya nchi, anayumba, mara kugombea 2025, mara haki za wanawake, kushughulika na Polepole, Gwajima, minor issue.

Sasa hapa tuna Viongozi?
 
Huyu ni kiongozi aliyepikwa na kupikika chini ya uongozi imara na madhubuti wa JPM. Haihitaji akili nyingi kugundua kuwa serikali iliyopo ni dhaifu na imepoteza mwelekeo. ukiwa kama kiongozi uliyepikwa na kupikika chini ya JPM hauwezi kukaa kimya
Exactly polepole anachopigania anakijuwa na amekuwa mwiba kwao Memba alijaribu kumtaja taja alimpa jibu moja tu kapotelea porini bulembo tangu ajibiwe mpaka leo kimya tusimdharau polepole anajuwa mambo mengi ya watu wabaya na wazuri anawajuwa ndo maana anapata mapingamiza mengi sna lakini tunaompinga wengi wetu tuna mahaba na viongozi fulani ila ukweli hatuujuwi
 
Katika SHULE ya Uongozi ya Humphrey Polepole kuna Siku alisema Watu wanapoteshwa kuambiwa hii ni AWAMU ya 6
Leo ndio nimeamini hii ni AWAMU 5 kwa sababu Hata ILANI inayotumika ni ya Awamu ya 5 Waliyoinadi Hayati MAGUFULI kama RAIS na Mama SAMIA kama Makamu wa RAIS AWAMU ni Miaka 10 (Vipindi 2 vya Miaka 5) Hivyo RAIS Samia ATAITIMISHA Utawala wa AWAMU ya 5 Wa MIAKA 10 ifikapo 2025 ili Kupisha UCHAGUZI MKUU wa Kumpata RAIS wa AWAMU ya 6 Na ILANI YAKE.

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Shida mama hatak isomeke awam ya tano sababu ikisomeka ivyo itampasa 2025 kuingia ulingon na wana ccm wenzake kugombea nafasi ya uraisi wakat ye anataka 2025 kusowepo na uchaguzi ndani ya ccm
 
Katika SHULE ya Uongozi ya Humphrey Polepole kuna Siku alisema Watu wanapoteshwa kuambiwa hii ni AWAMU ya 6
Leo ndio nimeamini hii ni AWAMU 5 kwa sababu Hata ILANI inayotumika ni ya Awamu ya 5 Waliyoinadi Hayati MAGUFULI kama RAIS na Mama SAMIA kama Makamu wa RAIS AWAMU ni Miaka 10 (Vipindi 2 vya Miaka 5) Hivyo RAIS Samia ATAITIMISHA Utawala wa AWAMU ya 5 Wa MIAKA 10 ifikapo 2025 ili Kupisha UCHAGUZI MKUU wa Kumpata RAIS wa AWAMU ya 6 Na ILANI YAKE.

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
Mwalimu Polepole
JamiiForums1655508168.jpg


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Wadau naomba kumpatia UFAFANUZI juu ya Utawala uliopo ni wa AWAMU ya NGAPI? Wapo wanaosema ni Wa AWAMU ya 5 Na Hoja yao ni Mwendelezo wa Awamu ya 5 na Kwamba ILANI ni ile ile ya Awamu ya 5 na Uchaguzi ni ule ule wa 2015 na 2020 Ila Wale wanaosema Awamu ya 6 sijasikia.

HOJA zao.
Naomba tujulishwe hii ni AWAMU ya 5 Au ya 6?
 
Back
Top Bottom