Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

Polepole anatakiwa kujua Samia ni Amiri Jeshi Mkuu!

Anaesema hii ni awamu ya Sita ni Rais Samia Mwenyewe! Sasa kama anapinga hii sio awamu ya Sita ajue anapingana na Rais Samia mwenyewe!

Kifupi anatakiwa ajue sonono aliyokuwa nayo juu ya Rais Samia sasa itaenda kumuonesha kuwa Samia ni Rais Kweli na Amiri Jeshi Mkuu
Acha kumtisha, wako wapi waliokuwa na nguvu zaidi ya yeye. Wamekufa kifo kibaya. Hata awe na ulinzi kiasi gani Mungu akitaka roho yake sekunde tu.
 
Wewe umeona una akili hapo? Kama zimeanza kutumika wakati wa mwinyi mnaitaje ya magufuli ni awamu ya tano badala ya nne?. Awamu zinatajwa kwa kila Rais akipita au kafa na awamu imepita. Ndiyo maana hii inaitwa ya sita kuanzia nyerere mpaka samia
Kuita hii Ni awamu ya sita Ni uzuzu, Ni rais wa sita lakini awamu ya tano
 
Mkuu miongozo haimtaji mtu kuwa awamu, inataja uchaguzi kuwa awamu, kwa hyo kinachozaa awamu Ni uchaguzi, kwa Sasa tupo awamu ya 5 Ila tuna rais wa 6,

Nyogeza tu kidg, baada ya nyerere aliekaa madarakani miaka 20+ Toka mwaka 1985- Sasa tuna awamu za vipindi vya miaka 5, na kwa rais miaka 10, kwa hyo ingetokea tumefanya uchaguzi, Basi rais angekuwa ktk awam ya 6 Ila kwa Sasa Ni awamu 5 ya kazi iendeleee, Kama unabisha, njoo unipige@drmsukuma

Huwezi kumwajibisha Samia Kwa mambo ya Magu, hata Kama alikuwa makam
 
Kwani awamu ni nini?

Ulikwishawahi kusikia:

1) Awamu ya Mwalimu Nyerere

Au

2) Awamu ya kwanza, ya Mwalimu Nyerere?

Unaelewa nini?
Hukuwahi kusikia wimbo wa John Komba (RIP) akizitaja hizo awamu?
Unadhani wanaposema awamu ya kwanza wanamaanisha nini?
 
Wakuu,

Mbunge wa kuteuliwa na mtunga Sheria Humphrey Polepole, anadai hii awamu ya rais Samia sio awamu ya sita.

Rais Samia alisema yeye ndiye rais ya awamu ya Sita. Kwamba ni awamu ya sita kipindi cha kwanza.

"Hii serikali sio mpya,haikupigiwa kura, huwezi ukaita awamu ya sita, awamu lazima iwe na miaka10, ilani na Sera zinazopaswa kutekelezwa ni zile tulizozinadi 2020, asiwadanganye mtu kuwa hii ni awamu ya sita,Kwa sababu aliyeondoka ni Magufuli peke yake" kasema polepole.

RAIS SAMIA ANASEMA UFISADI ULIFANYIKA AWAMU ZILIZOPITA SIO AWAMU YAKE YA SITA
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali, na yanageuka kusema serikali ya awamu ya 6 ufisadi umerudi mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo, mambo hayo yalifanyika huko nyuma, gari bovu linaangushiwa awamu ya 6 sitakubali"
Rais Samia Suluhu akiwa Bandarini.

Je, nani yupo sahihi na Sheria inasemaje?

View attachment 2041066
Katika utawala wa CCM anachosema Rais ndicho kinachokuwa. Ndio sheria. Polepole anajua vizuri sana. Mfano alishuhudia wabunge wa viti maalum wa CHADEMA wakiingizwa bungeni kinyume cha katiba hakuona tabu. Asijifanye hajui chama chake kinavyoongoza nchi.
 
Wewe umeona una akili hapo? Kama zimeanza kutumika wakati wa mwinyi mnaitaje ya magufuli ni awamu ya tano badala ya nne?. Awamu zinatajwa kwa kila Rais akipita au kafa na awamu imepita. Ndiyo maana hii inaitwa ya sita kuanzia nyerere mpaka samia
👍👍
 
Amuulize Mbunge wetu wa Kawe!
Polepole anatakiwa kujua Samia ni Amiri Jeshi Mkuu!

Anaesema hii ni awamu ya Sita ni Rais Samia Mwenyewe! Sasa kama anapinga hii sio awamu ya Sita ajue anapingana na Rais Samia mwenyewe!

Kifupi anatakiwa ajue sonono aliyokuwa nayo juu ya Rais Samia sasa itaenda kumuonesha kuwa Samia ni Rais Kweli na Amiri Jeshi Mkuu
 
Toa huyo wa Mwisho
Hata ikiwa ni awamu ya kumi hiyo itatusaidia nini sisi?
Kwangu mimi awamu maana yake ni kipindi cha mtawala akiwa madarakani, na hapa Tz mtawala ni rais.
Rais=awamu
Nyerere (awamu ya kwanza)
Mwinyi (awamu ya pili)
Mkapa (awamu ya tatu)
Kikwete (awamu ya nne)
Magufuli (awamu ya tano)
Samia (awamu ya Sita)
Chakubanga (awamu ya saba?!)
 
KWA UELEWA WANGU MIMI NADHANI AWAMU ZINAHESABIKA KWA KUANGALIA IDADI YA MARAIS, KWAMBA RAIS TULIYENAYE NI WA NGAPI TANGU TUMEPATA UHURU. HATUHESABU AWAMU KWA KUTUMIA MAFUNGU YA MIAKA KUMI KUMI, MAANA TUKIFANYA HIVYO HUKO MVELE YA SAFARI BAADA YA MIAKA MINGI LAZIMA TUTACHANGANYA MADESA. NAOMBA MH POLEPOLE ASHAURIWE NA AKUBALIANE NA FACT KWAMBA AWAMU TULIYONAYO NI YA SITA, NA KWAMBA ANATAKIWA AZIDI KUMUOMBEA MAMA, MAMA AZIDI KWENDA KWA KISHINDO KIKUU AKIWA AMEAMBATANA NA BWANA, MITHILI YA BWANA ALIVYOWAHI KWENDA NA WALE WATU WANNE WALIOWAHI KUSABABISHA MAJESHI YA WASHAMI KUIKIMBIA KAMBI YAKE HUKU NYUMA YAKIACHA CHAKULA TELE WAKATI WA NJAA KALI. MUNGU AZIDI KWENDA NA.MAMA KWA KISHINDO KIKUU CHA AINA HIYO, NAMUOMBEA KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYE HAI!
 
Ni ya 6 Kwa sababu rais hakuwa Samia; maamuzi alikuwa anafanya mwingine; Samia hausiki kabisa Na Makosa ya awamu ya 5
Hahusiki kivipi akati alikua second in command na kwenye karatasi ya kura tulimchagua? Yeye ndo alipaswa ahusike, kama si yeye basi nani?
 
Mh Polepole yuko sahihi sana ila kwa sababu UNAFIKI UMETAMALAKI KWENYE TAIFA HILI HATA UKWELI UKIBADILISHWA KUWA UONGO WATU WANAONA SAWA TU.

INASIKITISHA MNO
 
Shukuruni mama Samia kasema hii ni awamu ya sita. Angeweza kuiita ya tano kisha baadaye akagombea ya sita 2025 hadi 2035. Ni kiasi cha kuweka sawa nyenzo zake ndani ya chama na dola. Kanuni zinarekebishwa tu.

Jiwe alishaonyesha njia jinsi ya kuitengeneza serikali na chama kama unavyotaka na Watanzania wasikohoe.
 
Back
Top Bottom