Polepole: Hata Mungu hakutaka upinzani ndiyo maana alimfukuza shetani mbinguni

Polepole amewataka wapinzani waache kupiga kelele kuhusu kubanwa kwa vyama vya siasa.

Amewaambia kwani hata mungu alimfukuza shetani mbinguni kwani alikuwa hataki upinzani.

Kazi kwenu

Huyo ni mpuuzi kila mwenye akili timamu ameshampuuza.
 
Hamna anaetaka upinzani Hilo lina ukweli hata Mimi mwanangu hawezi GEUKA kichwa nyumbani kwangu Ntamtimua tu...Japo ndio inategemea huyu mtoto anataka kunipindua mimi niwe mtoto yeye awe baba au VIPI? tutasikilizana kwanza nikigundua ni hivyo sitomuelewa.

Upinzani TZ hamna na hautotokea Tunadanganyana tu

Kwa anayetumia kijambio kufikiri atafikiri hivyo.
 
Kama Polepole kayasema hayo kweli inabidi ajitafakari uwezo wake kiakili.

Kuiweka CCM kwenye mizani moja na MUNGU MUUMBA VYOTE, hakika ni kumkufuru MUNGU.

1. MUNGU hakosei, je Ccm ina makosa mangapi?

2. MUNGU ni mkamilifu, je Ccm ina ukamilifu gani?

3. MUNGU ni mpenda haki, je, Ccm inapenda haki?

4. MUNGU alimuumba shetani, je, Ccm ilimuumba Mbowe ama Lissu am Zitto ama Maalimu ama iliumba nini hasa?

5. MUNGU hadanganyi, hadhulumu, haonei, hana chuki, je, Ccm ikoje?
Bottom line ni kuwa Mungu hafananishwi na kitu chochote. Kumfananisha na kitu chochote ni upumbavu na kama kweli Polepole kasema haya ni lazima atubu, hakina namna!
 
Mwambieni Pole Polena Viunga vyake wakakasome Ayubu Sura ya Kwanza.Bwana Mungu anapiga Story sana na Shetani na hata kuna muda anampa nafasi Shetani tena ya kufanya mambo makubwa tu.Sio wao Umungu wao ni wa wapi?Wao hata kuongelshwa hawataki..tena kuna Bwana mkubwa wao alidai akifa ataomba Mungu ampe Nafasi ya Kutawala kule Mbinguni.

''7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.

8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.

9 Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure?

10 Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.

11 Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.

12 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.''
 
Polepole amewataka wapinzani waache kupiga kelele kuhusu kubanwa kwa vyama vya siasa.

Amewaambia kwani hata mungu alimfukuza shetani mbinguni kwani alikuwa hataki upinzani.

Kazi kwenu
Ndo maana nao wameamua kuwafukuza wapinzani duniani! Sasa nimeelewa maana ya hizi pyupyu.
 
Mkuu unajua nashangaa sana,

Ccm inajua kila baada ya miaka mitano kuna uchaguzi, na kama ikitokea Chama Cha Upinzani kikashinda inabidi Ccm ikabidhi madaraka kwa Upinzani.

Je, kwa Mungu kuna uchaguzi?

Je, kuna wakati Mungu ataachia Mamlaka yake na awe na cheo tofauti na Mungu?

Sijui kwanini wengine wakipata madaraka wanajikweza kiasi cha kukufuru!!!

Si alisema anataka akawe kiongozi wa malaika?
 
Watu wengine wanasikitisha sana,wanaabudu kwa mungu halafu wanajifanya wanaabudu kwa Mungu.Na ndiyo maana wanasoma maandiko ya Mungu kama wanavyosoma magazeti ya wana Lumumba.Ni vema mkabaki na mungu wenu mnayemwabudu kuliko kumtania Mungu wetu aliye hai.Plato aliposema kuwa mtu aishie pasipo reasoning ni sawa na mfu sijuwi alifikiria nini!Heri kufa ukiwa umeacha fikra hai kuliko kuishi ukiwa na fikra zilizokufa.
 
Polepole amewataka wapinzani waache kupiga kelele kuhusu kubanwa kwa vyama vya siasa.

Amewaambia kwani hata mungu alimfukuza shetani mbinguni kwani alikuwa hataki upinzani.

Kazi kwenu
Bangi za kisukuma hizo
 
Kama Polepole kayasema hayo kweli inabidi ajitafakari uwezo wake kiakili.

Kuiweka CCM kwenye mizani moja na MUNGU MUUMBA VYOTE, hakika ni kumkufuru MUNGU.

1. MUNGU hakosei, je Ccm ina makosa mangapi?

2. MUNGU ni mkamilifu, je Ccm ina ukamilifu gani?

3. MUNGU ni mpenda haki, je, Ccm inapenda haki?

4. MUNGU alimuumba shetani, je, Ccm ilimuumba Mbowe ama Lissu am Zitto ama Maalimu ama iliumba nini hasa?

5. MUNGU hadanganyi, hadhulumu, haonei, hana chuki, je, Ccm ikoje?
Sasa kama Mungu alimuumba shetani, alafu akamfukuza, bado tu huoni Mungu alikosea kumuumba. Alafu unasema Mungu hakosei

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Polepole amewataka wapinzani waache kupiga kelele kuhusu kubanwa kwa vyama vya siasa.

Amewaambia kwani hata mungu alimfukuza shetani mbinguni kwani alikuwa hataki upinzani.

Kazi kwenu
Hmmm, amefikia hatua hii?
 
Nilijua tu ipo siku rangi halisi ya huyu ZUZU itajulikana. Wao ni Mungu na Wapinzani ni Shetani? Kufuru gani hii?? Kujilinganisha na Mungu inaruhusiwa dini gani? Hivi Mchungaji wake amemsikia na bado akienda Kanisani hataambiwa kufuru hii? Viongozi wa dini ifike mahali msimamie viapo vyenu katika kulinda neno la Mungu. Haiwezekani MPUMBAVU mmoja kwa sababu ya madaraka aanze kulinganisha utukufu wa mbinguni na chama chenye wanachama binadamu wadhambi na wadhulumaji kama CCM. Ifike mahali msimame kama watetezi halisi wa Mungu na neno lake bila kuhofia limetolewa na Nani! Hawa ni Walevi tu, tena walevi wa muda mfupi, pombe ya madaraka ikiwaisha wanarejea kwenye akili zao, hivyo ni wajibu wenu kukemea pale mambo matakatifu yanapofananishwa na Upumbavu wa wapumbavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alianza baba yake kusema akifa atakuwa zaidi ya Gabriel huko mbinguni!

Kitu kimoja nina hakika nacho. Mungi hafanyiwi masihara!
 
Mtu yeyote aishiye kwakutegemea akili ya mwingine huyo hana tija kwa jamii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom