Najaribu kuangalia tofauti kati ya Katibu Mwenezi wa CCM aliyepo Humphrey Polepole na Katibu Mwenezi aliyepita Nape Nnauye. Inavyoonekana Polepole ameishiwa mbinu au hana kabisa mbinu za ushawishi kwa wananchi.
Polepole alipoteuliwa tu alianza kuwarubuni wapinzani hasa viongozi kwa kuwahonga pesa na vyeo mbinu ambayo ilikuwa haina tija sana kisiasa, tofauti na wenzake waliokuwa wakishinda vijijini kushirikiana na wananchi kwenye ujenzi mbalimbali wa maendeleo, sasa ameanzisha vikundi vya kihalifu vya kujilinda ndani ya kitengo cha vijana vikundi ambavyo ni kinyume na katiba ya vyama vya siasa. Ni dalili ambayo siyo afya kwa chama, ni dalili ya kuanza kujihami, ni dalili ya kuleta vurugu ina viashiria vya uhalifu.
Polepole anaona fahari vikundi hivyo vinapofanya uhalifu na kuvihujumu vyama vingine, anafurahia anaposikia ofisi ya upinzani imechomwa moto, au kiongozi wa upinzani amepigwa risasi, anaona fahari vyama vingine vinaponyimwa vibali vya kufanya mikutano na kuandamana, anapoona anaruhusiwa kuandamana peke yake anatamba kwenye mitandao anafikiri hiyo ndiyo siasa.
Mkiti mstaafu wa CCM JK aliwahi kusema Chama kikitegemea polisi kitashindwa. Napenda kumwambia Polepole kwamba cheo hicho kimekuwa kizito kwake hana mbinu zaidi za kukiongoza chama kikubwa kama hicho bila kuegemea ukuta wa polisi, hakisaidii chama wala Mkiti wake, atafute mbinu za kisiasa kama mwenzake Nape na Kinana walivyokuwa wakifanya bila msaada mkubwa wa jeshi la polisi.