Polepole: CHADEMA wanagawa rushwa Monduli

Kweli naamini ule msemo wa wahenga unao sema "Kunya anye kuku....... akinya bata ameharisha........."
 
Kweli ccm hamna issue. Kuanzia lini Masai anatumia chumvi kwenye misosi yao😅
Bora mngesema sukari. Polepole acha kutoka mapovu.
Kwani si mna uwezo wa kutangaza matokeo wakati wapiga kura bado kwenye foleni ya upigaji kura. Leo imekuwaje tena mnalalama.
NEC watangaze tu ccm imeshinda ili muone matokeo yake. Mnatafuta majanga tu.
Wananchi wa Monduli si wa kuchezea.
Huyo atapata tabu sana.
 
ndio hivyo mkuu , kuna kiongozi mmoja wa idara nyeti amevujisha makubaliano yao kwa Mh Lowassa ndio maana sisi wengine tumeyaona
Wana kazi sana hawa ma ccm kwa huu mchezo wao wa kipuuzi mana majamaa wao wanataka nyadhifa zao tu ktk hayo makubaliano yao na pesa juu.
 
Hivi hawa Vampire Killers washuhudie Chadema wanatoa rushwa halafu walalamike tu bila kuwatumia Gestapo?
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimesikitishwa sana na kitendo cha viongozi wa dini kufanya kampeni za kumnadi mgombea wa CHADEMA, tena kiongozi huyo akatoa lugha chafu dhidi ya mgombea wetu wa CCM.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu mwenezi wa Chama hicho, Hamphrey Polepole wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwendendo wa kampeni kufutia uchaguzi wa marudio wa majimbo na kata .

Amesema kuwa, wao kama chama tawala hawawezi kutumia dini kwenye majukwaa yao maana tunaheshimu sheria inayokataza mambo hayo na chama chao si cha mlengo wa kidini

Aidha ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wawamulike Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Monduli, kwani wanauthibitisho wa chama hicho kugawa rushwa ya chumvi nyumba kwa nyumba.

“Tunawaomba Takukuru wawaangalie Chadema jimbo la Monduli kwani wanatoa rushwa kwa kuwapa watu chunvi nyumba kwa nyumba na kwa bahati mbaya anayeongoza kugawa rushwa hii ni mgombea wao wa mwaka 2015″amesema Polepole

Amesema kuwa, Chadema wamepeleka watu kutoka sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwatisha akina mama ili wasijitokeze kwenda kupiga kura, kwani wamegundua akina mama wameonekana wanaielewa CCM kwa sababu imewaletea mikopo nafuu.

“Chadema wamekua na njama nyingi dhidi ya CCM sasa hivi wameelekea upande wa akina mama kuhakikisha hawapigi kura, hawamchagui kiongozi wanaemtaka, hivyo tunavitaka vyombo vya dola kuthibiti hawa wahuni ” amesema Polepole.

Hata hivyo, amesema anamshauri Lowassa akalee wajukuu, hapendi kumuona anastaafu siasa kwa fedheha, sisi chama cha Mapinduzi tulikuwa tunamsubiri huyu Lowassa ampeleke mtoto wake Fred ili tumyooshe.

“Lowassa alikuwa amejimilikisha jimbo la Monduli, watu wa Monduli hawamilikiwi na mtu na tunakwenda kurudisha heshima ya Komredi Sokoine wilayani Monduli ” amesema Polepole.
Mie nadhani anagawa rushwa ni yule aliyemfanya karanga na mwita wajiuzulu ubunge
 
haijawai tokea duniani popote mtu kuhama chama katika ngazi yake ya ubunge na kuhamia chama kingine na kugombea tena nafasi ile ile ,,,,,,,,,,,hii nin aibu sna
 
Back
Top Bottom