Tetesi: Polepole asema CHADEMA ruksa kutumia Dodoma Convention Centre

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
image.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema kuwa ni ruksa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kutumia ukumbi wao wa mikutano maarufu kama 'Dodoma Convention Centre'.

Kauli hiyo imetolewa na Polepole kufuatia mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe tarehe 14 Mei 2017 juu ya uwezekano wa chama hicho kutumia ukumbi huo. Polepole amemwambia Mbowe kuwa CCM haioni uzito wa kutoa kibali kwa CHADEMA kutumia ukumbi huo ikiwa watawasilisha maombi rasmi kwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.

Hata hivyo, Polepole amemweleza Mbowe kuwa wataruhusiwa tu kuutumia ukumbi huo ikiwa watakubali masharti ya kutoweka alama za chama chao nje ya ukumbi huo isipokuwa sehemu ya ndani.

Tarehe 27 Mei 2017, CHADEMA watafanya Mkutano wa Kamati Kuu Mjini Dodoma na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho Boniface Makene haijabainisha ukumbi watakaotumka. Upo uwezekano kuwa Mbowe ametekeleza masharti aliyopewa na huenda mkutano huo utafanyika ndani ya ukumbi wa CCM.

MYTAKE: Pamoja na Uadui wangu na CHADEMA, nasupport msimamo wa Polepole.
 
Hawa waliwahi kumtegeshea Slaa vinasa sauti akiwa bungeni Dodoma. Kwa chuki zao za kutisha watashindwa kutegesha vinasa sauti ili kuweza kujua nini kinazungumzwa na mikakati ya chama!? NGASTUKA!
Hahahahahaaaaaa. Umewaza kwa sauti kubwa. Mpigie Makene fastaaaaa
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema kuwa ni ruksa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kutumia ukumbi wao wa mikutano maarufu kama 'Dodoma Convention Centre'.

Kauli hiyo imetolewa na Polepole kufuatia mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe tarehe 14 Mei 2017 juu ya uwezekano wa chama hicho kutumia ukumbi huo. Polepole amemwambia Mbowe kuwa CCM haioni uzito wa kutoa kibali kwa CHADEMA kutumia ukumbi huo ikiwa watawasilisha maombi rasmi kwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.

Hata hivyo, Polepole amemweleza Mbowe kuwa wataruhusiwa tu kuutumia ukumbi huo ikiwa watakubali masharti ya kutoweka alama za chama chao nje ya ukumbi huo isipokuwa sehemu ya ndani.

Tarehe 27 Mei 2017, CHADEMA watafanya Mkutano wa Kamati Kuu Mjini Dodoma na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho Boniface Makene haijabainisha ukumbi watakaotumka. Upo uwezekano kuwa Mbowe ametekeleza masharti aliyopewa na huenda mkutano huo utafanyika ndani ya ukumbi wa CCM.

MYTAKE: Pamoja na Uadui wangu na CHADEMA, nasupport msimamo wa Polepole.

Kwa hiyo walikuwa wanawazuia mkutano ili wawakodishie ukumbiwa?au wanataka kurekodi wanayo
Yajadili?hii nchi CCM haitatolewa na chama kitakacho ongozwa na watu wa kilimanjaro,tutaishi kama mrema,mbatia na sasa mbowe,kuvunjika moyo na matumaini hewa.
 
Chanzo cha habari yako ni kipi?
Isije kuwa TBC waliozusha trump amemmwagia sifa bwana yule!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa hiyo walikuwa wanawazuia mkutano ili wawakodishie ukumbiwa?au wanataka kurekodi wanayo
Yajadili?hii nchi CCM haitatolewa na chama kitakacho ongozwa na watu wa kilimanjaro,tutaishi kama mrema,mbatia na sasa mbowe,kuvunjika moyo na matumaini hewa.
Aliyeomba ukumbi huo anajua kwa nini amefanya hivyo
 
Likiwezekana hili la kufanya mkutano litawezekana pia CCM kuwapangisha CHADEMA kwenye jengo lao la Makao Makuu pale Dodoma.
 
Hilo ni jambo jema hasa kwenye nchi ya watu wamoja kama hii. siasa siyo vita wala si uhasama.
 
MACCM si ya kuyaamini hata kidogo. Ukiona majitu yamefikia mpaka kugawana rushwa bungeni ili kupitisha muswaada uchwara unaopingwa na asilimia kubwa ya Watanzania basi hayo majitu ni kuyaogopa kama UKOMA.

Ukiona majitu yamemkolimba kolimba kwa kusema ukweli kwamba MACCM yamepoteza mwelekeo basi hayo majitu ni kuyaogopa kama ukoma.

Angalia jinsi mnavyomdhalilisha Nape kosa lake ni kupinga uhuni na ujambazi wa Mkolomije.

Hahahahahaaaaaa. Umewaza kwa sauti kubwa. Mpigie Makene fastaaaaa
 
Ah wapi aache kuzingua watu huyo....
Yani CCM hii hii ya sasa ninayoifahamu chini ya mheshimiwa na mtukufu sana wawape chadema kuutumia huo ukumbi??
Kama viwanja vya mpira kama kirumba, sheikh abeid na vingine ambavyo vimejengwa kwa pesa za walipa kodi wa nchi hii na kumilikiwa na CCM ni mwiko kutumiwa na vyama vingine itakuja kuwa huo ukumbi wa Dodoma walioujenga wenyewe??!!
Aache masikhara huyo
 
Back
Top Bottom