Polepole: CCM kuna majizi makubwa, kila nikitaka kuwataja wakubwa wananizuia! | Hao wakubwa ni nani zaidi ya M/kiti? Ukiwa CCM hukamatiki?

Kweli ccm wanapata tabu sana juu ya Chadema. Hakuna siku Polepole atazungumza bila kukitaja chama na M/K wake.

Polepole kwanza wewe wenye cm yao wanakudharau. Ww umewekwa pale tu ili kiti kile kisiwe wazi. Huna ubavu wala uhuru wakuwataja hadharani wezi wa ccm. Kwanini usubiri orodha? Hebu anza na Kangi Logola maana M/K wako ameshaweka wazi wizi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Katibu wa Itikadi Na Uenezi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole anasema mbele ya Kamera na vinasa sauti, Kuwa ndani ya Chama cha Mapinduzi kuna majizi Na anawajua ila Kila akiomba ruhusa awataje wakubwa ndani ya Chama wanamzuia.

Najiuliza maswali
1.Hao wakubwa wanaomzuia Polepole asiwataje ni akina Nani?wakubwa kiitifaki Kwa Polepole ni akina Nani?

2.Majizi ndani ya Chama wao hawakamatwi?Kwa hiyo Takukuru wanamipaka ya nani akamatwe na Nani asikamatwe?

Kama ndiyo tunavyoendesha nchi hivi,basi Safari yetu ni ndefu sana.

Hivi some of these guys Magufuli anawaokota wapi.... Jalalani!? Yaani hakuna elements za uongozi hata kidogo....!!
 
Kamuulize huyo polepole!

Kwakuwa serikali inapambana na wezi na mafisadi Polepole awataje, ili sisi tunaosema kuwa serikali haipambani na wezi au mafisadi, bali inapambana na matumizi ya neno fisadi watuzibe midomo. Hapo tutajua waliochukuliwa hatua sio visa bali ni vita isiyo na macho. Kinyume na hapo kwetu tunaona sio vita ya ufisadi, bali ni matumizi mabaya ya madaraka na chuki binafsi kwa baadhi ya watu.
 
Kaanza kuvuka mipaka sasa

Sio anavuka mipaka, sema akiwataja hao watamtaja na mwenyekiti wake. Nguvu kubwa inayotumika kuminya na kuwaumiza wapinzani ni ili ccm ionekane iko vizuri. Lakini inaonekana kuna msuguano wandani wa ccm wezi, na hao ccm academia under Magufuli, na kuna kundi linataka kumwaga mboga.
 
Anawafumba vinywa wapinzani kwamba hao mnaotaka kuwataja kama pale mwembeyanga sisi tunawajua hivyo hakutakuwa tena na List of shame kuelekea uchaguzi October.
Huoni tulivyowaharibia agenda ya Kangi na genge lake?? Upinzani hamtapata tena hoja kwani mafisadi tunawashughulikia kweli kweli kimatendo. Hao mtakao waibua tutasema; Tulikuwa tunawashughulikia

Mkuu kwani Kange ameshughulikiwa? Wanaoshughulikiwa si wanakutana na mkono wa sheria?
 
Back
Top Bottom