Polepole asema gazeti la Habari leo limepotosha juu ya m/kiti wa ccm kupita bila kupingwa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Screenshot_2017-03-24-12-01-44.png
Habari hii kama ilivyorushwa na kuandikwa sio ya kweli, imelenga kufanya upotoshaji. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinalaani mbinu za hila za kupotosha Dhamira njema ya CCM kufanya Mageuzi ya kukiimarisha Chama chetu. Naomba mpuuze taarifa hizi za upotoshwaji. Asante..

Mdau mmoja kamwuliza:
Ukisema huu ni uongo, inabidi useme ukweli wake...

Weka hapa mabadiliko yote yaliyofanywa ili kuondoa utata.

Kaingia mitini
 
Chanzo ni kipi sasa?
Hivi mnakuwaje? Miaka yote ya kufundishwa kwamba ukileta habari tuekeeni na chanzo,hamuelewi tuu.

WEKA PICHA NA CHANZO,SASA HIVI.
 
Ewe Polepole enenda polepole usimkanyage mwenzio. Chama kina wenyewe sasa na wenyewe ni bashite na babake.
 
Sasa pole pole na wewe na kuna akili yako ni Pole pole.kama ni taarifa za uwongo za ukweli ni zipi? Mnaficha nini wananchi wasijue?
 
Huyo polepole ajue kuwa mambo sasa yameshakwenda ndivyosivyo ukimwaga ugali mwenzako Ana mwaga unga na mwaka huu atakanusha mpaka povu limuishe
 
Nasikia wenye chama wamemgomea kupita bila kupingwa 2020,ajiandae kupambana na membe na nape.And this time around jk won't come to the rescue,you are on your own
 
nasubir kura za maoni za kupitisha mgombea wao 2020 lazima kivumbi kitokeee ccm watamuonesha umafia sizonjee
 
Kuna maajabu yanatokea. Yaani leo taarifa mbili za CCM (mkutano wa Kinana na waandishi na Raisi kutokuwa challenged) zilizoandikwa na gazeti la serikali pro-CCM zinakanushwa (Magufuli na Polepole). Ina maana hili gazeti haliaminiki au kuna tunachofichwa?
 
Watawala wa kiimla hawapendi mambo na mikakati yao ijulikane mapema.
 
Back
Top Bottom