Polepole anamshangaa Nyalandu kuondoka CCM inayofuata itikadi ya Ujamaa purely na kujiunga chama kisicho na itikadi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,607
141,429
Karibu ufuatilie mjadala!

Polepole anamshangaa Nyalandu kuondoka CCM inayofuata itikadi ya Ujamaa purely na kwenda kujiunga kwenye chama kisicho na itikadi yoyote. Anadai huyu ameshuka viwango na hajawahi kuitisha mikutano na wapiga kura wanamtafuta jimboni yeye hajulikani alipo.

Mwenezi anasema kuna wabunge wengi wanachunguzwa ndani ya chama kufuatia ushauri uliotolewa na spika kwa mwenyekiti wa CCM, hivyo wananchi wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu kamati za uchunguzi zitamaliza kazi na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wabunge wote watakaokutwa na kasoro mbalimbali!

Pia amemponda yule mbunge wa Kigoma aliyesahau shughuli zake za kibunge jimboni na kuzamia Dar alikojipa jukumu la kuishambulia serikali kwa kila jambo, liwe jema au vinginevyo!
 
Polepole ana haki ya kuongea kwani kuondoka kwa madiwani wa chadema ilikuwa nongwa mpaka Video shooting ilifanyika, Msigwa, Nassari na Lema wakasahu kama wanauguliwa kila kona wanatembea na frash sasa vipi polepole anyamaze kimya kuondokewa na mbunge
 
Karibu ufuatilie mjadala!

Siku zote Mtu aliye makini Kichwani huwa hakurupuki kufanya ' Counter ' ya jambo lolote lile very ' sensitive ' haraka hivi kama afanyavyo Msemaji wa CCM Humphrey Polepole. Kitendo hiki cha ' kuhama ' kwa Lazaro Nyalandu kinahitaji utulivu na umakini mkubwa katika kulijibia au kulitolea ufafanuzi. Ni mmoja kati ya Wasemaji ' hopeless ' ambao kwa miaka mingi Chama cha CCM haikuwahi kuwa nae.

Kuhama kwa Lazaro Nyalandu ni ' ishara ' tosha kwamba ndani ya CCM huenda kuna ' matatizo ' makubwa tena ya ' hatari ' kuliko ambavyo tunaaminishwa. Na bahati mbaya mno hilo ' tatizo ' halisemwi ila kuna ' Mtu ' mmoja ambaye namuita ' Kirusi ' Kikuu ndani ya Serikali ya CCM na kwa bahati mbaya sana hicho ' Kirusi ' ndicho kinapendwa na kusikilizwa mno na Mwenyekiti Taifa wa CCM hadi kinasikilizwa kuliko hata Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Kama hiki ' Kirusi ' Kikuu kilichopo Serikalini na ndani ya Chama cha CCM hakitadhibitiwa haraka natabiri ama ' anguko ' kubwa la CCM au ' machafuko ' makubwa yanakuja hasa mwaka 2020 kwani huyo ' Kirusi ' hivi sasa inasemekana amefikia hatua hadi anaingilia taratibu zingine tena za Idara / Taasisi ' Nyeti ' kabisa za nchi hii huku akijivunia ' Kupendwa ' na ' Kukubalika ' na Mwenyekiti Taifa.

Kwa siku za hivi karibuni na kama una macho yaliyojaa ' Saikolojia ' ya ' Body Language ' kila pakiwa na hafla pale IKULU halafu akawepo Makamu wa Rais na Jaji Mkuu achilia mbali Spika Ndugai ambaye ametukuka ' Kiunafiki ' utagundua ya kwamba ndani ya ' mioyo ' ya Samia ( VP ) na Juma ( CJ ) wanaumia sana na kuna ' Kitu ' hakipo sawa ndani ya ' Serikali ' na hata ' Chamani ' pia.

Ukiyasoma kwa umakini na kwa uangalifu mkubwa mno ' maelezo ' aliyoyatoa leo Lazaro Nyalandu utagundua kuna ' bomu ' lipo Serikalini na katika Chama na pengine badala ya Watu hasa wa CCM ' kumponda ' na ' kumkashifu ' mngetulia na kujitafakari kwa kina hasa mkitambua kwamba huyo Nyalandu ameshika ' nyadhifa ' nyingi za Kiserikali na Kichama hivyo ni ' Senior ' kabisa na kuanza ' kumpuuza ' na ' kummbeza ' ni kuonyesha ' udhaifu ' mkubwa wa akili na kufikiri.

Kuna ' hatari ' naiona na naomba niishie hapa tafadhali. Na bahati mbaya sana wengine tukisema, tukishauri na tukionya kwa maslahi mapana tunaonekana Sisi ni Wana CCM ' Vipepeo ' na siyo Wana CCM ' Viwanda ' wakati pengine inawezekana ' mawazo ' au ' mitazamo ' yetu ambayo huwa tunaitoa mara kwa mara humu JamiiForums ingeweza kusaidia na kukiweka Chama mahala pazuri na hata kuisaidia Serikali yetu. Namalizia tena kusema kuwa ' kuna hatari naiona ' na CCM pamoja na Serikali yake isipojitathmini haraka tutakuja ' Kujuta ' sana na mno hapo baadae.
 
Hapo kwa Spika siyo kama ameteleza kweli, hata kama Spika alitoa ushauri kwa m/kiti juu ya kuchunguzwa kwa wabunge wao na kuwachukulia hatua, je ni sahihi kuongea siri za ndani kwenye media! Mmmh ama kweli chama kimepata msemaji
Kwani Spika ushauri huo aliutoa kwa siri?!! Mbona wengi tulimsikia alivyoyasema hayo pale Ikulu akiwemo Silinde na Ole milya!!
 
Siku zote Mtu aliye makini Kichwani huwa hakurupuki kufanya ' Counter ' ya jambo lolote lile very ' sensitive ' haraka hivi kama afanyavyo Msemaji wa CCM Humphrey Polepole. Kitendo hiki cha ' kuhama ' kwa Lazaro Nyalandu kinahitaji utulivu na umakini mkubwa katika kulijibia au kulitolea ufafanuzi. Ni mmoja kati ya Wasemaji ' hopeless ' ambao kwa miaka mingi Chama cha CCM haikuwahi kuwa nae.

Kuhama kwa Lazaro Nyalandu ni ' ishara ' tosha kwamba ndani ya CCM huenda kuna ' matatizo ' makubwa tena ya ' hatari ' kuliko ambavyo tunaaminishwa. Na bahati mbaya mno hilo ' tatizo ' halisemwi ila kuna ' Mtu ' mmoja ambaye namuita ' Kirusi ' Kikuu ndani ya Serikali ya CCM na kwa bahati mbaya sana hicho ' Kirusi ' ndicho kinapendwa na kusikilizwa mno na Mwenyekiti Taifa wa CCM hadi kinasikilizwa kuliko hata Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Kama hiki ' Kirusi ' Kikuu kilichopo Serikalini na ndani ya Chama cha CCM hakitadhibitiwa haraka natabiri ama ' anguko ' kubwa la CCM au ' machafuko ' makubwa yanakuja hasa mwaka 2020 kwani huyo ' Kirusi ' hivi sasa inasemekana amefikia hatua hadi anaingilia taratibu zingine tena za Idara / Taasisi ' Nyeti ' kabisa za nchi hii huku akijivunia ' Kupendwa ' na ' Kukubalika ' na Mwenyekiti Taifa.

Kwa siku za hivi karibuni na kama una macho yaliyojaa ' Saikolojia ' ya ' Body Language ' kila pakiwa na hafla pale IKULU halafu akawepo Makamu wa Rais na Jaji Mkuu achilia mbali Spika Ndugai ambaye ametukuka ' Kiunafiki ' utagundua ya kwamba ndani ya ' mioyo ' ya Samia ( VP ) na Juma ( CJ ) wanaumia sana na kuna ' Kitu ' hakipo sawa ndani ya ' Serikali ' na hata ' Chamani ' pia.

Ukiyasoma kwa umakini na kwa uangalifu mkubwa mno ' maelezo ' aliyoyatoa leo Lazaro Nyalandu utagundua kuna ' bomu ' lipo Serikalini na katika Chama na pengine badala ya Watu hasa wa CCM ' kumponda ' na ' kumkashifu ' mngetulia na kujitafakari kwa kina hasa mkitambua kwamba huyo Nyalandu ameshika ' nyadhifa ' nyingi za Kiserikali na Kichama hivyo ni ' Senior ' kabisa na kuanza ' kumpuuza ' na ' kummbeza ' ni kuonyesha ' udhaifu ' mkubwa wa akili na kufikiri.

Kuna ' hatari ' naiona na naomba niishie hapa tafadhali. Na bahati mbaya sana wengine tukisema, tukishauri na tukionya kwa maslahi mapana tunaonekana Sisi ni Wana CCM ' Vipepeo ' na siyo Wana CCM ' Viwanda ' wakati pengine inawezekana ' mawazo ' au ' mitazamo ' yetu ambayo huwa tunaitoa mara kwa mara humu JamiiForums ingeweza kusaidia na kukiweka Chama mahala pazuri na hata kuisaidia Serikali yetu. Namalizia tena kusema kuwa ' kuna hatari naiona ' na CCM pamoja na Serikali yake isipojitathmini haraka tutakuja ' Kujuta ' sana na mno.
mtajua wenyewe na ccm yenu sisi tulishamuachia mungu afanye kazi yake
tunayaona sasa
 
Channel 10 na TBC nilisha zifuta kwenye king'amuzi changu kwa sababu ya upuuzi wa kuwabeba hao uchwara
 
mtajua wenyewe na ccm yenu sisi tulishamuachia mungu afanye kazi yake
tunayaona sasa

Mkuu kwani kuwa CCM ni dhambi? Una uhakika kwamba huko uliko au unakoamini Wewe hakuna matatizo? Nilichojaribu kukisema hapa ni mtizamo wangu kama mmoja wa ' Wadau ' wa CCM ili ' Wahusika ' wakiangalie na kifanyiwe Kazi haraka kwa maslahi mapana na Chama cha CCM na haimaanishi kwamba kwakuwa kuna matatizo fulani basi Mimi GENTAMYCINE niikimbie CCM bali nadhani ' maandiko ' yangu haya ambayo nayatoa humu katika hii platform nzuri ya JamiiForums yanaweza yakasaidia japo kidogo katika ' kurekebisha ' mambo fulani. Alichokifanya Lazaoro Nyalandu ni haki yake Kikatiba na ndiyo maana nawashangaa hata wale wana CCM wenzangu wanaomponda na kumkashifu.
 
Haishangazi kuondoka kwake ingawa alianza kuonyesha hayo kupitia ajali ya Arusha.

Jamani tukae mkao wa popcorn maana awamu hii inamengi mazuri kwa ajili ya nchi yetu.

Watu wanasaga meno hadi basi jamani...

Magufuli oyeeeeeeeeeee

Nape naye aliyasema kwa kideo hiki
 
Attachments

  • VID-20171030-WA0051.mp4
    1.3 MB · Views: 53
Ccm ni chama kikomavu kisicho na wanachama wakomavu,
Maana wangekuwa wakomavu kukwepa aibu wangekuwa wanakaa kimya kuficha aibu ipite
 
Siku zote Mtu aliye makini Kichwani huwa hakurupuki kufanya ' Counter ' ya jambo lolote lile very ' sensitive ' haraka hivi kama afanyavyo Msemaji wa CCM Humphrey Polepole. Kitendo hiki cha ' kuhama ' kwa Lazaro Nyalandu kinahitaji utulivu na umakini mkubwa katika kulijibia au kulitolea ufafanuzi. Ni mmoja kati ya Wasemaji ' hopeless ' ambao kwa miaka mingi Chama cha CCM haikuwahi kuwa nae.

Kuhama kwa Lazaro Nyalandu ni ' ishara ' tosha kwamba ndani ya CCM huenda kuna ' matatizo ' makubwa tena ya ' hatari ' kuliko ambavyo tunaaminishwa. Na bahati mbaya mno hilo ' tatizo ' halisemwi ila kuna ' Mtu ' mmoja ambaye namuita ' Kirusi ' Kikuu ndani ya Serikali ya CCM na kwa bahati mbaya sana hicho ' Kirusi ' ndicho kinapendwa na kusikilizwa mno na Mwenyekiti Taifa wa CCM hadi kinasikilizwa kuliko hata Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Kama hiki ' Kirusi ' Kikuu kilichopo Serikalini na ndani ya Chama cha CCM hakitadhibitiwa haraka natabiri ama ' anguko ' kubwa la CCM au ' machafuko ' makubwa yanakuja hasa mwaka 2020 kwani huyo ' Kirusi ' hivi sasa inasemekana amefikia hatua hadi anaingilia taratibu zingine tena za Idara / Taasisi ' Nyeti ' kabisa za nchi hii huku akijivunia ' Kupendwa ' na ' Kukubalika ' na Mwenyekiti Taifa.

Kwa siku za hivi karibuni na kama una macho yaliyojaa ' Saikolojia ' ya ' Body Language ' kila pakiwa na hafla pale IKULU halafu akawepo Makamu wa Rais na Jaji Mkuu achilia mbali Spika Ndugai ambaye ametukuka ' Kiunafiki ' utagundua ya kwamba ndani ya ' mioyo ' ya Samia ( VP ) na Juma ( CJ ) wanaumia sana na kuna ' Kitu ' hakipo sawa ndani ya ' Serikali ' na hata ' Chamani ' pia.

Ukiyasoma kwa umakini na kwa uangalifu mkubwa mno ' maelezo ' aliyoyatoa leo Lazaro Nyalandu utagundua kuna ' bomu ' lipo Serikalini na katika Chama na pengine badala ya Watu hasa wa CCM ' kumponda ' na ' kumkashifu ' mngetulia na kujitafakari kwa kina hasa mkitambua kwamba huyo Nyalandu ameshika ' nyadhifa ' nyingi za Kiserikali na Kichama hivyo ni ' Senior ' kabisa na kuanza ' kumpuuza ' na ' kummbeza ' ni kuonyesha ' udhaifu ' mkubwa wa akili na kufikiri.

Kuna ' hatari ' naiona na naomba niishie hapa tafadhali. Na bahati mbaya sana wengine tukisema, tukishauri na tukionya kwa maslahi mapana tunaonekana Sisi ni Wana CCM ' Vipepeo ' na siyo Wana CCM ' Viwanda ' wakati pengine inawezekana ' mawazo ' au ' mitazamo ' yetu ambayo huwa tunaitoa mara kwa mara humu JamiiForums ingeweza kusaidia na kukiweka Chama mahala pazuri na hata kuisaidia Serikali yetu. Namalizia tena kusema kuwa ' kuna hatari naiona ' na CCM pamoja na Serikali yake isipojitathmini haraka tutakuja ' Kujuta ' sana na mno.
Wewe jamaa una IQ kubwa sana hongera sana mkuu nimependa unavopangilia hoja zako hongera mno
 
Hapo kwa Spika siyo kama ameteleza kweli, hata kama Spika alitoa ushauri kwa m/kiti juu ya kuchunguzwa kwa wabunge wao na kuwachukulia hatua, je ni sahihi kuongea siri za ndani kwenye media! Mmmh ama kweli chama kimepata msemaji
Kamchonganisha subwoofer na mkiti
 
Back
Top Bottom