Polepole anamshangaa Nyalandu kuondoka CCM inayofuata itikadi ya Ujamaa purely na kujiunga chama kisicho na itikadi

Siku zote Mtu aliye makini Kichwani huwa hakurupuki kufanya ' Counter ' ya jambo lolote lile very ' sensitive ' haraka hivi kama afanyavyo Msemaji wa CCM Humphrey Polepole. Kitendo hiki cha ' kuhama ' kwa Lazaro Nyalandu kinahitaji utulivu na umakini mkubwa katika kulijibia au kulitolea ufafanuzi. Ni mmoja kati ya Wasemaji ' hopeless ' ambao kwa miaka mingi Chama cha CCM haikuwahi kuwa nae.

Kuhama kwa Lazaro Nyalandu ni ' ishara ' tosha kwamba ndani ya CCM huenda kuna ' matatizo ' makubwa tena ya ' hatari ' kuliko ambavyo tunaaminishwa. Na bahati mbaya mno hilo ' tatizo ' halisemwi ila kuna ' Mtu ' mmoja ambaye namuita ' Kirusi ' Kikuu ndani ya Serikali ya CCM na kwa bahati mbaya sana hicho ' Kirusi ' ndicho kinapendwa na kusikilizwa mno na Mwenyekiti Taifa wa CCM hadi kinasikilizwa kuliko hata Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Kama hiki ' Kirusi ' Kikuu kilichopo Serikalini na ndani ya Chama cha CCM hakitadhibitiwa haraka natabiri ama ' anguko ' kubwa la CCM au ' machafuko ' makubwa yanakuja hasa mwaka 2020 kwani huyo ' Kirusi ' hivi sasa inasemekana amefikia hatua hadi anaingilia taratibu zingine tena za Idara / Taasisi ' Nyeti ' kabisa za nchi hii huku akijivunia ' Kupendwa ' na ' Kukubalika ' na Mwenyekiti Taifa.

Kwa siku za hivi karibuni na kama una macho yaliyojaa ' Saikolojia ' ya ' Body Language ' kila pakiwa na hafla pale IKULU halafu akawepo Makamu wa Rais na Jaji Mkuu achilia mbali Spika Ndugai ambaye ametukuka ' Kiunafiki ' utagundua ya kwamba ndani ya ' mioyo ' ya Samia ( VP ) na Juma ( CJ ) wanaumia sana na kuna ' Kitu ' hakipo sawa ndani ya ' Serikali ' na hata ' Chamani ' pia.

Ukiyasoma kwa umakini na kwa uangalifu mkubwa mno ' maelezo ' aliyoyatoa leo Lazaro Nyalandu utagundua kuna ' bomu ' lipo Serikalini na katika Chama na pengine badala ya Watu hasa wa CCM ' kumponda ' na ' kumkashifu ' mngetulia na kujitafakari kwa kina hasa mkitambua kwamba huyo Nyalandu ameshika ' nyadhifa ' nyingi za Kiserikali na Kichama hivyo ni ' Senior ' kabisa na kuanza ' kumpuuza ' na ' kummbeza ' ni kuonyesha ' udhaifu ' mkubwa wa akili na kufikiri.

Kuna ' hatari ' naiona na naomba niishie hapa tafadhali. Na bahati mbaya sana wengine tukisema, tukishauri na tukionya kwa maslahi mapana tunaonekana Sisi ni Wana CCM ' Vipepeo ' na siyo Wana CCM ' Viwanda ' wakati pengine inawezekana ' mawazo ' au ' mitazamo ' yetu ambayo huwa tunaitoa mara kwa mara humu JamiiForums ingeweza kusaidia na kukiweka Chama mahala pazuri na hata kuisaidia Serikali yetu. Namalizia tena kusema kuwa ' kuna hatari naiona ' na CCM pamoja na Serikali yake isipojitathmini haraka tutakuja ' Kujuta ' sana na mno hapo baadae.
Mkuu kuna weza kukawa kuna tatizo kwenye CCM yenu lakini Nyalandu kajitoa sababu mojawapo hali tete kwenye vichaka alivyotjitengenezea kule wizara aliyowahi kuiongoza.
Kwani nani hajui kuhusu wale watu weupe walivyomtumia na yeye alivyofikiria watamfikisha jumba jeupe?
Sasa mirija imebanwa na vichaka vyote akina Kigwa wamevitia kiberiti.
 
Polepole ana haki ya kuongea kwani kuondoka kwa madiwani wa chadema ilikuwa nongwa mpaka Video shooting ilifanyika, Msigwa, Nassari na Lema wakasahu kama wanauguliwa kila kona wanatembea na frash sasa vipi polepole anyamaze kimya kuondokewa na mbunge
Frash.,.teheteheee
 
Wakuu.

Ni lazima kua na tafakari pana ambayo itatupeleka pazuri, hawa watanzania sio wajinga kukaa kimya na muda mwingine nyuso zao huongea.

Kuna kila sababu ya kujiuliza kwa nini biashara kwa sasa Tanzania haipo kama zamani, kwa nini hali ni ngumu kwa mtanzania wa kawaida?

Nyalandu ashaondoka nitashangaa watu kutukana mitandaoni wakati mtu katimiza matakwa ya katiba na ni haki yake kimsingi kabisa.

Tusimtukane Nyalandu tuangalie kosa liko wapi , lazima kuna kosa kubwa na wengi hawaridhishwi na mambo yalivo.
 
Karibu ufuatilie mjadala! Polepole anamshangaa Nyalandu kuondoka CCM inayofuata itikadi ya Ujamaa purely na kwenda kujiunga kwenye chama kisicho na itikadi yoyote. Anadai huyu ameshuka viwango na hajawahi kuitisha mikutano na wapiga kura wanamtafuta jimboni yeye hajulikani alipo. Mwenezi anasema kuna wabunge wengi wanachunguzwa ndani ya chama kufuatia ushauri uliotolewa na spika kwa mwenyekiti wa CCM, hivyo wananchi wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu kamati za uchunguzi zitamaliza kazi na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wabunge wote watakaokutwa na kasoro mbalimbali! Pia amemponda yule mbunge wa Kigoma aliyesahau shughuli zake za kibunge jimboni na kuzamia Dsm alikojipa jukumu la kuishambulia serikali kwa kila liwe jema au vinginevyo!
Polepole muongo kabisa mbona kwenye tv anaenda siku nyingi mbonahajawai kusema nyalandu anatafutwa na wapiga kura wenzake wa
Jimboni kwao kwanza nimsahihishe hapo sio wapiga kura wake amesubiri ametoka ndioamchonganishe na wanajimbo wenzake nakama kunawengine ambaowanawachunguza aweke adharani akija akisema baada yamtu kujitoa mpuuzeni hanamana achukuehatua sasa
 
Ulichosema ni sahihi na ukweli usiopingika. Sasa hao 27, wakifuata ndo matusi yatapendeza na kusaidia zaidi.

CCM endeleeni, mavuno ya mlichopanda yamefikia, sisi tutawapa makapu na viroba mkajaze mtakachovuna.mkiambiwa mtawala wenu anakopeleka nchi sipo.

Mnamsifia na kumdanganya kuwa yy ni Masihi, na utumishi wake umetukuka ! Kuuwa watu, kunyima haki, ni kutukuka !! Kutamkia wananchi maisha ya kishetani,nikutukuka !! Hapa ndipo nchi ilipofika !

Mungu, sitachoka kukuita juu ya huu utawala na wachache wanaunga mkono kupatiwa mateso kwa walio wengi.

Muumba wangu gharikisha,laana iliyo kuu,mateso na fedheha isiyo kipimo ktk huu utawala,kila kiumbe chini ya jua kishuhudie na kukutukuza kwamba hakika,hukumu hiyo imetoka kwako wewe uliye Masihi na hastahili awaye yeyote kuchangia Jina wala utukufu na wewe. Amen.
 
Ujinga na upumbavu bado vinaendelea,kiongozi wa chama anadai eti Nyalandu anatafutwa na wapiga kura wake lakini haonekani,chaajabu nikwakiongozi kulalamika badala ya kuchukuwa hatua.Eti ooo tunachunguza,heee unachunguza nini wakati umesema wananchi wanalalamika kuwa hawamuoni mbunge wao? Kweli hiki chama kimepoteza mwelekeo,na haya yalianza pindi Nyalandu alipoenda Nairobi.Yaani anaonekana ni msaliti.
 
Vyuma vimekaza sana, Mpaka marafiki na ndugu tumepoteana .

Ingekuwa mpira tunaongelea Barcelona 2004/2005 ilivyokuwa pale katikati kwenye kiungo inapiga pasi dakika 20 huku wakiwa wameshinda noma sana leo undugu na urafiki umekufa watu wanapambana na njaa zao
 
Karibu ufuatilie mjadala! Polepole anamshangaa Nyalandu kuondoka CCM inayofuata itikadi ya Ujamaa purely na kwenda kujiunga kwenye chama kisicho na itikadi yoyote. Anadai huyu ameshuka viwango na hajawahi kuitisha mikutano na wapiga kura wanamtafuta jimboni yeye hajulikani alipo. Mwenezi anasema kuna wabunge wengi wanachunguzwa ndani ya chama kufuatia ushauri uliotolewa na spika kwa mwenyekiti wa CCM, hivyo wananchi wakae mkao wa kula kwani muda si mrefu kamati za uchunguzi zitamaliza kazi na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wabunge wote watakaokutwa na kasoro mbalimbali! Pia amemponda yule mbunge wa Kigoma aliyesahau shughuli zake za kibunge jimboni na kuzamia Dsm alikojipa jukumu la kuishambulia serikali kwa kila liwe jema au vinginevyo!
Walewale
 
WanaCCM wataelewa hicho unachokisema siku wakiona hadi mama Janeth akisepa zake na kuachana na CCM.
Siku hazigandi, wewe subiri tu.
Mkuu, unawazungumzia wanaccm wa humu mtandaoni?
Watamuogesha matusi huyo mama mpaka utastaajabu!
 
Razaro Nyalandu ni mmoja wa majasusi walotukuka na hata alipokuwa pale Ilboru wazee wa Kitengo, walimwona kwamba anafaa kuandaliwa kuja kuwa mwanachama na mwanasiasa mwandamizi katika siasa za Tanzania.

Lakini wazee wa Kitengo waliamua kukuweka pamoja na akina Lowasa, Sumaye na waandamaizi wengine wa CCM basi wewe hauna chako.

Mbinu ya Nyalandu ni kuondoka halafu arudi tena bungeni kupitia Chadema, lakini nakuhakikishieni hatopita na sasa Chadema wanafikria mara mbilimbili juu ya ombi lake.

Sasa kazi wanayo akina Membe, Nape na Makamba Junior kusawazisha.

Lakini Polepole anasahau kwamba yupo mzee Yusuph Makamba ambae anayo makabrasha yote, kwanini asiombe reference?

Ni hayo tu kutoka kwa Richard hapa Kwamtogole, oops umeme umekatika!

Ntarudi.

Wewe ndio aina ya majasusi wapumbavu kuwahi kutokea sijui wako wapi wale vijana wa Nyerere walioweza kunusa kila kitu na ku neutralize kabla halija haribu image yoyote ya serikali

Nyalandu hatopita kwenye uchaguzi wa jimbo lake kwa maneno ya khanga haya bila kutupa facts na kutishia sijui nawa hakikishieni? Mtajifunza lini ninyi?

Ndio tutegemee utamshauri sponsor wako kwenye maswala ya uchumi, ulinzi nk?

Na kwa bahati mbaya wewe ndio aina ya washauri wanao pendwa na mkuu
Nyalandu akishinda uchaguzi kupitia chadema nitakutafuta

Off topic hiyo Tandale umerudi lini?
Treni za district line na Picaddily huzipandi na junk food za Burger King au makuku yenu ya Sainsbury na Tesco ushayachoka?

NB haitwi Razaro anaitwa Lazaro jasusi gani wewe hata jina tu huwezi ku copy?
 
Back
Top Bottom