Polepole amjibu Lowassa(CHADEMA) kuhusu kusamehewa kwa Babu Seya

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,761
5,877
"Hizi habari zipuuzwe zipuuzwe katika kiwango kikuu kabisa kwa sababu kwanza mtu ambaye amesema hana uhalali kwa alichokisema. Ni mtu ambaye hivi karibuni wamekuwa na mtu wa kudandia hoja kila jambo zuri linalofanywa amekuwa akidai kuwa yeye ndio muasisi wa jambo hilo, mtu anayeshindwa mara zote hupenda kuchuka sifa hata katika mambo yasiyomuhusu." Anasema Polepole

"Nikizungumzia hili la ndugu rais kusamehe wafungwa, mchakato wa kusamehe wafungwa upo kwa mujibu wa katiba na wafungwa wamekuwa wakisamehewa baada ya kukidhi vigezo fulani muhimu. Kwamba mchakato wake umekidhi masharti ya msingi ambayo mtu naweza kusamehewa. Rais amepewa mamalaka hayo kikatiba kwa mba anamsamehe mtu ambaye ameona anastahili msamaha baada ya mchakato maalumu madhubuti kabisa kukamilika" anaendelea kusema Polepole

Polepole anaendelea kwa kusema kuwa;

"Hili sio jambo la kubahatisha jambo la mtu kusema amemshawishi rais. Huyu mzee ambaye amezungumza kuwa hii ilikuwa ni ahadi yake wakati wa kampeni ni mzee ambaye amehudumu kwenye serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kipindi Babu Seya anafungwa huyu mzee alikuwa Waziri Mkuu, tena hakuwa waziri Mkuu bali waziri mkuu mwenye nguvu sana, kama alijua Babu Seya labda hakutendewa haki kwa namna yoyote kwa fikra zake angaliweza kumshauri rais wake kwa kipindi hicho kuwa huyu mtu hastahili kufungwa asamehewe"

"Kashindwa kuzuia asifungwe, kashindwa kwa miaka mingi kumshawishi rais wake amsamehe. leo mtu ambaye hakuwa sehemu ya uamuzi wala hakuwa na sehemu nyeti katika serikali, Ndugu Magufuli kipindi hicho alikuwa waziri wa kawaida tu, baada ya tafakuri ya kina na tathini yadidifu ya miaka miwili akaon akatika watu wamejirudi na kustahili msamaha. Huyo mzee anaibuka, aache tabia za kizandiki na kinafki watanzania wanataka upinzani unaojenga hoja na sio unaorukia hoja zisizowahusu"
 

Attachments

  • VID-20171210-WA0000.mp4
    14.2 MB · Views: 64
Huu jamaa inabidi apimwe uwezo wake wa kufikili maana hatumuelewi
 
Atasaidiwa na polisi
Ndiyo yanafanyika hayo huku watazidi kupanda mbegu ya chuki zaidi. Kwani baada ya chuki mwisho wake chama kama chama hakijui kitavuna. Kwa hiyo chama kujitadhimini kuendana mambo ya kutumia nguvu inayoacha chuki kwa Watanzania. Na Siasa za aina hii hutakaa utekeleze Ilani kwani siku zote utakuwa ufikirii chochote zaidi ya muda mwingi kufikiria namna ya kupambana na wapinzani.Siasa ni hoja kwa hoja sio ubabe au Kejeli
 
Nakumbuka 2015 during kampeni EL aliulizwa na wananchi kuhusu babu seya na mwanae pamoja na Daudi Balali.
Jibu nakumbuka lilikuwa "mkinichagua kuwa rais nitamtoa babu seya na pia nitamleta Saudi balali" watu walishangilia sana, sasa nasubiri huyo wa mwisho dalali.
 
Back
Top Bottom