security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole aliyepo Mkoani Arusha katika ziara ya kukiimarisha Chama, amekutana na Viongozi wa Kata na Wanachama wa CCM Wilaya za Arusha na Longido.
Katika mazungumzo, wanaCCM wilayani Longido walimuomba Mwenezi huyo wa CCM awasaidie ili waweze kutatua tatizo la upungufu wa chakula inayoikabili Wilaya hiyo, ambapo bei ya debe la mahindi imepanda kutoka 5000 mpaka 30,000 na gunia moja linauzwa kati ya laki moja na nusu mpaka laki mbilu badala ya bei ya awali ya elfu 45,000/=
Nae Ndg Polepole amewaambia Wananchi na wanachama hao kuwa ameiagiza Serikali ya CCM kusambaza chakula zaidi ya Tani 1500 katika Wilaya za Longido, Ngorongoro na Monduli.
Ndg Polepole amesisitiza kuwa CCM ni chama cha watu ambacho kimeundwa na watu kiwasemee, kiwatetee na kuwasimamia kutatua kero na changamoto zao, hivyo CCM haiwezi kujitenga na shida za watu.
Ziara ya Mwenezi huyo wa CCM inaendelea Mkoani Arusha ambapo aategemea kuihitimisha tarehe 7 mwezi huu wa tano na kuelekea Mkoa wa Manyara.