Poleni wazazi wa Abigael kuondokewa na mtoto wenu aliyekanyangwa na gari la taka

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,718
Pole kwa familia nzima, ndugu na jamaa walioguswa na msiba huu.

Niliposikia habari ya kukanyangwa mtoto tena gari la taka nilishtuka sana.

Ila asilimia kubwa makosa wa walezi au wazazi tunajitakia wenyewe.

Mtoto ambaye kuanzia mwaka 1-10 ni wakuwa makini naye sana na zaidi wale kuanzia umri wa miaka 1-6.

Ukitaka kujua wazazi au walezi kutokuwa makini na watoto kwenye uangalizi nenda hospitali ukakute kesi zilizopo, ”kuongua kwa mtoto kwenye maji au mafuta, kuchezea vitu vya hatari, kugongwa na gari na n.k

Inauma sana kuondokewa na mtoto ambaye hata dunia ajaifahamu vizuri.

Wazazi au walezi wengi wanafurahi kuona tu kiumbe kashushwa duniani! Kuhusu kuwa makini na mtoto hapa naona tupo nyuma.

Umri wa miaka 1-6 kiufupi mtoto ni mtundu sana, mwenye kutaka kujifunza mengi .

Sitapenda kulaumu kwa tukio lilotekea halafu ni mtoto wa mwaka 1 inaonesha uzembe ambao asilimia kubwa ulifanywa na mama wa mtoto (samahani kama nitawakwaza).

Hata mitaani unakuta vitoto vidogo vipo mtaani majira usiku vinazurura na kucheza cheza usiku wakati muda wa watoto mwisho saa 12 .

Ugumu wa maisha unafanya wazazi au walezi kutokuwa makini na watoto, mpaka sasa ni tatizo kubwa

IMG_0926.jpg

IMG_0925.jpg


poleni sana .ila tuliopo na watoto tuwe nao makini tusije kujuta
 
Ila mwaka 1 mpaka anagongwa na Lori? daa jamani wazazi tuwe makini sana na watoto!
 
Sheria za barabarani ni za kale mno
Boda boda anapiga honi huku akipita upande co wake.
Nani awakemee boda wanaoua kila siku wanaoua watu kwenye mwendo kasi?
Hawa bodaboda wapo juu ya sheria?????
 
Uswahilini Huku nyumba zimebana..playground ya watoto no barabarani..ndani hakukaliki
 
Back
Top Bottom