Poleni watumishi wa UMMA: Kesho kaeni mbali na TV msije mkazimia, COVID-19 itakuwa sababu

Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,520
2,000
Nianze kutoa pole kwa watumishi wa umma nchini kote, wale wa sekta binafsi neno pole sioni Kama ni sahihi kwao kwa asilimia kubwa Kama hawako ICU basi wamekata pumzi kabisa.

Kesho inaenda kuwa siku ngumu sana kwenu, nawaona "watumishi wa serikali" wanaohudumiwa kila kitu bure kwa Kodi za umma huku wakila mishahara minono na kupewa mafao yao bila usumbufu wamepata sababu ya kuongeza miaka mingine ya maumivu kwenu, hakika kesho ni siku ya huzuni kali kwenu.

Hakuna anaejali upandaji wa gharama za maisha ikiwa kipato chenu hakijawahi kupanda wakati yeye anahudumiwa kila huduma anayotaka bure tena kwa Kodi za umma. Hawajui maumivu ya upandaji wa gharama za maisha huku mtaani na hivyo hawana sababu ya kukujali wewe, wa kiburi cha aliye Shiba hamkumbuki mwenye njaa.

Kwa uzoefu wangu, serikali ikiongeza mishahara mara nyingi sekta binafsi nako waajiri huongeza, ndugu zangu mlioko sekta binafsi na nyie poleni sana mjifunge mkanda najua huko mpaka leo Kuna watu wanalipwa chini ya 100k per month na hakuna anaejali.

Kwa wastaafu, huu mwaka unaenda kuwa mgumu sana yawezekana ukawa mwanzo wa kutolipwa mafao yenu kwa makali zaidi ya yaliyopo kwa miaka 4 iliyopita..poleni sana wazee wangu, waziri Jenister Mhagama hajali kabisa kuhumu cha ajabu Waziri wa utumishi Mkuchika nae juzi bungenu anashangaa na kusikitika nyie kucheleweshewa mafao mpaka wengine mnapoteza maisha.

Cha kushangaza nae hajui nini afanye ili mafao yenu yatoke kwa wakati kama ilivyokuwa awamu zilizopita. Kura niliyopiga tar.25 October 2015 sikutegemea italeta maumivu makubwa kiasi hiki kwenu, NISAMEHENI SANA kwa hili sikujua aslani laiti Kama ningejua nisingepiga kura ambayo imenifanya nimekuwa miongoni mwa watesi wenu.

Kustaafu katika taifa hili leo imekuwa ni zaidi ya laana kwa watumishi wa umma, tembelea ofisi za NSSF/PSSSF uone madhira yanayowakuta hawa wazee, wengi mmetangulia mbele za haki kwa misongo ya mawazo/presha zilizosababishwa na kukosa mafao yao kwa zaidi ya miaka 4, ni kama mnaomba misaada kumbe ni haki yanu na pesa ni zenu.

Matumaini kwenu hayapo tena, ukisema uache kazi uchukue mafao yako ukawe mjasiliamali utaambiwa usubiri mpaka miaka 55 ufike, hakuna namna zaida ya kufunga mikanda ndugu zangu huku mkijua hii nchi inajengwa na watu wenye moyo ambao ni nyie watumishi wa umma na INALIWA na wenye meno ambao ni hao watumishi wa serikali. Hao ndio wanaoshiriki kutunga sheria za kuwakandamiza ikiwa wao haziwahusu.

Chama cha wafanyakazi mmekikabidhi chini ya uongozi wa chama tawala na kinaendeshwa kwa maagizo maalum, msitegemee mapya kesho ndugu zangu na hili ni kosa kubwa mlilofanya kumpa KIONGOZI wa chama tawala uongozi wa chama chenu cha wafanyakazi mtalijutia kipindi chote cha utawala wake.

Muwe na siku njema
Endeleeni kujifukiza

Parabora
Geneva - Switsland

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
2,798
2,000
Unasema tu hapa. Novemba 2020 utakuwa umesahau na kupigia wapiga pushap majukwaani tena.
Kura niliyopiga tar.25 October 2015 sikutegemea italeta maumivu makubwa kiasi hiki kwenu, NISAMEHENI SANA kwa hili sikujua aslani laiti Kama ningejua nisingepiga kura ambayo imenifanya nimekuwa miongoni mwa watesi wenu, Kustaafu katika taifa hili leo imekuwa ni zaidi ya laana kwa watumishi wa umma, tembelea ofisi za NSSF/PSSSF uone madhira yanayowakuta Hawa wazee, wengi mmetangulia mbele za haki kwa misongo ya mawazo/presha zilizosababishwa na kukosa mafao yao kwa zaidi ya miaka 4, ni Kama mnaomba misaada kumbe ni haki yanu na pesa ni zenu.
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
22,566
2,000
Serikali ya kidemokrasia yenye kufuata katiba ya jamhuri ya Malawi inaanza kuingiza dola arobaini kwenye akaunti zote za wafanyakazi wa umma ili kuwapunguzia makali ya Covid19

Ngoja tuisubiri hii ya kijambazi itakuja na nini
 

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
7,577
2,000
Ingekuwa Chadema ndiyo iko madarakani, watumishi wangeongezwa mishahara licha ya taharuki ya Corona, na watu wangewekwa lockdown na kugawiwa vyakula ndani ya miezi sita!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,818
2,000
Hatuna budi kuvishukuru virusi vya Corona. Walau vimetuletea kisingizio kipya badala ya vile vilivyozoeleka kwa miaka yote 4! Mara uhakiki, mara tunanunua ndege, mara wakandarasi wako site!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom