Poleni watanznaia kwa ukandamizaji wa maisha tunayotendewa

Babylon

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
1,332
82
Imenisikitisha na kuniuma sana naweza kusema nimechukia nilikuwa namini hawa watu wana utu inapofika maisha ya mtu wa kawaida hapa kwetu ,lakini sasa wamenifanya nifikirie tena .leo inakuwaje mtu wa kima cha chini kipatao chake cha miaka 65 ndio sawa na kipato cha Mbunge ndani ya Miezi 5 ?Hizi ni moja kati ya lana kwani lana zipo za aina nyingi.

Date::5/1/2009
POSHO ZA WABUNGE:Wafanyakazi Dar wamuunga mkono Slaa

WAFANYAKAZI wa Mkoa wa Dar es Salaam, wameunga mkono hoja ya Mbunge wa Karatu, Dk Wilbrod Slaa kwamba mawaziri na wabunge wanalipwa mishahara mikubwa na ya kutisha.


Walisema hali hiyo pia , inachochea ufisadi na utovu wa nidhamu kazini.


Kauli ya wafanyakazi hao imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutetea wabunge kuwa wanalipwa mishahara midogo.


Kauli hiyo ya wafanyakazi, iko katika risala yao ya kudhimisha sherehe za Mei Mosi zilizofanyika jana.


Walisema kila waziri na mbunge ana malipo yasiyopungua Sh12 milioni kwa mwezi, kiwango ambacho kwa mfanyakazi wa kima cha chini ni sawa na mshahara wa miezi 144 au miaka 12.


"Mfano mbunge au waziri ana malipo si chini ya Sh milioni 12 kwa mwezi kwa mujibu wa marekebisho ya sasa, malipo hayo ni mshahara wa miaka 12 kwa mfanyakazi wa kima cha chini," alisema Katibu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), mkoani Dar es Salaam Everist Mwalongo.


Risala hiyo ilisomwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi.


Mwalongo alisema kima cha chini cha mfanyakazi wa sekta ya umma ni Sh101,480 na sekta binafsi ni Sh65,000.


Alielezea mazingira hayo ya kuwepo kwa pengo kubwa la kiwango cha mishahara, kinawakatisha tamaa wafanyakazi.


Alisema kwa msingi huo kuna haja kwa serikali kushirikiana na vyama vya wafanyakazi katika kupanga upya kima cha chini.


Mwalongo alisema kima cha chini kinacholipwa ni kinyume na katiba ya nchi na sheria ya kazi na kwamba pendekezo lao Tucta ni angalau kifikie Sh315,000 kwa mwezi.


"Kuendelea kulipa mshahara wa sasa licha ya kwamba haitoshi ni kukiuka katiba ya nchi na sheria za kazi, pia kukaribisha mianya ya rushwa, wizi na ufisadi kwa baadhi ya wafanyakazi, jambo ambalo limeanza kuchafua sifa nzuri ya nchi yetu," alisema.


Akijibu hoja hiyo, Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani mkoani Iringa, alisema risala hiyo ni ya kisiasa zaidi na kwamba wabunge na mawaziri hawalipwi mishahara kwa kiwango walichokitaja.


Alisema yuko tayari kuwakaribisha wafanyakazi ofisini kwake ili washuhudie hati za malipo ya mishahara ya ubunge.

Hata hivyo, alikiri kuwa wabunge na mawaziri hupata posho nyingi kwamba hiyo inatokana na nafasi za kazi wanayoifanya.


"Suala la posho lisiwasumbue kwa kuwa kila mtu anakula mezani kwake lakini hata hivyo hawafikii kiwango hicho cha milioni 12," alisema Lukuvi.
 
mimi nilikuwa nawaomba hao wabunge wetu wafikiri kidogo tu siku ambapo hawatakuwa katika hivyo viti na kukosa hayo mafao manono watakuwaje, au ndio watakuwa wameshajilimbikizia jamani hebu waangalie mshahara wa chini na milion saba let alone 12 jamani jamani hivi mungu yuko kweli nchi kama hii ina dhulma namna hii ndo maana hakuna lolote toka mkoloni barabara ni zile zile tu zenye lami laana iko hapa
 
Back
Top Bottom