Nipe Andiko
Senior Member
- Jan 20, 2017
- 133
- 133
Hatuwatayarishi vijana wetu vizuri jinsi ya kuomba vyuo. TCU yenyewe pia imechanganyikiwa na safari hii zile multiple selections zimevuruga. Kuna vijana wameconfirm lakini TCU/Vyuo inaonekana hawaja confirm. Wengine wanasingiziwa kuomba baada ya kuwa approved na TCU kitu ambacho si kweli kwa baadhi ya wanafunzi.
Tunatakiwa tuangalie mambo haya kwa angle mbili: anngle ya mwanafunzi mmoja mmoja lakini pia angle ya taifa. Ukilinganisha ufaulu wa vijana na namba zinazo dahiliwa vyuo vikuu sudhani kama Tanzania imefanya vizuri sana ukilinganisha na jirani zetu. Wakuu wetu wakisimama hupati ujumbe mzuri kuhusu private universities hivyo si ajabu vijana kujazana kwenye government universities, Je tuna sera rafiki za kuweza kusaidia private universities ziweze kuwa na capacity kubwa zaidi na watoe quality education au tunajua kuwazodoa tu?
Vyuo vya serikali vinaelemewa na wanafuzi, havina miundo mbinu ya kutosha matokeo yake masomo hayaendi kwa ufanisi unaotakiwa no wonder tunatoa vijana ambao elimu yao ingeweza kuboreshwa zaidi,
Je tunajua kweli uwezo wa wazazi kusomesha watoto wao vyuo vikuu? Kuna wengine wanasema hilo ni jukumu la mzazi lakini hata nchi zilizoendelea serikali hutoa mikopo. Wakiomba mikopo 60000 ukawapa 30000 una uhakika gani kwamba hao 30000 wataweza kupata karo kwa njia mbadala.
Wachumu watakuambia level ya developmet ya nchi inachochewa na level ya elimu ya nchi hasa university na technical education. Bila investment ya kutosha tusitarajie mabadiliko makubwa.