Poleni wana Mtwara, poleni sana kusini. Hakuna anayezungumza kuhusu kupanda kwa ufaulu Mtwara

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
886
1,000
Habarini wadau!

Hakuna kitu nachokipenda dunia hii kama ukweli na haki, hata uwe unaniumiza kiasi gani lakini ukiwa ukweli tu basi roho yangu inabaki kuwa kwatu kabisa!

Kuanzia muda fulani jana jioni, masaa machache baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka, habari iliyoenea na kusambaa kwa kasi ni kuhusu matokeo fulani ya shule kumi (10) dhaifu zaidi katika matokeo hayo ya jana ya kidato cha nne ambapo katika hizo tisa (9) zimetoka mkoa wa Mtwara. kwakuwa taarifa hiyo ilitolewa muda huhuo wa matokeo basi moja kwa moja ikahusishwa na matokeo ya 2020 na kama kawaida, 'wachambuzi' wakaibuka na chambuzi kedekede kuhusu mtwara na watu wake.

Kama utani nilianza kuona hilo kwenye group la rafiki yangu fulani ambae ni mkuu wa shule huko lindi (wana group lao wa wakuu kanda ya kusini) tulipokuwa tunajadili hayo matokeo. alinionyesha mjadala wao mule na jinsi gani wakuu wa mtwara wa shule tajwa walivyokuwa wanashangaa na kubishia hizo taarifa kwa kuyarusha matokeo yao ya mwaka 2020 (ikumbukwe kuwa mtwara na lindi ni ndugu wenye utani na ushindani kiasi flani hivyo hoja hii iliibua u-mtwara na u-lindi fulani baina yao) .

Nakumbuka mkuu mmoja mle akasema hayo matokeo ni ya 2016 na kuwataka wakuu wajiridhishe kwa kuyaangali matokeo ya shule tajwa ya mwaka 2016 wajionee wenyewe. yule rafiki akadowload matokeo ya shule mojawapo ya 2016 na kweli yalikuwa kama yanavyoonekana haya yanayotembea..... nikaachana nalo kwakuwa haikuwa interest yangu na wala siyo mnufaika na wa kwanza au mwisho lkn pia nikajua kwakuwa iko hivyo basi taarifa hii itakuwa imeshapuuzwa kitambo tu. tukahamia kwenye mada zingine.

Ilipofika usiku nikaingia zangu JF kuperuzi (kama kawaida yangu ya kila siku....ndo starehe yangu kuu). nilistuka kukuta threads za kutosha huko za habari hiyo...kama kawaida, watu wa mtwara walishambuliwa mno kwenye treads hizo na michango; malaya, wavivu, hawana akili n.k. Lindi pia haikubaki salama hapo, watu wake nao waliambulia matusi kibao. hiyo ni JF; kwenye wasomi, wachunguzi na wachambuzi mahili tu.

Leo tena, humu JF, mjadala huo umeendelea kwa kasi.....kila mmoja anasema anavyoweza. wapo waliojitokeza na kutoa taarifa kuwa hiyo habari siyo sahihi bila mafanikio; wakajitahidi hadi kutoa matokeo ya mwaka 2020 ya shule hizo bila mafanikio. mashambulizi ya kusini yakazidi. nilibaki kinywa wazi kwakweli, nilibaki kinywa wazi kwa sababu humu ni JF na siyo kitu kingine.

Mshangao wangu haukuegemea dhihaka na dharau za watu wa kusini, hapana! hilo lipo kila siku humu na ni nadra kupita mwezi usione thread ya kupondea kusini. mshangao ulikuwa kwenye kuvuma na kuaminika kwa hiyo habari hadi humu JF na jinsi wadau walivyokuwa wanajitahidi, kwa umakini mkubwa, kutoangalia au kusikiliza wale waliokuwa wanatoa taarifa sahihi.

Habari ikavuma mno na mkuu wa mkoa akaona isiwe tabu (maana alikuwa anaulizwa sana, bila shaka) akaamua, kitendo ambacho kwangu (labda kwakuwa elimu yangu ndogo) niliona ni cha busara mno, kuwaeleza waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kuwa ameamua KUMUOMBA katibu mtendaji wa baraza la mitihani, KWAKUWA TAASISI YAKE NDIYO ILIYOTANGAZA NA NDIYO YENYE MAMLAKA YA KUKANUSHA KUTANGAZWA KWA ISICHOKITANGAZA. sijajua kama kuna protokali iliyonyooka zaidi ya hiii!

Mkuu wa mkoa huyu, baada ya kutoa taarifa hiyo, ametukanwa vya kutosha tu.....kilaza kama wananchi wake (eti 'anamuamrisha katibu wa baraza' ye kama nani? (ingawa mi nilichokisikia ni kuwa AMEMUOMBA)), nonsensical, anatumbuliwa huyu sasa hivi n.k. ikumbukwe kuwa kuna watu waliyarusha matokeo ya 2020 ya shule hizo tangu jana masaa kadhaa kabla ya mkuu wa mkoa kusema chochote.

Baraza lilipokanusha uvumi huo baadae leo; wachangiaji, kwa makusudi nafikiri, wanasema kuwa 'baraza limefuta na kupanga tena'......dah, HII DUNIA HII, acha tu!

Poleni wana Mtwara na kusini kwa ujumla, mna gundu hampendeki wala hamna sifa ya kusifiwa. kwangu JF naiheshimu sana na ni kipimo kizuri tu cha yanayoendelea. kushadadiwa huku kwa habari fake kama hii na KUTOTAKA KABISA KUGEUZA, ANGALAU KIDOGO, KWA SHINGO ZAO KUUTAKA UKWELI ULIO WAZI KABISA ni ushahidi tosha kwa nikisemacho kwa watu wa kusini,,,,mna gundu. gundu sugu! hebu oneni:-

1. Hakuna yeyote anayezungumza kuhusu kupanda kwa ufaulu wa halmashauri ya Manispaa ya Mtwara.

2. Hakuna yeyote anayezungumzia kushika nafasi ya pili kwa mkoa wa lindi katika matokeo ya darasa la nne 2020.

3. Hakuna yeyote anayezungumza chochote kuhusu kupanda kwa ufaulu wa kidato cha pili kwa mkoa wa lindi kwa miaka mitatu mfululizo.

4. Hakuna yeyote anayezungumza chochote kuhusu kupanda kwa ufaulu wa kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo kwa mkoa wa Lindi.

5. Hakuna yeyote anaesema chochote kuhusu mafanikio haya yaliyoanza kuonekana yanachagizwa na R.E.O ambaye pia ni mtu wa kusini huko huko.....hakuna!

Poleni wanu Mtwara, poleni wanakusini!
 

el nino

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
4,705
2,000
Mlishasema Kaskazini ndio wanaochagua upinzani hivyo wanachelewesha maendeleo.

Magufuli Kanyaga twende, mpaka mnyooke..
 

njoo kwetu

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
648
1,000
Hata kama yale matokeo sio ya mwaka huu.. Lakn bado ki elimu mtwara ipo chini sana.. Ni ukweli usiopindika..

Watoto wa Mtwara wanaangalia wao ni korosho na elimu ya dini... Wengi wao elimu hakuna kabisa..

Wazazi na walezi wengi wa Mtwara hawatilii maanani kuhusu elimu.. Wao wakipata elaza korosha wanachofikiria ni kuongeza wake..

Nadhani unakumbuka kuna kipindi mwanaume flani alipata ela nying za korosho mpaka akamumulia mbuzi wake creti zima la soda...

Mtwara wanarudisha nyuma nchi huu, bila shaka serikali iangalie kwa jicho la pili mkoa wa Mtwara..

Kwani uongo ndugu zangu?
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
886
1,000
Mlishasema Kaskazini ndio wanaochagua upinzani hivyo wanachelewesha maendeleo.

Magufuli Kanyaga twende, mpaka mnyooke..
Kwenye hili hahusiki Magufuli wala CHADEMA, zinahusika chuki, hila na ubinafsi
 

mkandu

Senior Member
Dec 29, 2016
197
250
Umenena ya msingi chief na kama ulivyosema ni UKWELI wasioupenda wengi na hii inachagizwa na FIKRA MGANDO ambazo watu wameaminishwa na kukaririshwa majambo pasi na utafiti km vile.

NGONO ni Mtanzania muhamiaji labda ndio atakaeshindwa kufahamu kuwa kabila lenye sifa ya ngono biashara ndio linaongoza kuwa na wasomi wengi kuliko mengine Tanzania.

Na hii dhana imetiwa nyama zaidi hususan pale panaposemwa kuwa Mabinti wa kimakonde ni mabingwa wa kukatika viuno hili likachukuliwa moja kwa moja kuwa ni wapenzi zaidi wa ngono kumbe wangetafuta source ya hivyo viuno vinavyosemwa wangeweza kunyambua.

BINAFSI suala la matokeo hususan mikoa ya Pwani ya Tz ni jambo linalohitaji wataalam walifuatie kuanzia baraza NEC hadi Mashuleni huko maaana tunaona mikoa mingine watoto madarasa machakavu hadi wengine wanakaa chini madarasani lakini wanatusua ila kwa pwani shule nyingi ziko safi na matokeo yao mara nyingi hayawi safi
 

mkandu

Senior Member
Dec 29, 2016
197
250
Hata kama yale matokeo sio ya mwaka huu.. Lakn bado ki elimu mtwara ipo chini sana.. Ni ukweli usiopindika...
Na haya ndio madhara ya kusema pasi na utafiti hakuna jambo kama hilo la kumnunulia Soda mbuzi lilitengenezwa kisiasa ili kucreate akili ya watz wajue kuna jambo linaendelea Mikoa ya kusini kwa kuwa walilipa kiasi kilichokaendana na mkulima na ili kuhakiki hilo tafuta jina la sehemu ambayo ilifanyika hilo tukio km utapata.

Hayo Masuala ya dini hayaingii akilini maana tunajua ziko Seminary nyingi wanafanya vizuri labda utuletee ushahidi kuwa hizo seminar ni geresha tu hawasomi dini..
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
886
1,000
Umenena ya msingi chief na kama ulivyosema ni UKWELI wasioupenda wengi na hii inachagizwa na FIKRA MGANDO ambazo watu wameaminishwa na kukaririshwa majambo pasi na utafiti km vile...
Yaani, acha tu kiongozi!
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
10,994
2,000
Tangu Hawa necta walipotangaza PEACE LAND ndo shule iliyoongoza taifa Zima niliwapuuza Sana.

Inaonekana hii wizara wanakurupuka mno
 

Dorrlyn

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
1,081
2,000
Umenena ya msingi chief na kama ulivyosema ni UKWELI wasioupenda wengi na hii inachagizwa na FIKRA MGANDO ambazo watu wameaminishwa na kukaririshwa majambo pasi na utafiti km vile...
Waangalie pia lishe ya watoto na wamama wajawazito Kuna vyakula ni akila mama mjamzito na mtoto vinasaidia sana kwenye brain development.
 

njoo kwetu

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
648
1,000
Unataka utafiti gani ?

Kama utafiti angalia shule 10 za mwsho kwa miaka 10 mfululizo angalia zinatoka mkoa gani?

Nadhani huo ni utafiti tosha kbsa
Na haya ndio madhara ya kusema pasi na utafiti hakuna jambo kama hilo la kumnunulia Soda mbuzi lilitengenezwa kisiasa ili kucreate akili ya watz wajue kuna jambo linaendelea Mikoa ya kusini kwa kuwa walilipa kiasi kilichokaendana na mkulima na ili kuhakiki hilo tafuta jina la sehemu ambayo ilifanyika hilo tukio km utapata..
Hayo Masuala ya dini hayaingii akilini maana tunajua ziko Seminary nyingi wanafanya vizuri labda utuletee ushahidi kuwa hizo seminar ni geresha tu hawasomi dini..
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
886
1,000
Na haya ndio madhara ya kusema pasi na utafiti hakuna jambo kama hilo la kumnunulia Soda mbuzi lilitengenezwa kisiasa ili kucreate akili ya watz wajue kuna jambo linaendelea Mikoa ya kusini kwa kuwa walilipa kiasi kilichokaendana na mkulima na ili kuhakiki hilo tafuta jina la sehemu ambayo ilifanyika hilo tukio km utapata..
Hayo Masuala ya dini hayaingii akilini maana tunajua ziko Seminary nyingi wanafanya vizuri labda utuletee ushahidi kuwa hizo seminar ni geresha tu hawasomi dini..
Mimi ndio maana nilijibu tu, 'sawa' maana niliona ananirejesha kule kule. hiyo habari ukifika Masasi watakwambi ilitokea Mtwara, ukifika Mtwara utaambiwa ilitokea mnolela (Lindi). Ukifika mnolela utaambiwa ilitokea Tandahima.........utaishia kusikia hivyo hivyo basi
Tangu Hawa necta walipotangaza PEACE LAND ndo shule iliyoongoza taifa Zima niliwapuuza Sana.

Inaonekana hii wizara wanakurupuka mno
Kwanini mkuu? Ina nini hiyo PEACE LAND?
 

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,698
2,000
habarini wadau!

hakuna kitu nachokipenda dunia hii kama ukweli na haki, hata uwe unaniumiza kiasi gani lakini ukiwa ukweli tu basi roho yangu inabaki kuwa kwatu kabisaaa!...
Mti wenye matunda ndio unaotupiwa mawe,

Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Hawa wakishinda, hatushangai ni desturi yao enzi na enzi,

Mtwara na Lindi ni ishu nyingine, Elimu Haina kipaumbele, lazima tuwaseme tu, Ili wabadilike kama tunavyowasema Wahaya ni Malaya,

Wasukuma ni washamba, Wachaga wanaweza kukutoa roho kwa ajili ya pesa, Lindi na Mtwara wanapenda uvivu na ngono.

Wewe jamaa hujaishi Kusini bado,huko wanathsmini unyago kwa na mabinti kuriko Elimu.

Nenda Masasi,kupata mwanamke ni rahisi Kama kukutana na mmachinga Kariakoo.

Tunawasema Ili wabadirike
 

mcndomba maprosoo

JF-Expert Member
Apr 8, 2013
224
225
habarini wadau!

hakuna kitu nachokipenda dunia hii kama ukweli na haki, hata uwe unaniumiza kiasi gani lakini ukiwa ukweli tu basi roho yangu inabaki kuwa kwatu kabisaaa!...
Hata 2019 Mtwara ilipoongoza kitaifa matokeo ya fomu 6 Hakuna aliyezungumzia. Waache waendelee kusema wakati wenzao wanasonga mbele. Wacha wabaki na simulizi Za zamani.

Karibu wanakutwa ndo maana wanaendelea kupiga kelele. Hata wakati wa Yesu, Wapo ambao hawakuamini km Kuna kitu kizuri kitatoka Yerusalemu. Time will tell
 

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
514
1,000
Poleni sana kusini, nadhani NECTA wamechangia kwa kutozitaja shule kumi za mwisho kama ilivyozoeleka watu wakaamua kutengeneza zao..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom