Poleni Wamachinga lakini hongera Rais Samia kwa uamuzi mgumu uliochukua

Jul 1, 2021
41
95
Machinga wameondolewa nini kitafuata? Kwanza niipongeze serikali kwa zoezi hili zuri. Kwa kweli ilikuwa kero na sijui tungefika wapi na wababe hawa, maana walijaa barabarani kama magari, mitaroni kama maji taka. Haikuwa nzuri hata kidogo. Waliowaruhusu waliwaita wanyonge na mkakubari kuuitwa hivyo.

Pamoja na hatua hiyo nzuri lakini kwanini tuwe na uharaka wa kufanya zoezi hili kwa jinsi hii.

Kwanini tusingetafuta maeneo yenye kukidhi ili watu hawa wawekwe hapo, pesa ipo tena siyo yenu ni tozo yetu ingeweza kufanya hiyo kazi.

Mngeweza sema tozo yenu ya mwezi wa 11 hadi Januari itatue tazo la machinga. Kwasababu ni yetu wananchi, tungeweza kununua maeneo na kuyapanga vizuri, lakini sio huko tunapowatekeleza.

Tena maeneo hayo yangeweza kuingizia taifa mapato makubwa, shida yetu kubwa hatuna watu wanaofikiria na kupanga mambo, wanaamua tu. Jambo la machinga sio la kuamua eti kila mkuu wa mkoa atekeleze agizo.

Hii ni ishu ya kitaifa, sijui Tamisemi na watu wa Mipango Miji wanafanya nini, wangefanya kazi zao kitaaluma hizi lawama zingekuwa hazimfikii rais, wapowapo tu hata hawaongei kitu.

Tuchukulie Dar es Salaam ule uwanja wa Karume wa kazi gani? Pangevunjwa pangejengwa juu na chini alafu wale wa ilala wangeamishiwa hapo kisha pale napo pangejengwa wale wa kariakoo wangeamishiwa hapo, tuna stendi ya mabasi ya zamani ubungo mngewajengea hapo nasikia mnataka kuweka soko la kimataifa.

Eneo la magomeni mlipovunja nyumba mmejenga magorofa, bado kuna nafasi jengeni kituo kizuri cha biashara pale muwaweke. Mwenge mmejenga sijui nini? Mnafukuza watu maelfu mnajenga flemu Mia nne aaah. Rais washughulikie hawa watu. Kuna vitu lazima ukasirike mama.

Tuna shida kubwa ya fikra za kimaendeleo. Mngekuwa mnachukua ata mawazo ya wajinga kama sisi huku mitaani tungefika mbali, wasomi mmeshindwa

Hawa machinga ni mtaji kama vichwa vyenu wahusika vitakaa na kufikiri jinsi ya kuwasaidia basi mtapata mapato makubwa sana

Wachina waliwekewa vikwazo kwa miaka mingi, lakini wingi wa watu wao ikawa mtaji kwao, waliwatumia kuendeleza nchi yao.

Lakini sisi tunawaita walalaoi eti ni wapiga kura wetu wakae wanapotaka, hata juu ya mitaro Kama maji taka.

Poleni machinga lakini hongera mama kwa uamuzi mgumu uliochukua.

Naeatakia sijui Nini Nini kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,654
2,000
Subiri kwanza Marehemu tukimtoa mochwari ndo tutaanza kumuwekea dripu!

Hii serikali hain mkakati wa maana, wa akili na nia ya kutengea bajeti suala hili la wamachinga ili kulitatua.
 

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
5,756
2,000
Walio ondolewa hatuwaiti machinga, labda kama maana ya neno machinga haieleweki.

Machinga anatembea kutoka hapa kwenda pale huyo ndio machnga,JE NI NANI aliezuiwa

kutembeza bidhaa zake hii nchi? wanao (tunao) ondolewa tunawaita wafanyabiashara walio

kaa bila mpangilio sehemu za miji na sehemu ziszo ruhusiwa,Machinga hana jengo wala kibanda.
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,520
2,000
Walio ondolewa hatuwaiti machinga, labda kama maana ya neno machinga haieleweki.

Machinga anatembea kutoka hapa kwenda pale huyo ndio machnga,JE NI NANI aliezuiwa

kutembeza bidhaa zake hii nchi? wanao (tunao) ondolewa tunawaita wafanyabiashara walio

kaa bila mpangilio sehemu za miji na sehemu ziszo ruhusiwa,Machinga hana jengo wala kibanda.
Upo sahihi, nafikiri kulikuwa na evolution ya wamachinga hadi kufikia hatua ya kujenga mabanda, kwa sababu machinga tunayemjua toka kitambo ni yule anayetembeza bidhaa mitaani. Kwa kuwa wamefikia hatua ya kujenga mabanda serikali ni bora wakaona namna ya kuwewezesha hawa wafanyabiashara ndogo ndogo wakawekwa kwenye maeneo rasmi ambayo hayaleti usumbufu kwa wapita njia na kwa utaratibu ambao hauchafui taswira ya kimazingira. Hili nimeliona kwa taxi, unakuta kwenye kituo kimoja cha taxi kuna idadi iliyopangwa ya taxi zinazotakiwa kuegesha hilo eneo.​
 

Mcharo son

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
2,757
2,000
Walio ondolewa hatuwaiti machinga, labda kama maana ya neno machinga haieleweki.

Machinga anatembea kutoka hapa kwenda pale huyo ndio machnga,JE NI NANI aliezuiwa

kutembeza bidhaa zake hii nchi? wanao (tunao) ondolewa tunawaita wafanyabiashara walio

kaa bila mpangilio sehemu za miji na sehemu ziszo ruhusiwa,Machinga hana jengo wala kibanda.
Hao ndio wamachinga ndugu, wamefanya kujiongeza. Hata wewe ukianza umachinga kwanza utatembea, mtaji ukikua utaanza kukaa pahala
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom