Poleni Wakurugenzi mliotoswa, hayo ndio malipo yenu

Galamgendela

Member
Jul 13, 2015
83
36
Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ni wasimamizi wa uchaguzi katika jimbo lililopo ktk halmashauri yake. Octoba 2015 ulifanyika uchaguzi mkuu nchini, ambapo baadhi ya wakurugenzi walishiriki kuchakachua matokeo na kuwabeba wabunge wa chama tawala na kutangaza ni washindi kinyume na maamuzi ya wapiga kura.

Ajabu wale wote waliotangaza wapinzani kuwa washindi wamekwenda na maji, sambamba na hao ambao walijipendekeza kutangaza CCM imeshinda wakati haikushinda ktk majimbo hayo.

Tahadhali!, tunakokwenda serikali itakuwa inaajiri watu kufuata itikadi za siasa. Ukionekana huna kadi ya CCM utaishia kusikia tu utumishi wa umma.

Hii si ishara njema kwa ustawi wa demokrasia nchini.
 
Si kweli. Mbona mimi sina kadi ya chama chochote cha siasa na nadunda serikalini?
 
Ukweli Mtupu nchi inaenda pabaya sana dawa ya yote haya ni KATIBA MPYA!
 
acha majungu kama huna majina bora ukae kimya
Jamani tuache majungu ndio maana mlipiga kelele na kulaani sana sukari ilipoadimika sasa leo imejaa na haina mnunuaji. Mimi nina watoto wangu wapo serikalini na ni Chadema na Cuf wa kikweli kweli sababu ni viongozi kwenye vyama vyao, sijasikia wakilalamika kwamba wanatengwa au kunyanyaswa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom