Poleni waandishi na Polisi, hongereni wanasiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Poleni waandishi na Polisi, hongereni wanasiasa

Discussion in 'Utambulisho (Member Intro Forum)' started by SAUTI KUTOKA NYIKANI, Sep 13, 2012.

 1. S

  SAUTI KUTOKA NYIKANI New Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp]NASHINDWA kuyazuia machozi yangu yanapobubujika na kudondoa kwenye kope za macho yangu hasa ninapokumbuka kifo cha Mwandishi Daud Mwangosi na watanzania wengine waliokufa na kujeruhiwa kwenye mikutano ya kisiasa hapa nchini kwetu Tanzania. [/FONT]

  [FONT=&amp]Nianze kwa kutoa pole kwa wananchi wote wakiwemo wanataaluma wote wakiwemo waandishi wa habari na askari Polisi Tanzania walioumia na wanaotarajiwa kuumizwa katika mikutano ya wanasiasa wetu kupitia ‘’Chama cha Migomo na matatizo yasiyokwisha’’ huku Polisi wakikosa mtu wa kuwasemea na kuendelea kuumizwa na kutukanwa majukwaani.[/FONT]

  [FONT=&amp]Sitaki kuorodhesha orodha ndefu ya matukiom ya kisiasa yaliyowahi kutusikitisha wengi hasa wananchi na askari polisi wanapoumizwa na hata vifo kutokea kutokana na ukaidi wa wanasiasa wenye uchu wa madaraka hapa nchini.[/FONT]

  [FONT=&amp]Nawapa ‘’Hongera’’ sana wanasiasa mnaaona ni fahari mioyoni mwenu kuona damu za watanzania zinamwagika na wengine wakipa ulemavu katika mikutano yenu ili tu ninyi mpate nafasi ya upangaji pale Ikulu. Hongereni sana lakini mjue kuwa damu hizo zitakuwa juu yenu na watoto wenu.[/FONT]
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,329
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Karibu sana JF.
   
 3. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,967
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Pole. Karibu sana.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,054
  Likes Received: 3,804
  Trophy Points: 280
  Karibu sana japo una majonzi.
   
Loading...