Poleni sana wamachinga, hiyo ndiyo CCM haijawahi kubadilika

Yaani hawa wanovunjiwa na kusema hawajui kitu ni wapuuzi, inabidi wavijenge na wawasubiri hao wanaobomoa...

Watu Mia wanatosha kabisa kuishikisha adabu serikali
 
Hapa naona busara inapaswa itumike, kwanza kwa kukutanana na viongozi wa Machinga ili kuongelea kuhusu kuhamishiwa katika maeneo mapya watakayopangiwa. Pili bado wapewe muda wa kutosha ili waweze kujipanga kuondoka, ikiwezekana mpaka ifikapo mwisho wa mwaka.
 
Ajira huto,,utaratibu huufuati na kwa bahati mbaya hata vyama vya upinzani haviwasaidii
 
Ni TANZANIA pekee kila mtu hata mwenye uwezo anajiita machinga!
Kwa kilichofanyika wengi hawatapenda ila ukweli ni kwamba lililofanyika ni sahihi japo linaumiza kwa upande mmoja ila unapokuwa machinga kuna limit yake unakaa umachinga miaka ishirini ww mtaji wako huwa haukuwi?

Angalia wageni wanakwenda na kutoka airport wanapokelewa na vibanda huku wakijua Tz ni nchi ya uchumi wa kati hilo nalo ni sawa?

Mji lazima upangwe watu waishi kwa sheria na sio mazoea
Watakuja wa kulaumu ambao wao yawezekana ndio wawezeshaji wa hao machinga/ wanaowapa mizigo kwa kukwepa kodi ,na hili ndo kundi kubwa nyuma ya pazia

Nb;kupanga ni kuchagua miji yote Tz lazima isafishwe na ipangwe upya
Mie nilizoe kuwa ukisikia machinga Basi ni yule anazunguka na bidhaa kidogo,pengine heleni,nguo mitumba nk.Lakini siku hizi unakuta machinga kajenga Banda kaweka bidhaa Kama Duka vile lakini naye Ni machinga
 



My Take
Naona serikali ya Samia imeanza kufanya mambo kama wachawi, inategea wamachinga wamelala, bila jicho la media inaenda kuvunja vibanda vyao

Huu siyo uungwana hata kidogo. Hawa watu walitoa shilingi elfu ishiriniishirini zao, mkawaahidi kufanya biashara popote, leo kwenda kuwavunjia usiku wa manane siyo uungwana hata kidogo.

Najua lengo ni kuondoa kumulikwa na jicho la wananchi kwenye operesheni yenu ya kikatili na pia ili wamachinga wasijimobilize kuresist ndiyo maana mbavamia usiku wa manane kimya kimya na kuwavunjia. Hii siyo heshima kabis kwa wananchi, this is wrong!
20000 ndio izuie serikali kufanya Mambo yake? Waulize Kimara waliobomolewa nyumba zao
 
Kwa hiyo ccm haina directory?inajiongoza kama mbuzi asiye na kamba!
Hivi unajua maana ya demokrasia?

Ila si shangai na ndio maana kwa demokrasia yetu,wanasiasa hawapo huru kwenye vyama vyao, wakiwa na mitizamo tofauti CCM utasikia "hana adabu....... mtovu wa nidhamu.......".

Ukiwa upinzani unaitwa "msaliti........ mara kanunuliwa ".

Yaani demokrasia yetu ndani ya hivi vyama sizani kama kuna mgongano wa mawazo kwani baadhi wa viongozi ambao wanajifanya miungu watu hawapendi kupingwa.

So kuwa ndani ya hivi vyama haina maana kwamba hautakuwa na mtizamo binafsi.
 
Kwanini uwavunjia unataka wakafe maana hao sio matajiri sasa kama kila kitu kimevunjwa

Wanaishi je? Inamaana wewe unakaa upande wa serikali utakuwa unashida kwenye ubongo

Au umepata uteuzi ndo maana unapopo yaani unaropoka ropoka sana!

Kwani hilo eneo linawafanya nini

Machinga walikuwa wanajipatia maisha yao bila shida

Subiri haya majimbo yote ya majiji na mijini yote niya upinzani

Ccm inarudi kule kule unatesa wananchi kisa umerithi urais kwa kufa rais waliomtegemea


Unataka kuniambia kuwa matajiri wanao iendesha serikali ndio wataiweka madarakani


Hao wamachinga ndio watanzania wengi tajiri huwezi mkuta huko mamalishe na machinga ndio wanateseka
Kuna mijitu ikihemkwa haina hata muda wa kutafakari. Yanaweza kuhamaki na kitu ambacho wala hayajelewa. Haya tunayaita mabongolala.mara nyingi hatuyasaidii, unayaacha kama yalivyo.Unayajulisha tu kuwa ni mabongolala.
 
Tena Koma kama u



Tena koma kabisa kumtaja JPM hiyo ni habari nyingine nyie endeeni na mambo yenu wakati sisi tukiomboleza!
Unaomboleza wewe na nani?huyu yupo kuzimu
JamiiForums922358689.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom