Poleni sana wamachinga, hiyo ndiyo CCM haijawahi kubadilika

Ngwakwiii

Member
Dec 6, 2019
92
125
Tatizo wamachinga wanajiweka kwenye kundi la vulnerable kama wasiojiweza wazee na watoto. Wanataka serikali iwapatie sehemu za biashara, iwape mitaji, wasifuate sheria zozote, wasilipe kodi , hata akiwa na uwezo wa kukodi fremu hataki
Ni TANZANIA pekee kila mtu hata mwenye uwezo anajiita machinga!
Kwa kilichofanyika wengi hawatapenda ila ukweli ni kwamba lililofanyika ni sahihi japo linaumiza kwa upande mmoja ila unapokuwa machinga kuna limit yake unakaa umachinga miaka ishirini ww mtaji wako huwa haukuwi?

Angalia wageni wanakwenda na kutoka airport wanapokelewa na vibanda huku wakijua Tz ni nchi ya uchumi wa kati hilo nalo ni sawa?

Mji lazima upangwe watu waishi kwa sheria na sio mazoea
Watakuja wa kulaumu ambao wao yawezekana ndio wawezeshaji wa hao machinga/ wanaowapa mizigo kwa kukwepa kodi ,na hili ndo kundi kubwa nyuma ya pazia

Nb;kupanga ni kuchagua miji yote Tz lazima isafishwe na ipangwe upya
 
Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,256
2,000
lqkini huwezi kuvunja jiji zima na mali zikiwemo..siwaliwapa mwezi mmoja..mama samia atie ajira kwa malaki ya graduates ana kama hawezi basi aache watu wajitafutie riziki..utqratibu uliotumika Dar ni wakikatili sana kwa watu masikini..Hii Tabia ilikuwepo wakati wa kikwetwe..mgambo kuwanyanganya machinga mali zao
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,245
2,000
lqkini huwezi kuvunja jiji zima na mali zikiwemo..siwaliwapa mwezi mmoja..mama samia atie ajira kwa malaki ya graduates ana kama hawezi basi aache watu wajitafutie riziki..utqratibu uliotumika Dar ni wakikatili sana kwa watu masikini..Hii Tabia ilikuwepo wakati wa kikwetwe..mgambo kuwanyanganya machinga mali zao
Anacheza na moto!
 
Omary - Msamalia

JF-Expert Member
Jan 19, 2020
814
1,000
Yaani hawa wanovunjiwa na kusema hawajui kitu ni wapuuzi, inabidi wavijenge na wawasubiri hao wanaobomoa...

Watu Mia wanatosha kabisa kuishikisha adabu serikali
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,336
2,000
Hapa naona busara inapaswa itumike, kwanza kwa kukutanana na viongozi wa Machinga ili kuongelea kuhusu kuhamishiwa katika maeneo mapya watakayopangiwa. Pili bado wapewe muda wa kutosha ili waweze kujipanga kuondoka, ikiwezekana mpaka ifikapo mwisho wa mwaka.
 
Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,256
2,000
Ajira huto,,utaratibu huufuati na kwa bahati mbaya hata vyama vya upinzani haviwasaidii
 
Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
16,692
2,000
Ni TANZANIA pekee kila mtu hata mwenye uwezo anajiita machinga!
Kwa kilichofanyika wengi hawatapenda ila ukweli ni kwamba lililofanyika ni sahihi japo linaumiza kwa upande mmoja ila unapokuwa machinga kuna limit yake unakaa umachinga miaka ishirini ww mtaji wako huwa haukuwi?

Angalia wageni wanakwenda na kutoka airport wanapokelewa na vibanda huku wakijua Tz ni nchi ya uchumi wa kati hilo nalo ni sawa?

Mji lazima upangwe watu waishi kwa sheria na sio mazoea
Watakuja wa kulaumu ambao wao yawezekana ndio wawezeshaji wa hao machinga/ wanaowapa mizigo kwa kukwepa kodi ,na hili ndo kundi kubwa nyuma ya pazia

Nb;kupanga ni kuchagua miji yote Tz lazima isafishwe na ipangwe upya
Mie nilizoe kuwa ukisikia machinga Basi ni yule anazunguka na bidhaa kidogo,pengine heleni,nguo mitumba nk.Lakini siku hizi unakuta machinga kajenga Banda kaweka bidhaa Kama Duka vile lakini naye Ni machinga
 
Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
16,692
2,000

My Take
Naona serikali ya Samia imeanza kufanya mambo kama wachawi, inategea wamachinga wamelala, bila jicho la media inaenda kuvunja vibanda vyao

Huu siyo uungwana hata kidogo. Hawa watu walitoa shilingi elfu ishiriniishirini zao, mkawaahidi kufanya biashara popote, leo kwenda kuwavunjia usiku wa manane siyo uungwana hata kidogo.

Najua lengo ni kuondoa kumulikwa na jicho la wananchi kwenye operesheni yenu ya kikatili na pia ili wamachinga wasijimobilize kuresist ndiyo maana mbavamia usiku wa manane kimya kimya na kuwavunjia. Hii siyo heshima kabis kwa wananchi, this is wrong!
20000 ndio izuie serikali kufanya Mambo yake? Waulize Kimara waliobomolewa nyumba zao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom