Poleni sana mliomwaga damu kwa ajili ya CHADEMA, ukweli mmeuona!

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
8,119
Points
2,000

meningitis

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
8,119 2,000
Rubbish.......

Tambua mkuu Meningitis, waliomwaga damu katika Chadema, wamefanya hivyo kutokana na udikteta wa Mwenyekiti wako Jiwe......

Kuna aliyemwaga damu zaidi ya Jiwe katika nchi hii??
Waliomwaga damu ni kipindi cha JK..wewe ulikuwa hujazaliwa
 

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
8,119
Points
2,000

meningitis

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
8,119 2,000
Tutaendelea kumwaga damu chini ya Kamanda Mbowe,uovu mnaomfanyia Mbowe kupitia Kubenea na komu uko hadharani unajulikana
Maoni yangu yana base kabla hata Kubenea hajaingia Chadema...tuliza mzuka unisome vyema...mimi sio mtu wa kufuata mafuriko
 

1000 digits

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Messages
4,429
Points
2,000

1000 digits

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2012
4,429 2,000
Chadema kimebaki kama TLP.

Mbowe anafikiri anafiki kura mil.6 zilitoka Machame pekee.

Anampiga vita mpaka Mseminarist msomi Anthony Komu. Kweli?!! Mbowe anataka Chama kibaki na Bendera Fuata. Upepo.

Hivi haoni kuwa Muda sio Mrefu Chadema kitaifuata CUF?

CUF ilipokua na Maalim Seif Akiwa kama Makamu wa Rais Zanzibar ilipata Heshima kubwa Wajinga wengi wasiojua siasa za kuongoza nchi kama Chama wakaanza kuwaita CUF kama CCM B. Lakini Kisiasa kwenye nchi za Kiafrika ilikua ni Advantage kubwa sana.

Hata uwepo wa Sumaye na Lowassa kisiasa ilikua ni advantage kubwa. Duniani Kote Vyama vinaundwa na kuongozwa na maveterani waliowahi kuwa katika serikali.

Huwezi kutegemea machokoraa from ni where waachiwe nchi kwa sanduku la kura labda kwa kugeuka kuwa mbwa koko na kuingia msituni.

Chadema imetumia ujinga wa Mwenyekiti kinganganizi kuua chama wakidhani kuwa kwa sasa wataweza tena kurudi kwenye siasa za kiharakariti za vyuo. Kwanza hakuna Msomi anayemuunga mkono Mbowe. Wasomi walikua wanavutiwa na Umahiri wa kujenga Hoja wa Dr. Slaa. Hata kabisa Katoliki lililojaa wasomi limeshaona kuwa Mbowe hana nia ya kujenga Demokrasia ndio maana limejitenga naye na kujiweka pembeni.

Bakwata imejitenga na Mbowe, CUF inejitenga na Mbowe, ACT haipo na Mbowe, Wachaga wengi wamejitenga na Mbowe wamebaki wale wa ukoo wake ndio maana hata wenyeviti wa kijijini kwake wakeshamchoka.

Kabisa la KKKT na Makanisa ya kipentekoste akiwemo Kakobe wamejitenga na Mbowe baada ya kugundua kuwa hana dira wala lengo Jema na nchi hii zaidi ya Uenyekiti wake.

Watu wanatekwa na kuuawa kwa ajili ya Chadema lakini Mbowe anachopigania kwa kila mbinu ni Uenyekiti wake.

Hivi katika sayansi ya siasa Mbowe haoni kabisa kuwa Summaye alikua na umuhimu mkubwa kabisa ndani ya Chadema mpaka akatumia uhuni kumhujumu kisiasa?

Hivi huo uenyekiti tu aliorithishwa na mkwe wake bila hata kushindanishwa kwa hoja anaungangania kwa kiwango hicho angeshinda Urais 2005 ingekuaje ?

Summaye alinyanyasika sana kwa sababu ya Chadema halafu leo anafanyiwa vitimbwi bila kujali kuwa ni mtanzania.

Niwaombe viongozi wa dini na wanaharakati wote kujitenga kabisa na Siasa za Mbowe na Chadema ya Mbowe kwa sababu anayoyalalamikia toka kwenye serikali ya CCM ni yale yale anayoyatenda tena kwa uovu na ubaya zaidi.

Analalamikia Demokrasia lakini ameua Demokrasia ndani ya Chadema.

Mbowe analalamikia tume huru ya Uchaguzi lakini ameua kabisa Uchaguzi huru ndani ya Chadema.

Analalamikia Uhuru wa kujieleza lakini amewapiga marufuku Anthony Komu na Kubenea kuzungumzia chochote kuhusu Chadema kwa sababu tu ana hofu ya watu wenye uwezo kujijenga na kukubalika kuliko yeye.

Mbowe analalamikia hofu na vitisho toka kwa serikali ya CCM lakini Mbowe amekua ni kitisho kikubwa sana watu wanahofu hata ya kuchukua form za Uenyekiti na wakijaribu wanafanyiwa hila za kila namna na genge la vijana wake.

Mbowe analalamikia sheria ya manunuzi kutofuatwa lakini yeye hafuati kabisa sheria ya manunuzi.

Mbowe analalamikia uwazi kwenye serikali lakini ndani ya chama chake kila anayehoji anaitwa msaliti.

Watanzania wa Makabila yote ,Dini zote , Mashirika yote ya Haki za binadam ni wakati sasa wa kujitenga kabisa na Mbowe mtu anayeongea kile asichokiamini na kukilalamikia kwa wengine lakini kwake ni sawa.

Huyu ni kikwako katika harakati za kupigania Demokrasia.

Mbowe anapigania Uenyekiti wake kitaifa lakini sio Taifa hili.

Mbowe anatumia kila mbinu kuunganisha wanachama dhaifu wanamuogopa na kumwona kama Mungu mtu ndani ya Chama huku akishindwa kabisa kujenga maridhiano ya Kisiasa ndani na nje ya chama chake.

Mbowe analalamikia kutengwa kwa wapinzani kwenye masuala ya kitaifa lakini Mbowe na genge lake wanawatenga wanachama wanaoonekana kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiuongozi ndani us chama Chake.

Je, huyu Mbowe anastahili kuungwa mkono katika harakati za kupigania haki na Demokrasia katika taifa hili.

Je, kuna taasisi,dini, Chama,NGO'S au mwanaharakati aliye tayari kupata misukosuko kwa ajili ya Mbowe?

Je,serikali ipo tayari kuona Mbowe akiendelea kulaghai watu na kuhamasisha siasa za kisanii kwa lengo la kujenga chama cha Ukoo kwa kodi za watanzania?

Hapana ,watanzania wate tujitenge na Mbowe na Siasa zake.
 

Forum statistics

Threads 1,391,998
Members 528,520
Posts 34,095,131
Top